Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 2,406
- 8,039
Habarini,
Juzi kati tulitembelewa na mdada mgeni toka taasisi ingine, alikuwa amekuja hapo kuchukua taarifa za mambo ya kikazi, sasa mkuu wangu wa kitengo aka-suggest tuliopo hapo tu-exchange namba na huyo mdada, nikampa huyo mdada namba yangu.
Baada ya dk 5 mdada akani-text kujitambulisha, akaniuliza mambo ya kiofisi, nikamjibu siku ikaisha.
Imepita zaidi ya wiki 2, nikaona namba ngeni inani-text, kuuliza nani akajitambulisha, akani-text nimpigie hana dakika, sikumpigia na sikumtilia maanani, nikaendelea na mishe zangu, baada ya hapo siku tatu mfululizo mtu anapiga simu kila mara (nlikuwa sizipokei) na text lukuki za salamu k.v mambo, vip, etc (nlikuwa sizijibu)
Siku ya nne anani-text vip, nkamwambia sina cha ziada cha kikazi nachoweza kumsaidia, hee akaniambia ana mambo binafsi tu anataka aniambie, akaomba nimuazime laki 1, yuko dar ana mgonjwa, nikamwambia hapana, kumjibu ivo, cha ajabu ananiuliza nitaweza kumpa sh ngapi nikamwambia live, sitaki na siwezi kumpa hela.
Embu nisaidieni jamani, kila mtu hua anapatwa na shida ya hela, ila kumuomba hela a total stranger mbona haiingii akilini, ni sawa wewe utoke hapa uende mahali uchukue namba ya mtu stranger humjui hakujui, halafu ndani ya wiki utegemee akupe laki 1, hio ni akili ya namna gani?? 😲😯
Heri hata ingekuwa nimeonesha dalili za kumshobokea na kutaka kumtongoza, wala hata sikuwa na wazo hilo. Mimi kwa uzoefu wangu nkipatwa na shida ya hela, nitaomba toka kwa ndugu, marafiki, co-workers, previous classmates, jirani, kote kukishindikana, naenda kupiga goti kwa Mungu. Huyo anaeomba laki 1 toka kwa a total stranger, na kutegemea kuwa atapewa, reasoning yake iko vipi? 😯😯
Bado naendelea kujifunza aisee, kuna mambo mengi bado siyajui.