Wanawake tunaolewa na walio tayari kwa ndoa

Ukweli mtupu,ninachokupendea unapoibuka unaibuka na chuma🤜sana cute
 
Shida kubwa ni kushindwa kuhimili pressure tunazokumbana nazo kwenye jamii, na kujiona umri unakimbia.
Nyumbani kila siku uulizwe unaolewa lini wenzio wanaolewa tu, utafkiri we ndo unaamua sasa naolewa.

Bado hujaja kwa marafiki (wale wenye marafiki kama utitiri na asilimia kubwa wawe wameolewa) kila leo nao wakukomalie mara olewa shosti sa sijui ukaolewe mke wa pili na mume wake 😏
sasa kama hujielewi nawewe ndo unajitumbukiza tu popote ilimradi kasema ndoa ili tu wakuone nawewe kumbe unaweza kuolewa, kumbe maskini unayeenda kuolewa naye hisia naye tu hunaaa.

Wadada tufanye mambo mengine hizo ndoa zitukutage mbeleni tusikimbilie too sad wengine mpaka tunajioa, yani ukampe mwanaume hela akulipie mahari upuuzi wa kiwango cha lami.
Mamkubwa zangu walishaniulizaga unaolewa lini nikawajibu, kama raha kuolewa waolewe mara ya pili ila tusiulizane mambo ambayo siamui mimi ebooo.
 
Yaani jamii ikikukomalia utajuta.
Hasa mashangazi wa shangazi kaja
 
Ni mtihani sana
 
Sasa kwa nini mnakubali kuolewa hamjapenda?mkipigwa risasi muanze kulia lia 😝
Kama hujapenda bora uamue mapema
 
 
Huwezi kumuheshimu mwanaume usiempenda.
Mmepata watoto sita na wote mwanamke hajachepuka! Halafu bado mnasema mwanamke hampendi mumewe! Kweli?

Wengine wana watoto 13 kabisa Lakini mume haheshimiwi analazimika kwenda kupata mwanamke mwingine!!!

Sasa ni heshima ya namna gani hiyo inayofungamana na Upendo wa mwanamke kwa mume wake?

Natanguliza Shukrani kwa majibu yenu.
 
 
Hahaha kuna mtoto wa dada aliulizwa unaolewa lini, akajibu nikiolewa kwani nyie mnafaidika nini? Mpaka leo hakuna aliyeuliza tena swali kama hilo
 
Jifunze kupenda acha ujinga!
 
Tamaa zinawaponzaga wakion wenzao wanaolewa wanahisi wanafaidi kwenye ndoa
 
Ila wanawake wengi hawajui basics needs zao, wengi wao wana fikiria luxury life. Mwisho wa Siku anaolewa na MO ,ila kamwacha Muddy ambaye anampenda na anao uwezo wa kumtimizia mahitaji yake ya msingi, ila kamchagua MO sababu tu ya luxury life. Halafu kesho anambembeleza Muddy awe kidumu chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…