Wanawake si wabinafsi kama wanaume mnavyotuchukulia, huwa tunawaza msiyo ya waza

Mara ngapi mnatuacha nyumbani tunakula ugali na kachumbari sisi na watoto nyiinyi mkila nyama choma?
Hilo ni chaguo lenu... Kwani wee huwezi toka na watoto ukale nyamachoma tena eapecially mwanamke ambae unakipato chako.
 
Ni kweli kabisa!
Wanaume wanashindwa kusoma akili ya mwanamke
Mwanamke anawaza kutekeleza matatu kwa wakati mmoja

Wanawake wanahitaji attention kuliko shilingi kumi yako unayoikimbiza siku na mchana na haionekani.. MNAKERA SANA

Sio wote wanavutiwa na pesa zenu bana
Mwanamke ni pambo la nyumba
** Mnatuvuruga tu
 
wanawake wanaweza kuisoma akili ya mwanaume?upewe attention wewe ni nani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weee kumtajia mwanaume GAWIO la kikoba ni kosa la jinaiii.. Mbona hutabakiwa na hata sent tano. Plans zote za pesa atapanga yeyeee hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa kapanga nyumba kwa mika kumi na familia yake bila kujua kuwa nyumba aliyopanga ni ya mke wake.[emoji41][emoji41]alafu leo unajitetea et sio mbinafsi..W.t.f

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kumbuka kuna majukumu mengine mke anayafanya ndani ya nyumba ambayo wewe hauyafanyi
 


Kumbe mbavu zetu wanaume ndiyo Venus? Nilikuwa sijajuwa hili, Ahsante dada Sky Eclat
 
Ubinafsi mnao tena mkubwa sana nitakupa mifano hai
1, kwa wale wana chuo watakuwa mashaidi ukienda kwenye hostel za Girls tumeona mengi ni vigumu wao kwa wao kuvaliana tu hata viatu au malapa labda)na wanabaguana sana(hubaguana wao kwa wao na kuwa na vijembe au kutengeneza makundi)

2,Kuna wengine hujiona wapo matawi sana kusalimia hamna,na ukimsalimia anaweza kukaa kimya akkijiona ndo top,kisa mpo class moja

3, na pale anapokuzidi kimatokeo class naweza kukuona kama huna lolote kwake,kumbe pengine uwezo wa kukalili ndo umemsaidia na sio kuelwa, na elimu yetu ya chuo kukalii ndo unatoboa.

4,Wakichukizana ni ngumu kurudiana au kusalimiana wao kwa wao wanawake au na njisia ya kiume

5,Mwingine anaweza kukujibu ovyo tu ukimuuliza swali fulani kwa nia njema kisa tu amekuchukia. Au akijisikia

Kwa kifupi nyinyi wengi wenu ni wabinfsi sana sio kidogo, ni wachace wanaojitambua hasa wale wasichana wanaopenda kukaa na wanaume sana kidogo hao hujielewa.

Nb kwa boyz au wanaume huwezi kukutana wanafanya hayo niliyotaja hapo juu na ikitokea basi ni wachache au hamna kabisa

Tumeyaona mengi
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…