Wanawake pindi mnapokuwa na miaka 17-25 kwanini huwa hamshauriki mkasikia?

Binti akishakuwa mrembo na akishaanza kurembua macho ukimdhauri anakuangalia juu hadi chini kisha anakusonya live ama kimoyomoyo kulingana na namna mnavyohusiana.

Ila tukiwa kama wazazi, walezi, kaka na dada tusichoke tuendelee kuongea nao kwa mifano halisi. Pia mtoto wa kike anahitaji kuwa controlled kwa kiasi huwa inasaidia.
 
Aisee alikuwa vizuri nanyi mlikuwa mnaisikia ya mzee wengine hata ufanyaje pia kipindi hicho maadili yalikuwepo bado
 
Amina
 
Sawa mkuu
 
Aisee alikuwa vizuri nanyi mlikuwa mnaisikia ya mzee wengine hata ufanyaje pia kipindi hicho maadili yalikuwepo bado
Namshukuru sana mzee wetu na ujue hapo alikuwa mkali balaa nyumbani kwa mambo mengine yaan hata akiwa likizo raha hakuna kila siku tunamuuliza mama hivi baba ataanza lini kuingia kazini๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ ila suala la malezi ya makuzi alikuwa mtaratibu sana, siku moja jirani yetu alimpiga binti yake amekutwa na mimba mzee ndo akaenda kuamlia kuuliza shida nini yule mzee akamwambia eti nimempima nimekuta ana mimba. Mzee akamwambia unavompiga utabadili kile kilichotokea? Akamwambia utamuua mtoto muache awe akishazaa atajifunza....alafu ndo tumemaliza la 7 nikajiuliza huyu yeye amewezaje kufanya mapenzi mapema hivi? Bahati mbaya Bertha hakujifunza akawahi kuolewa nasikia alikuja kupigwa na mumewe hadi kufariki wakati huko tuko o level sisi dah
 
Zaidi kipigo hakifai katika kumrekebisha kwenye makuzi yake, huyo anatakikana kila unapokaa naye case studies zinakuwa nyingi ili aelewe unamaanisha nini
 
Duh๐Ÿ‘ฟ pole sana aisee!!!
 
Daah sikio la kufa hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ