Shida kubwa ni kushindwa kuhimili pressure tunazokumbana nazo kwenye jamii, na kujiona umri unakimbia.
Nyumbani kila siku uulizwe unaolewa lini wenzio wanaolewa tu, utafkiri we ndo unaamua sasa naolewa.
Bado hujaja kwa marafiki (wale wenye marafiki kama utitiri na asilimia kubwa wawe wameolewa) kila leo nao wakukomalie mara olewa shosti sa sijui ukaolewe mke wa pili na mume wake [emoji57]
sasa kama hujielewi nawewe ndo unajitumbukiza tu popote ilimradi kasema ndoa ili tu wakuone naweqe kumbe unaweza kuolewa, kumbe maskini unayeenda kuolewa naye hisia naye tu hunaaa.
Wadada tufanye mambo mengine hizo ndoa zitukutage mbeleni tusikimbilie too sad wengine mpaka tunajioa, yani ukampe mwanaume hela akulipie mahari upuuzi wa kiwango cha lami.
Mamkubwa zangu walishaniulizaga unaolewa lini nikawajibu, kama raha kuolewa waolewe mara ya pili ila tusiulizane mambo ambayo siamui mimi ebooo.