Wanawake pisi kali wana tofauti gani na hawa wengine kwenye mapenzi?

Pisi kali ni mdada wa kisasa mwenye mambo mengi. Vipuli mwili mzima, tamaa, mtu wa mutandao na mwenye kushindana na dunia yaani dunia ikisema kuvaa chupi ni ushamba yeye kesho havai... anajizingatia kuteka wanaume. Kuhusu utofauti sijui kama upo kwa sasa maana asilimia kubwa dunia ya sasa mabinti karibu wote ni pisi kali tu
 
Mkuu Mr Pixel3a Pisi kali nyingi Zina sifa kama kupostika, presentable, unapata sifa kwa washkaji, etc ila hasara kubwa ni gharama, amani ya moyo, kugongewa, maana ulichoona ww kizuri kila mtu anakiona, na mara nyingi pisi kali hazina maoenzi ya kweli zinakupendea kitu flani (gari au bata) na hawana focus ya maisha.
 
Vijana ombeni sana hekima kwa maana yote yang’aayo si dhahabu. What you see isn’t necessarily what you get. Siri ya mtungi aijuaye kata. Mara kadhaa mambo mazuri; mambo adhimu huwekwa pasipotazamiwa au kutazamika kirahisi.

Mfalme Charles wa UK alioa pisi kali sana (Diana Spencer) akaishia kuchepuka tangu asubuhi yake na kitu “tofauti” kabisa. Yote ni ubatili mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…