Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Kiasili na kwa utafiti wanawake wanapenda au wanajisikia faraja wamekamilika wanapokandamizwa kimfumo dume zaidi kuliko wakiwa diplomatic zaidi yaani laizer affair hivi kuwa kuachwa huru zaidi wajitawale. Zile ndoa ambazo mwanaume ni mbabe na ana kipato nyingi hazivunjiki tofauti na hizi za mwanaume mpole, muungwana na kamwachia huru mkewe. Wanawake wanapenda kutawaliwa na sio kujiongoza. Thus ndoa za zamani zilikuwa zinadumu.
Unaweza vipi kumcheat, kumletea dharau au jeuri mwanaume mbabe, saikolojia yao tu inakataa wakajikuta wanakaa kwenye mstari. Ukiwa na elimu na dini huwezi kuwa dikteta.
Kwahiyo kwenye ndoa hamnaga 50 kwa 50?
 
Hakuna mwanaume anayemfokea mwanamke mpole na asiye na mdomo. jiangalie Sana. anajihami kwa kukufokea baada ya kugundua una kiburi au mdomo pistol.

Mie sio mwongeaji Wala mpigaji. Ila mwaka huu nimeanza tabia ya kumfokea wife. amebaki anaduwaa kuwa miaka 16 yote sijawahi mfokea, imekuwaje Tena? namjibu tu achague mawili, kutuliza kimdomo chake au nimzibue mateke kabisa.

wanawake nanyi mnatubadilisha sana
Sidhani. Wapo wanaume wengi wenye tabia hiyo, hata mke awe mpole namna gani. Watu kama hawa huitwa ''bullies'' kwa kiingereza. Pia kuna wanawake wenye tabia hii kwa waume zao au watoto.
 
Itakua ana mambo aliyopitia kipindi cha nyuma ambayo yamemuathiri kisaikolojia, pia inaweza ikawa ni mfumo wa maisha ya familia aliyokulia udogoni umemfanya awe hivyo.
 
mwambie akuheshimu we siyo mtoto wake sema kama kila siku unakaa nyumbani hiyo nayo ni changamoto
 
Kwahiyo uliamua kuja JF kunianzishia uzi? Haya nimekuelewa sitakufokea tena lakini na wewe tatizo lako 6*6 unakuwa gogo
Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana mie nimesahau mafundisho ya shangazi, wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anaye fokafoka? Maana mimi naona yamenifika hapa!

Huyu mwanaume amenizidi umri kwa miaka saba, sasa sijui ananichukulia mimi mdogo yake! Yaani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho kali, haijalishi kuna dada wa kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu.

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda, kugombana nae siwezi atanibonda nife.

Naombeni mbinu jamani nifanyeje, yamenifika kwa koo mwenzenu?!
 
Back
Top Bottom