Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Nimeeleza mengi sana kwenye ushauri !
1. KAMA Unafokewa kwa kukosea jirekebishe na muahidi mumeo kwamba utajirekebisha kuondoa mafoko na thibitisha mabadiliko kwa vitendo, ongeza USIKIVU, uliza usipoelewa, usifanye kama hujaelewa.
2. Mbinu ya pili angalia mafoko kama yanatija kama ukiona ni utata na ubabe tu usioisha basi ONDOKA hukuzaliwa naye siku atakuchinja huyo
3. Mbinu ya tatu Kama unataka ubaki ila huioni furaha kwa Huyo mume basi CHEPUKA kisomi kwani bei gani eboo! Unampanuliaje mtu anakufokea fokea c bora ukachepuke tu

Za kiambiwa changanya na zako
Astaghifilullah!
 
Itabidi ujifunze ndondi, ndoa za sasaiv zataka kujipanga kwa mbinu zote[emoji23] uwe mkimya, mwenye busara hekima, mchapakazi, mwanasaikolojia, mjasiriamali, mwana mieleka, mwenye kidomo,, kahaba kitandani, mlezi na mzazi,, kazi tuko nayo walahi
Kungwi, the legend.....hadi raha
 
Si tutafika mbinguni tumechoka sana? 😀😀

Ila kama ni kweli anachokisema mama K, basi yuko katika trouble kubwa sana. I'v been there zamani kidogo, sema tu kwa leo nasikia uvivu kuandika. Uzuri mimi haikua ndoa ikawa rahisi kufanya maamuzi ya kumove on na kueleza kuwa nimeshindwa. Kila mtu ana anachoweza kuvumilia, mimi siwezi kabisa kuvumilia kufokewa kila saa.

Pole mama K, ongea nae sana.
Yani Kuna wanaume wasumbufu jamani,,, Sasa mtu si ajue kuwa stress za nje hazihusiani na ndani?
 
Habari zenu jamani.

Naomba kuuliza, inawezekana mie nimesahau mafundisho ya shangazi, wanawake wenzangu mnawezaje kuishi na mwanaume anaye fokafoka? Maana mimi naona yamenifika hapa!

Huyu mwanaume amenizidi umri kwa miaka saba, sasa sijui ananichukulia mimi mdogo yake! Yaani nikikosea kitu kidogo atafoka huku ananikata jicho kali, haijalishi kuna dada wa kazi karibu, ni atafoka tu! Huyo dada wa kazi nae anafokewa hadi namuonea huruma mtoto wa watu.

Huwa nanyamaza kisha namtafutia pose zuri namwambia anavyonikwaza ila routine ni ile Ile, nahisi kukonda, kugombana nae siwezi atanibonda nife.

Naombeni mbinu jamani nifanyeje, yamenifika kwa koo mwenzenu?!
Pole sana, binadamu tunatofautia sana, mimi binafsi ni mkimya sana hata kwenye makosa ya dhahiri hasira zangu hunielekeza kwenye ukimya, matokeo yake naonekana boya!
Cha kufanya endelea kutafuta nafasi nzuri ya kumwambia vile unakwazika na hio tabia yake, hata kama itachukua miaka mingi kubadilika atabadilika tu, akili ya binadamu imeumbwa na hali ya kujifunza na kubadilika kulingana na wakati na mazingira, so ipo siku atabadilika.

Pia mtu wa namna hiyo ikiisha mjulia basi wewe timiza wajibu wako kadiri ya dhamiri yako hata kama ataongea vipi wewe puuza tu usitarajie kupata amani kutoka kwake ilimradi tu wajibu wako unautekeleza. Itakusaidia sana kupata amani nje ya binadamu mwenzako kwa binadamu mwenzako tarajia makwazo tu.
 
Kama hana kero nyinginezo mzoee jitahidi kupuuza tu,, Tena siku nyingine akifoka jililishe kwa machozi maana wa hivyo wajuzi wa kubembeleza hatari na akiona chozi anajua umeumia pengine atapunguza,,
Ushauri mzuri sana trust me, kila akifikiria akikufokea utalia atapunguza ila anavyofoka na anakuona umekausha anahisi una jeuri.. Its kinda inferiority complex
 
Ushauri mzuri sana trust me, kila akifikiria akikufokea utalia atapunguza ila anavyofoka na anakuona umekausha anahisi una jeuri.. Its kinda inferiority complex
Hata mie nimewaza hivyo kuwa akifoka ajifanye mnyonge, huenda ikasaidia, nae alijibu kuwa alikuwa akilia na haikusaidia chochote,,
Kwa ninavyojua wanaume aina hii wengi wao wanapenda kunyenyekewa sana zaidi ya kawaida,, kupigiwa magoti, ujinyenyekeze kama unasujudu, ndo wale wanaopenda kunawishwa miguu na hii wanawake wa Tanga wanaiweza na ndipo hapo wanamwagiwa sifa kemkem,,
siku akiwa ktk mood nzuri atumie hapo kumueleza anavyokwazika,
 
Kwani kufoka ameanza mwaka huu?? Kama alikuwa hivyo tangu uchumba wenu na ukakiri kumtumilia mpaka kifo kiwatenganishe jikaze, maana katika zile shida ulizosema Kwa midomo yako bila kulazimishwa na ntu kwamba utavumilia ni pamoja na hiyo
 
Achana na hiyo ndoa, kwa nini? Mimi ni mwanaume, sikiliza:

1. Mwanamke akigombezwa hawezi kuwa na mapenzi ya hiyari.

2. Mwanaume anaweza asielewe na akikosa mapenzi ugomvi pale pale.

3. Usipokuwa na mapenzi naye atawaza unabated mtu nje ya ndoa - ugomvi Unaendelea.

4. Ataanza toka nje ya ndoa kwa sababu anaitaji mapenzi!

Achana naye! Hiyo cycle huishia kwenye mauaji
Aachane naye aende wapi? Kamzidi miaka Saba kiufupi anamuona kama Mtoto, hapo cha msingi awe mtii na mnyenyekevu hiyo hali itaisha, akiondoka hamna waoaji si unaona singo Maza shuruba wanazokutana nazo
 
Hata mie nimewaza hivyo kuwa akifoka ajifanye mnyonge, huenda ikasaidia, nae alijibu kuwa alikuwa akilia na haikusaidia chochote,,
Kwa ninavyojua wanaume aina hii wengi wao wanapenda kunyenyekewa sana zaidi ya kawaida,, kupigiwa magoti, ujinyenyekeze kama unasujudu, ndo wale wanaopenda kunawishwa miguu na hii wanawake wa Tanga wanaiweza na ndipo hapo wanamwagiwa sifa kemkem,,
siku akiwa ktk mood nzuri atumie hapo kumueleza anavyokwazika,
Na kucha amkate mwambieni awe soft Sio softness inapatikana tu Wakat wamahanjamu chumbani hivi mnajua hata wanaume wanapenda kudekezwa sometimes, aweke kichwa chake kwenye mapaja ya mkewe huku sotori na vijisifa vya hapa na pale vinaendelea atafoka hapo kweli??? Hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Ungetuambia ndoa Ina miaka mingapi, jekabla ya hapo alikuwa anakufokea ya laa, nakama sivyo Basi Kuna namna anakuchukulia poa, na kwa kiasi Sasa haoni thamani yako wewe, vumilia
Huyu sidhani kama ana ndoa maana inaonesha mabaharia wanapishana tu 😂😂😂!!! Kila wakati case mpya
 
Na kucha amkate mwambieni awe soft Sio softness inapatikana tu Wakat wamahanjamu chumbani hivi mnajua hata wanaume wanapenda kudekezwa sometimes, aweke kichwa chake kwenye mapaja ya mkewe huku sotori na vijisifa vya hapa na pale vinaendelea atafoka hapo kweli??? Hakuna mkate mgumu mbele ya chai
Yataka moyo Sana kumdekeza mtu anaekufokea ovyo,,
 
Gubu tu hilo analo,Rudi tena kwa kungwi wako bibie akufundishe kumpa yotee..Gubu lote litakwisha..
 
Nunua kiredio kile cha bluetooth, hakikisha akiwa around unawasha mziki sauti ya juu usimpe chance ya kukupigia makelele....unafanya kazi zako huku unaimba imba tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huko kwenye kumpea hafoki, kwanza sijawahi kumnyima toka anioe....ye mwenyewe anakiri hilo.
Ila hebu fikiria labda namtengea chakula, bahati mbaya wakati naweka glass mezani nikosee hesabu glass ijigonge, jamani atafokaaa, Yani atanifokea Kama mtoto.
ana gubu huyo, mvumilie tu
 
Back
Top Bottom