Wanawake punguzeni kuomba sana hela, imekuwa kero
Nimekutana na kikundi cha wanawake saluni ya kike, mmoja akaniita akaniomba hela akale mgahawani, nikampa, ishu ikawa sina hela ndogo ndogo nina elfu kumi kumi tu. Mmoja kuona ile noti akataka na yeye apate. Nikaona isiwe nongwa nikaacha hiyo noti wagawane wote watano iwe furaha yao na mimi nikaondoka hapo sina raha kwa kutoa zaidi bila kupanga
 
Kuna mmoja aliomba nimnunulie soda, akanipeleka sehemu tulivu kunako vinywaji. Kujipindua kidogo tu akanijazia wenzake wawili wakawa watatu. Cha ajabu waliagiza bia za machupa ya shingo ndefu na nyama nusu kilo kitimoto. Mmoja akasema hali kitimoto anataka mbuzi choma. Palepale elfu sabini ikateketea kizembe kisa mwanamke aliniomba hela ya soda. Nazidi kuwa mgumu kutoa hela kwa mwanamke bila win to win situation
 
Wakuu bola uishi na panya ana kung'ata uku ana kupuliza, ila sio huyu mwanamke wangu anaomba kuzidi omba omba, hataki nitimize malengo yangu.

Juzi kaniomba kitita cha elfu tano nikampa, leo ananiomba kitita cha elfu tatu, elfu moja 3, miatano 6, miambili 15, mia 30, hamsini 60.

Hapana inatosha.
 

Attachments

  • Screenshot_20241113-211518.png
    Screenshot_20241113-211518.png
    259.9 KB · Views: 6
Wakuu bola uishi na panya ana kung'ata uku ana kupuliza, ila sio huyu mwanamke wangu anaomba kuzidi omba omba, hataki nitimize malengo yangu.

Juzi kaniomba kitita cha elfu tano nikampa, leo ananiomba kitita cha elfu tatu, elfu moja tano, miatano 10, miambili 25, mia 50, hamsini 100.

Hapana inatosha.
Madhara ya kumjibu mpenz wako ukiwa juani😂😂
 
Kitita cha "Afu tatu" ndugu mjumbe ungetoa tungekuchukulia hatua kinidhamu kumbuka tulisema anatakiwa kupewa 2% kama Mwenyekiti mstaafu AKON alivyotoa nasaha, hata hivyo itabidi iundwe kamati kuchunguza hicho kitika cha Afu tano kilitokaje
 
Back
Top Bottom