Wanawake ni viumbe hatari sana, nimemuona brother Mabeste chozi limetaka kunitoka

Kuna watu humu wanasema jamaa alikua parasite, yani kutegemea mkewe, wanachekesha sana, mtu ni mgonjwa hizo kazi alikua anafanyaje? Na kipindi hicho nani alikua anamlisha
Ingekuwa hivyo ni angemkimbia pale alipoanza kuumwa. Lakini jamaa alistick na mwanamke kimya kimya alipoisha kabisa ndio akaanza kuomba michango mpaka mwanamke anakaa sawa jamaa bado yupo nae tuu. Hivi parasite anakaa kwa unfavorable conditions?
 
Naona machungu wake zetu wanayopitia! Kweli si sahihi ila mnapolikoroga ni kulipiza kisasi!
 
Kosa limeanzia kwenye no 2,yaani video model unamfanya kuwa mke,jamaa alijilipua na akalipuka kweli sema Mungu kampenda na kampigania, ashukuru ana wana wakumpigania.
 
Haijalishi kama demu alijilipa mahali au laah,anahela au laah ila kwenye dunia hii kumpata partner ambaye yupo Bega kwa Bega na wewe kwenye matatizo wapo wachache mno.Huoni Mabeste alionyesha upendo mkubwa sana kwa mkewe mpaka kufikia hatua ya kutoa kidogo alicho nacho Najua utamuona Mabeste anazingua na si shangai mara nyingi mwanaume akiwa anauchumi mdogo akidate na mwanamke mwenye uchumi mkubwa,kile kidogo anacho toa kinaonekana hakina maana ndio maana hata wewe unasema anazingua/alishindwa kusimama kama mwanaume. Ila ukiangalie jamaa alijitahidi kwa uwezo wake na kweli kipindi akifanya hizi movement za kumsaidia mkewe ,ili apate hicho kidogo tulimuona akihangaika kwenye maredio huku.

Real love unaijua unapopitia misukosuko, Mabeste kweli sio msanii mkubwa kivile ila alikuwa na access ya kuwapata mabinti wengi wazuri na wakali kuliko mke wake,ila still bado akachagua kukaa na kupambana na mke wake wakati wa nyakati ngumu. Kuna ndoa kibao tunaziona na wenza wote wapo vizuri kiuchumi,ila msukosuko kidogo washaachana. Tena yote kwa yote unatembea na mtu wa karibu wa rafiki wa mme wako, kweliiiiiii.............wewe unaona sawa,eti hajasimama kwenye nafasi yake. Halafu hivi unajua maana ya neno Parasite? Yaani parasite akae na wewe kipindi unapitia nyakati ngumu, kweliiii......?

Ila si shangai ndio maana wanaume wengi, hawapendi wanawake waliokuwa vizuri kiuchumi sababu ya mtizamo kama wako wa kuonekana "wanazingua ........ hawasimami kwenye nafasi zao........",ila Mabeste alipambana kama mwanaume anaye mpenda mkewe,kwa nguvu zake zote, kwa akili zake zote na kwa kidogo alicho jaaliwa.

Ktk dunia ya sasa haijalishi kama ni mwanaume au mwanamke ila ni ngumu kupata mtu aina Mabeste ,wapo wachache mnoo, alicho kifanya Mabeste ni upendo wa kweli kwa kile alicho jaaliwa.
 
Mimi ningetumia uchawi kwakweli,roho ya uvumilivu ninapofanyiwa usaliti na kuumizwa huwa sina kabisa..Mimi ukiniacha kwa kuniumiza jua umetangaza vita huko unapoenda hutadumu ukiforce hata 100 utakuwa hupati katika maisha yako sometimes sijipend kwa roho yangu hii ya kizigua
 
Dunia ukiutafsiri upendo kwenye vitu/fedha utapotea, ila ukiwa na mwenzi yupo nawe bega kwa bega kwenye nyakati ngumu za kiafya au kiuchumi basi hiyo ni ishara ya upendo. Nasikia kaachwa na huyo jamaa kaenda kumuoa mwanamke mwengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…