Wanawake ni viumbe hatari sana, nimemuona brother Mabeste chozi limetaka kunitoka

Wanawake ni viumbe hatari sana, nimemuona brother Mabeste chozi limetaka kunitoka

Kuna watu humu wanasema jamaa alikua parasite, yani kutegemea mkewe, wanachekesha sana, mtu ni mgonjwa hizo kazi alikua anafanyaje? Na kipindi hicho nani alikua anamlisha
Ingekuwa hivyo ni angemkimbia pale alipoanza kuumwa. Lakini jamaa alistick na mwanamke kimya kimya alipoisha kabisa ndio akaanza kuomba michango mpaka mwanamke anakaa sawa jamaa bado yupo nae tuu. Hivi parasite anakaa kwa unfavorable conditions?
 
Wanaume wanaongoza kuumiza wanawake kutelekeza famlia kuwapiga wenza wao matukio usaliti,vipigo kutembea na ndugu had wasichana wa kazi na mengine mengi mbona km yenu mnayaonaga madogo sana kuliko ya wanawake wakt nyie ndo vinara wa kuumiza mioyo ya watu,hii inanifikirishaga sana
Naona machungu wake zetu wanayopitia! Kweli si sahihi ila mnapolikoroga ni kulipiza kisasi!
 
1. Kwa wasio mjua MABESTE, alikua msanii wa MZIKI bongo fleva miaka hiyo. Moja ya hit song yake kubwa Kwa wakati huo ni, sirudi TENA. Anaimba, nakimbiza chapa, ZANGU kila saa, kwenye dhiki, sirudi te, TENA na TENA na TENA na tena na.

2. PICHA linaanza baada ya kumuoa dada Mmoja aitwae lisa, inasemekana alikua video queen, walijaaliwa kupata mtoto wa kiume.

3. Ghafla lisa akapata matatatizo ya kiafya, alikutwa na saratani, hivyo ikahitajika gharama kumtibu.

4. Hicho ni kipindi ambacho mabeste alitaka kuchanganyikiwa hususani Kwa miaka hiyo, gharama zilikua juu ye mwenyewe hakua amejipata kivile.

5. Jamaa hakumtupa demu, wakaanza kuhangaika, huku mara kule, pesa ikakata.

6. Kwa sababu mabeste alikua msanii, akawapanga wana, kama vipi waandae show alafu mauzo yote apewe mwana ili yamsaidie kumtibu mkewe wa ndoa, MANA lisa alikua mke halali na walifunga ndoa tena kipindi mabeste akiwa hot, ni jinsi GANI bro alikua na future kaacha ukapela tena enzi hizo kajala, wema, aunt, uwoya wako form, mshikaji kawategea kisogo akaoa zake.

View attachment 3641088View attachment 3641089

7. MUNGU si athumani lisa akapona kansa, shukran Kwa wana kumshikia mkono mwana na familia yake kama mnavo jua ugumu wa kuuguza una chacha fasta usishangae wakina marehemu ruge kuomba mchango wakina mkubwa fela bro kuuguza ni noma.

8. Mabeste alikua na rafiki yake wa damu ye alimtambulisha kama mdogo wake, asee kumbe dogo akaanza kumgonga mkewe, mabeste hajui ye anachukulia ni mtu na shemeji yake kumbe mwana ana mzunguka.

9.demu akaona ili awe huru akatangaza rasmi kuachana na mabeste na kumtambulisha huyo dogo wa pembeni, ambae alikua rafiki yake na mumewe,

10. Mabeste aka loose mpaka hapo jamaa akawa cha pombe, uchungu sana kila akifikiria mtu alie MUONA kama mdogo wake kamvunjia familia, kamgongea mkewe, inauma sana mnajua, yani mke kabisa tena kavunja na ndoa na kampeleka kwenye vyombo vya Sheria juu weee.


11. Wana wanafiki wakawa wanachekea chini, wanamcheka mabeste huyooooooo aliwahi kuoaa tulimkanya haaaaaaaaa, mara ghafla wana wakashtuka mchizi anapotea.

12. Mapaparazi na wasanii ikavuja video ikimuonesha mabeste kalewa chakali, Yuko kwenye boxer tu, kakonda ka muathirika wa ukimwi ikasemekena super star hana makazi ana lala nje daaaah. NADHANI maumivu baada ya kusikia dogo kamuoa kabisa mkewe na ujauzito juu.

13. Wana wakajiitisha kuokoa jahazi, simu zika pigwa kila Kona huyu aje na huyu aje oyaaa hii inshu serious mjue, mambo si mambo.

14. Harakati za kumsevu mwamba zikaanza, watu walitoboka hasa sijui ni wakina nani, mwisho ukaishia hapo.

15. Leo ndo naona jamaa anajipost huko mwili umerudi Yuko ulaya siku hizi na Alisha oa nadhani jamaa atakumbuka hili tukio mpaka anazikwa.
Kosa limeanzia kwenye no 2,yaani video model unamfanya kuwa mke,jamaa alijilipua na akalipuka kweli sema Mungu kampenda na kampigania, ashukuru ana wana wakumpigania.
 
Hii story utakua umeiskia juu juu, hata jina la huyo dada sio lita ni Lisa fickenscher,
Ukweli ulioko nyuma ya pazia huyu dada ndo aliyetoa hela ya mahari kwa niaba ya mabeste ili tuu aolewe, tangu mwanzo mama ake hakua anataka aolewe na mabeste

Licha ya lisa kuumwa, lakini sababu kubwa iliyopelekea huyu dada akafanya maamuzi ya kutoka na rafiki wa mabeste ni sababu ya mabeste kusahau nafasi yake kama mwanaume, Huyu dada kama humjui unaweza ukamlaumu lakini ni mpambanaji sana, na inaonekana alimpenda mabeste kwa moyo wote ila baada ya kukaa naye akagundua mabeste ni aina ya wanaume wasiopenda kujishughulisha

Story ya mabeste kukutana na lisa ilianzia kwenye kazi zake huyu dada kama video vixen,

Hawa watu kiasi flani nawajua, tukisimama kwenye ukweli Mabeste ndo alizingua
Haijalishi kama demu alijilipa mahali au laah,anahela au laah ila kwenye dunia hii kumpata partner ambaye yupo Bega kwa Bega na wewe kwenye matatizo wapo wachache mno.Huoni Mabeste alionyesha upendo mkubwa sana kwa mkewe mpaka kufikia hatua ya kutoa kidogo alicho nacho Najua utamuona Mabeste anazingua na si shangai mara nyingi mwanaume akiwa anauchumi mdogo akidate na mwanamke mwenye uchumi mkubwa,kile kidogo anacho toa kinaonekana hakina maana ndio maana hata wewe unasema anazingua/alishindwa kusimama kama mwanaume. Ila ukiangalie jamaa alijitahidi kwa uwezo wake na kweli kipindi akifanya hizi movement za kumsaidia mkewe ,ili apate hicho kidogo tulimuona akihangaika kwenye maredio huku.

Real love unaijua unapopitia misukosuko, Mabeste kweli sio msanii mkubwa kivile ila alikuwa na access ya kuwapata mabinti wengi wazuri na wakali kuliko mke wake,ila still bado akachagua kukaa na kupambana na mke wake wakati wa nyakati ngumu. Kuna ndoa kibao tunaziona na wenza wote wapo vizuri kiuchumi,ila msukosuko kidogo washaachana. Tena yote kwa yote unatembea na mtu wa karibu wa rafiki wa mme wako, kweliiiiiii.............wewe unaona sawa,eti hajasimama kwenye nafasi yake. Halafu hivi unajua maana ya neno Parasite? Yaani parasite akae na wewe kipindi unapitia nyakati ngumu, kweliiii......?

Ila si shangai ndio maana wanaume wengi, hawapendi wanawake waliokuwa vizuri kiuchumi sababu ya mtizamo kama wako wa kuonekana "wanazingua ........ hawasimami kwenye nafasi zao........",ila Mabeste alipambana kama mwanaume anaye mpenda mkewe,kwa nguvu zake zote, kwa akili zake zote na kwa kidogo alicho jaaliwa.

Ktk dunia ya sasa haijalishi kama ni mwanaume au mwanamke ila ni ngumu kupata mtu aina Mabeste ,wapo wachache mnoo, alicho kifanya Mabeste ni upendo wa kweli kwa kile alicho jaaliwa.
 
Hii story utakua umeiskia juu juu, hata jina la huyo dada sio lita ni Lisa fickenscher,
Ukweli ulioko nyuma ya pazia huyu dada ndo aliyetoa hela ya mahari kwa niaba ya mabeste ili tuu aolewe, tangu mwanzo mama ake hakua anataka aolewe na mabeste

Licha ya lisa kuumwa, lakini sababu kubwa iliyopelekea huyu dada akafanya maamuzi ya kutoka na rafiki wa mabeste ni sababu ya mabeste kusahau nafasi yake kama mwanaume, Huyu dada kama humjui unaweza ukamlaumu lakini ni mpambanaji sana, na inaonekana alimpenda mabeste kwa moyo wote ila baada ya kukaa naye akagundua mabeste ni aina ya wanaume wasiopenda kujishughulisha

Story ya mabeste kukutana na lisa ilianzia kwenye kazi zake huyu dada kama video vixen,

Hawa watu kiasi flani nawajua, tukisimama kwenye ukweli Mabeste ndo alizingua
Dunia ukiutafsiri upendo kwenye vitu/fedha utapotea, ila ukiwa na mwenzi yupo nawe bega kwa bega kwenye nyakati ngumu za kiafya au kiuchumi basi hiyo ni ishara ya upendo. Nasikia kaachwa na huyo jamaa kaenda kumuoa mwanamke mwengine.
 
Back
Top Bottom