Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Wanawake mnaojenga nyumba kwa siri bila mwenza kujua huwa mnamaanisha nini?

Mimi namfahamu mwanamke aliyefanya hivyo baada ya kuchoka visa vya mume kuchepuka na manyanyaso.

Sababu yake ilikua kufanya maandalizi ya kutengana na kuhakikisha watoto wake hawakosi pa kuishi.
Hao watoto aliwazaa peke yake!?mume wake hawamhusu!!?
Ina maana huyo mwanamke alijilala mwenyewe ndio akazaa au watoto sio was huyo mume!!?

Funguka zaid wenye akili timamu tuelewe!!
 
Nataka kujua ndio ujanja,umaarufu,ukisasa, usomi,kiburi,majigambo,majivuno,dharau,umwamba au!!?

Na tena wakati unafanya hivyo upo kwako na mlishajenga pa kuishi,na mwenza anakushirikisha Kila jambo la kifamilia analofanya!

MSAADA TAFADHALI,sio kwamba natumika baadae nitangulizwe baada ya mpangokazi wake wa ukwasi kukamilika!

Maoni yenu nitayazingatia!

Kataa ndoa mje pole pole!!

Na wale waume wenza mliopo humu mje pole pole nawajua!
Maana yake ni kuwa ndoa ndoano. Muda wowote samaki anavuliwa kutoka majini anakuja nchi kavu. Huko nchi kavu kama hajaandaa mazingira ataishije?
 
Wanajiahami siku mkiachana vitu vyake visiwekwe kwenye mgao.

Jirani yetu anajenga tokea muda ila nyumba bado haijaisha huku mkewe tayari amejenga na nyumba imeisha kaweka wapangaji.
Mume hajui ila majirani tunajua.
Kwahiyo vya mwanaume ndiyo viwe vya mgao? Cha ajabu pamoja na kujenga nyumba kwa siri lakini ikifika hatua ya kuachana mwanamke atataka mgawane naye mali zako hata nyumba pia.
Ile roho ya shetani kutoka pale eden bado mnayo mpaka sasa hivi
 
Mkuu ndio maana mwanamke alipaswa kukaa nyumbani azae na kulea watoto. Kwa sababu tunakiuka sheria za mungu ndio maana haya yanatokea.
Inawezekana wakati unaanza maisha nae hakuwa na kazi Sasa alipata ajira mikononi mwako Sasa utamkataa kisa ameajiriwa!!?na mlianza mambo masomoni huko na wewe ndio ukaajiriwa!l Yeye bado!!!?
 
Ni kama wanaume mnavyofanya mambo yenu kimya kimya basi na wanawake ni hivyo hivyo. Kuna dada alienda kununua kiwanja mahala hakumuambia mumewe kumbe mumewe nae katafuta kiwanja eneo hilo hilo bila kujua na hakumuambia mkewe. Mbeleni wamekuja kujua wamenunua viwanja eneo moja na kila mtu kamficha mwenzake.
 
Hao watoto aliwazaa peke yake!?mume wake hawamhusu!!?
Ina maana huyo mwanamke alijilala mwenyewe ndio akazaa au watoto sio was huyo mume!!?

Funguka zaid wenye akili timamu tuelewe!!
Wanaume wanaongoza kwa kutelekeza watoto wao, hata wale waliozaa ndani ya ndoa kabla ya kutengana, fuatilia kesi ustawi wa jamii na mahakamani ziko tele. Mbali na kesi, kuna ushuhuda wa watu wengi hata humu JF ambao wamelelewa na mama zao bila mchango wa baba zao.

Ingekua hakuna hiyo tabia ya kuachana na kukacha malezi ya watoto, nafikiri baadhi ya wanawake wasingeona sababu ya kufanya maandalizi kama hayo.

PS:
Kuna wanawake wabinafsi wanafanya hivyo kwa maslahi yao ila siyo wote wengine hali zao za maisha zinawalazimu.
 
Back
Top Bottom