Wanawake mnawezaje kuishi na mwanaume anayefokafoka?

Kwahiyo kwenye ndoa hamnaga 50 kwa 50?
 
Sidhani. Wapo wanaume wengi wenye tabia hiyo, hata mke awe mpole namna gani. Watu kama hawa huitwa ''bullies'' kwa kiingereza. Pia kuna wanawake wenye tabia hii kwa waume zao au watoto.
 
Itakua ana mambo aliyopitia kipindi cha nyuma ambayo yamemuathiri kisaikolojia, pia inaweza ikawa ni mfumo wa maisha ya familia aliyokulia udogoni umemfanya awe hivyo.
 
mwambie akuheshimu we siyo mtoto wake sema kama kila siku unakaa nyumbani hiyo nayo ni changamoto
 
Pole mkuu..Akiwa anafoka foka..Nenda kwake then anza kumpa romance. .

Kila akifoka mnyamazishe kwa romance then mnongoneze kwa kumwambia mume wangu kipenzi naomba unisamehe ila nieleweshe taratibu nitakuelewa
 
Kwahiyo uliamua kuja JF kunianzishia uzi? Haya nimekuelewa sitakufokea tena lakini na wewe tatizo lako 6*6 unakuwa gogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…