Wanasemaga hakuna jipya chini ya jua...
Historia humfanya binadamu wa leo na kesho kuishi aidha kuepuka yaliyotokea nyuma yasimpate, au azidi waliyofanya kizazi cha nyuma au ashangaze kwa kuvumbua mapya.
Wanawake wa kizazi cha tatu hadi cha nne nyuma ya sasa pia walikuwa na namna ya kujikwamua kiuchumi kwa malengo tofautitofauti na bado waliishi na waume zao. Ukiona mtu anafanya jambo nje, kama hakushawishiwa basi lilianza kama wazo au ni moja ya kutatua matatizo yanayomkumba.
Mume mlevi na mhuni anawatoto kila mtaa na nyumbani kwake haijulikani wanakula nini wanavaa nini, mama ndo ajiongeze apike mataptap au mama ntilie watoto wale wasome. Wengi kwenye jamii yetu walilelewa hivi halafu wamekuwa watuwazima wanasahau walikotoka wanafanya ushuzi uliofanywa na wazazi wao kwa kuwadhihaki wenza wao kinyume na mmoja wa mzazi wake alivyohangaika kumlea.
Kuna watu wamelelewa kwa shida, baba ni.mwanajeshi mshahara ukitoka unaisha baada ya siku 3 sikuzote yuko njwiii, mama akijiongeza afanye kamradi watoto wale anaiba hizo hela ananywea pombe na bado huyo mwanamke amekaa kwenye ndoa hadi watoto wanamaliza chuo.... nyaambaaffff Hapa kataa ndoa nawaunga mkono.
Hii ni pande zote, kuna wanawake ni pasua kichwa, akipewa hela ya matumizi anaenda kwa waganga bora hata huyo anayecheza mchezo, baba ndo anahangaika watoto waende shule gani ndo afanye manunuzi ya chakula nyumbani, mama hana habari na hawa tumeona kwenye jamii yetu.
Hakunaga formula kwenye kuishi na mwenza, mchukulie namna alivyo ukiona umeshindwa lea watoto wakikua jikate endelea na maisha yako.
Ni wanadamu wachache sana wanawajibika vile wanapaswa kuwajibika, na ndio maana unaona lawama haziishi na ugomvi, hisda, chuki....
Heri nowe pekeyanguuu, heri niwe pekeyanguu, heri niwe pekeyangu mamaa...🎵🎵🎼.