Wanawake muelewe; kwa Sisi Wanaume watoto wote sio Sawa. Tunawapenda na kubariki wale wanaotusikiliza

Wanawake muelewe; kwa Sisi Wanaume watoto wote sio Sawa. Tunawapenda na kubariki wale wanaotusikiliza

Umeamua Tu kukaza fuvu lakini ukweli uko wazi!

Sizungumzii nadharia.
Tunazungumzia uhalisia

Mtoto kama angekuwa connected na mama yake au Baba yake. Hii inamaanisha pasingekuwepo na watoto wasiowapenda Mama zao au wasio na ukaribu na Mama zao.
Wewe ndio unakaza Fuvu
 
Huo ndio uhalisia wenyewe,lakini huwa inatokea mama anaamua kuharibu kwa nguvu huo muunganiko ndo inatokea Ile ya mtoto kutompenda *****!
 
Mwanaume anazalisha Mwanamke anazaa.

Hakuna Mwanamke mwenye uchungu wala mwanaume mwenye uchungu zote hizi ni nadharia za mtu mweusi ambazo zinatokana na uhaba wa maarifa na akili
Anayezalisha ni mkunga, mama anajigungua baba na mama wanazaa ila mtoto ni wa baba.

Kinachochanganya watu ni ukaribu wa mtoto na mama, ambao pia saiv hiyo nafasi mahousegirl wameiteka.
 
Anayezalisha ni mkunga, mama anajigungua baba na mama wanazaa ila mtoto ni wa baba.

Kinachochanganya watu ni ukaribu wa mtoto na mama, ambao pia saiv hiyo nafasi mahousegirl wameiteka.
Binadamu pia ni mnyama wa kawaida japo hii concepts watu wanikataa Ila tabia za kujimilikisha mtoto hazina maana na hazifai na zinasababisha Phobia ukubwani ya mtu kushindwa kujitegemea.
 
Mwanaume anazalisha Mwanamke anazaa.

Hakuna Mwanamke mwenye uchungu wala mwanaume mwenye uchungu zote hizi ni nadharia za mtu mweusi ambazo zinatokana na uhaba wa maarifa na akili
Au siyo.

Narudia tena.

Mwanamme ndiye anayezaa mtoto. Ukija bila kujitia ujuaji, nitakufafanulia kwa nini nasema mwanamme ndiye anayezaa.
 
Mimi niliowazaa ndo najua uchungu wa kila mmoja wao. Hata kama hawakusikilizi wewe
Huo uchungu mnaona kama adhabu sio, hiv wew na mmeo mkichukua mbegu zenu zikarutubishwa na kutungishwa kwrnye tumbo la Amina hivi huyo mtoto atakuwa kazaliwa ns nani?. Na mbali na uchungu unaousema hivi wew kama mama utakuwa na swaga zipi tena za kumpenda huyo mtoto?
 
Anatoa hoja za kisiasa .

Je uchungu wa kuzaa ni sawa na ule wa Baba kuipambania familia yake ili ipate mkate?
 
Binadamu pia ni mnyama wa kawaida japo hii concepts watu wanikataa Ila tabia za kujimilikisha mtoto hazina maana na hazifai na zinasababisha Phobia ukubwani ya mtu kushindwa kujitegemea.
Mkuu sio kujimilikisha inategemeana misingi ya familia imdjengwa kwenye falsafa ya iman ipi.
Kama wazaz wanaamin ktk Mungu suala la mtoto kuwa wa baba sio mjadala hata kidogo.
 
Mkuu sio kujimilikisha inategemeana misingi ya familia imdjengwa kwenye falsafa ya iman ipi.
Kama wazaz wanaamin ktk Mungu suala la mtoto kuwa wa baba sio mjadala hata kidogo.
Mtoto anabidi kuandaliwa kwa ajili ya jamii nzima na sio hizi mambo za kugombania mtoto hii inazalisha ubinafsi na kuleta phobia
 
Anatoa hoja za kisiasa .

Je uchungu wa kuzaa ni sawa na ule wa Baba kuipambania familia yake ili ipate mkate?
Wenyew wanaujua ukweli kwamba hawana huo uchungu wanaousema.
Mbona kutwa kucha kuwalaum wanaume kwamba wamewaachia mzigo wa malezi?.

Wengi wanaozaa na mastaa huwa hawawazi kuhusu watoto bali kujinufaisha wao wenyew.

Wengind wanazaa ilimradi waonekane wana mtoto hata kama hawajui watamlea vip mtoto.
Yote tisa hao ndo vinara wa kuwaangamiza baba za watoto wao ilihali wao wanawaombea baba zao waendelee kuwa hai. Inshot kuna namna wanawake wako roho ya nyoka yaan wanakaroho flan kabaya kwa watoto ila wanajivisha vazi la uchungu na blaa blaa kibao.
 
100%
 
Duh mwanamke akianza kusema kama wewe ni hatari mno , yani unamwacha haraka sana tena kwa siri.
kenge kama hiyo, ilopoke huko huko, kwangu mimi muuza mapanga yaliyoNOLEWA kabisa kwa bei cheeee, nitayajaribu kwenye shingo yake,..
 
WANAWAKE MUELEWE; KWA SISI WANAUME WATOTO WOTE SIO SAWA. TUNAWAPENDA NA KUBARIKI WALE WANAOTUSIKILIZA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Kutuzalia Sisi tunaweza kukushukuru Sana lakini linapokuja suala la Upendo wa Baba kwa Mtoto ni kipengele kingine.
Yaani Baba kusema sasa huyu ndiye mtoto wangu hiyo ni Hatua ya juu kabisa ya thamani ya Baba na mwanaume kwenye maisha yake.

Mwanaume anaweza akapata watoto hata kumi lakini asiwe na mtoto hata Mmoja. Sio kwamba kabambikiwa nope! Alipata watoto kweli kibaolojia lakini asiwe na mtoto hata Mmoja ambaye anasema huyo ni Mtoto wangu.

Wanawake hutuona wakatili Sana. Wakati mwingine hushangaa kwa nini wanaume hukataaga mtoto tangu akiwa tumbonk yaani hukataa Mimba badala ya kufurahia. Zipo sababu nyingi Sana lakini kubwa kuliko ni Ile Sababu ya ndani ya Mwanaume kusema sasa huyu ni mtoto wangu.

Mwanaume ili ampende Mtoto yaani aseme sasa huyu ni mtoto wangu au hawa ni watoto wangu kuna Sababu kuu mbili ambazo ni;

1. Kuzaa na Mwanamke wanaopendana Sana(wote Mwanaume na mwanamke wanapendana)
Mwanaume ikitokea akaoa au kuzaa na Mwanamke anayempenda Sana ni hakika mtoto anayezaliwa atampenda automatically.
Mwanaume anapopenda mwanamke Akili yake na Mawazo yake hufikiria Mpaka watoto wataozaliwa hata kabla hajalala na huyo mwanamke
Ni mwanamke wa ndoto zake.
Kama mwanamke alikupenda na wewe ulimpenda kikamilifu hapana Shaka yoyote hata watoto wenu watapendwa na Baba na kumpenda Baba Yao. Hata yatokee mazingira gani.

2. Mwanamke Kumtii na Kumsikiliza MWANAUME.
Ni wazi kuwa mwanamke kama anakusikiliza hata watoto utakaozaa naye watakusikiliza.
Na mtoto Kumtii na kumheshimu Babaake NI kuuteka Moyo wa Baba.

Mwanamke anaathari kubwa katika malezi na makuzi ya mtoto
Mwanamke asipokuwa msikivu na Akawa jeuri huathiri upendo wa Baba kwa Mtoto wake.

Kuna wakati mwanaume hujuta kuwa na watoto. Na wababa wasioeavumilivu husema Kabisa kuwa wao hawana watoto licha ya kuwa wanawatoto
Wanaume wengine huchukua maamuzi magumu Kutafuta watoto kwa Wanawake wengine kujaribu bahati yao kuona kama watapata angalau mtu wa kumuita Mtoto.

Moja ya mambo yanayowaumiza wanaume watu wazima ni suala la kukosa watoto wanaowasikiliza hata Mmoja.

WATOTO WA BABA WANASIFA ZIFUATAZO;

1. Ni Alpha Male.
2. Wanaheshimu Baba Zao katika mazingira magumu.
3. Ni marafiki wa Baba Zao. Huwaambii kitu kuhusu Baba Zao.
4. Hawanaga Kisasi na vita na Baba zao.
5. Ni walinzi wa Baba Yao.
6. Hawakubali kuingilia ugomvi wa Baba na Mama isipokuwa wao huwa wapatanishi.
7. Wanajua kuwa Ili wawe Baba na Mume Bora lazima wawaheshimu Baba waliowazaa.
Na ili wawe Mama na Wake Bora lazima wamheshimu Baba.

Kwa Sisi Watibeli kabla hatujaoa Mke lazima tujue huyo mwanamke tunayeenda kumuoa humchukulia vipi Babaake Mzazi.
Kwa sababu ni hakika vile anavyomchukulia Babaake ndivyo atakavyokuchukulia wewe.

8. Huunganisha familia na ndugu kuliko kuwatenganisha.
Watoto wa Baba ni wale wanaounganisha ndugu, jamaa na rafiki bila kujali kulikuwa na vita na migogoro. Hutafuta Nafasi ya kupatanisha wazazi na ndugu ili watu waishi pamoja.
Watoto wa hivi huitwaga watoto wa BABA

Na wengi ndio huachiwa familia na Baba zao bila kujali mtoto huyo ni wakike au wakiume ila Akiwa wakiume itapendeza zaidi. Ila kwa familia isiyo na kijana Basi wakike mwenye sifa hizo hupewa Mkoba na KUBEBA hiyo Familia.
Bila kujali ni Mtoto WA ndani au wa nje. Mtoto WA Mke Mkubwa au Mke mdogo.

Moja ya Hasara atakayopata mwanaume na Kufa mapema Kabisa au kuwa na uzee mbaya ni kukosa mtoto hata Mmoja.

Moja ya dalili kuwa familia Fulani Mzee Fulani Hana mtoto hata Mmoja ni kuangalia maisha ya Mzee MWENYEWE. Picha linaanza ametelekezwa, mwingine anatengwa na watoto wake.

Mtoto mwenye akili zilizotimia kamwe hatoweza kukubali Baba yake aishi maisha ya ajabu ilihali yeye anaishi maisha mazuri.
Watoto wa Baba hawapo hivyo. Nazungumzia Alpha Male.

Kizazi kisicho na Baba ni kizazi ambacho hakidumu. Hakiwezi Kupata mafanikio ya Muda mrefu.
Ni kizazi kitakachokuwa kinatumikishwa na familia au koo zingine zenye Baba.
Wapo baadhi ya watoto Wachache watakuwa wanaoteaotea mafanikio lakini wakiondoka ule ukoo unarudi kwenye umaskini Mkubwa tena.

Familia nyingi kubwa, zina Wababa.
Kwenye jamii au nchi yoyote Ile. Ili familia idumu walau kwa Karne kadhaa lazima watoto wawe watoto wa Baba.

Watoto wafundishwe kumheshimu Baba hata kwa namna yoyote Ile.

Tofauti na hapo, kizazi hiko kitaishia kuwa Watumwa wa familia na koo zingine zenye Wababa yaani wenye kumheshimu Baba.

Kitendo cha mwanamke kutaka kupewa sifa zaidi kuliko Baba mbele za watu ni dalili za Hatari Kabisa kuwa familia hiyo iko hatarini.

Mtoto mwenye AKILI na mwenye kuona Mbali, utukufu wake wa Kwanza lazima uanzie kwa Baba yake. Kisha mengine ndiyo yafuate.

Wanawake wenye Akili na wenye Maono.
Hata awe na uwezo Mkubwa Kiasi gani kumzidi Mumewe. Akisimama mbele za watu kuhusu mambo ya kifamilia lazima ampe utukufu Mumewe. Hata kama Mume ni goigoi.

Kuna watu hawawezi kunielewa hasahasa wale ambao wametoka kwenye familia za chini na wao ndio pengine wameotea mafanikio tena ya kutumikishwa na watu waliotokea kwenye familia zenye Baba(kumheshimu Baba).

Kuna wakati niliwahi kuandika, Mkeo asikuzidi umaarufu na nguvu. Andiko lile
Linaenda sambamba na hili. Ingawaje sio kila mtu anaweza kunielewa.
Mwanamke mwenye akili yeyote apitapo mbele za watu lazima ajitambulishe kwa jina la mumewe ili kukuza jina na heshima ya familia yake aliyoanzisha.

Swalk Linakuja, je wewe Baba yako anakutambua kama mtoto wake?
Je anajivunia?
Hapo ndipo ilipo Siri ya Mafanikio ya Muda mrefu na sio Yale ya mpito.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Mtibeli kunywa soda Kwa Mangi. Ila iwe jioni baada ya futuru. Something people don't understand Kwa nini mtoto wa nne au wa SITA anakuwa anabeba familia licha ya kuwa kuna wakubwa zake ni hili.

Kati ya watu nisioacha kusoma andiko lake wewe ni mmojawapo.
 
Back
Top Bottom