Wanawake tunaolewa na walio tayari kwa ndoa

Wanawake tunaolewa na walio tayari kwa ndoa

Sio nyodo muda mwingine shukuru kama mtu hakupendi na anakuonyesha
Atakuletea suluba kwenye ndoa buree
Mtoa mada naunga mkono hoja and vice versa ata sis wanaume unakuta unaempenda ana nyodo anaamua kuoa aliyepo kwa vigezo vya tabia maisha yaende mbele
 
Upo sahihi 100% mfano hai mimi kuna mrembo mmoja nilikua nae kwenye mahusiano na tunapendana haswaa, sasa mimi mipango yangu sio kuoa kwa sasa na mdogo wake mwaka jana aliolewa, wazazi wake na ndugu wamemforce san aolewe kila siku ananiomba ata mahari tuchangie ila ratiba zangu haziruhusu kuoa sasa kuna jamaa kaenda kutoa posa na bint kakubali kutokana na hali ya wazazi kumlazimisha ila pale kwa kweli sioni ndoa maana bint kila siku ananitafuta na anasema ata akiolewa atanizalia imebidi nimpige stop kunitafuta acocentrate na ndoa yake tarajiwa ila bado akili yake ipo kwangu mda wote.
Hizi bahati wenzetu mnazipataje?
 
Hapo kwenye pesa alafu ikwishe daah,,kumuheshimu mwanaume usompenda ni mtihani sana
 
Hahaha kuna mtoto wa dada aliulizwa unaolewa lini, akajibu nikiolewa kwani nyie mnafaidika nini? Mpaka leo hakuna aliyeuliza tena swali kama hilo
Aisee wazazi wa siku hizi wajinga sana. Ningekuwa baba yake nasikia amejibu hivyo nitamwita na kumwambia huo umalaya usilete kwangu.

Hivi kweli mzazi mtoto wako anafikisha miaka 30 hajaoa wala kuolewa unafirahi tuu...ujinga mtupu.
 
Ndoa ni jambo la kheri mkuu au hujui
Ni jambo la heri ambalo ndani yake kuna viapo ambavyo unavyotakiwa uviishi "nitakuwa naye kwa shida na raha........ uzima na ugonjwa........".

Hivyo viapo ndio ndoa yenyewe, ukikubali ndoa manake umekubali kuuishi ktk hivyo viapo.Sio leo ana hela upo naye kesho hana una mkimbia.
 
Shida kubwa ni kushindwa kuhimili pressure tunazokumbana nazo kwenye jamii, na kujiona umri unakimbia.
Nyumbani kila siku uulizwe unaolewa lini wenzio wanaolewa tu, utafkiri we ndo unaamua sasa naolewa.

Bado hujaja kwa marafiki (wale wenye marafiki kama utitiri na asilimia kubwa wawe wameolewa) kila leo nao wakukomalie mara olewa shosti sa sijui ukaolewe mke wa pili na mume wake 😏
sasa kama hujielewi nawewe ndo unajitumbukiza tu popote ilimradi kasema ndoa ili tu wakuone nawewe kumbe unaweza kuolewa, kumbe maskini unayeenda kuolewa naye hisia naye tu hunaaa.

Wadada tufanye mambo mengine hizo ndoa zitukutage mbeleni tusikimbilie too sad wengine mpaka tunajioa, yani ukampe mwanaume hela akulipie mahari upuuzi wa kiwango cha lami.
Mamkubwa zangu walishaniulizaga unaolewa lini nikawajibu, kama raha kuolewa waolewe mara ya pili ila tusiulizane mambo ambayo siamui mimi ebooo.
Nauhakika bado ni kijana uko 20's ukifika 30's alafu uendelee kuwa single internal struggle itakutesa sana kiasili mwanadamu hajaumbwa kuishi single

Unaongea kirahis rahis sababu bado ni kijana na unanguvu
 
Ni jambo la heri ambalo ndani yake kuna viapo ambavyo unavyotakiwa uviishi "nitakuwa naye kwa shida na raha........ uzima na ugonjwa........".

Hivyo viapo ndio ndoa yenyewe, ukikubali ndoa manake umekubali kuuishi ktk hivyo viapo.Sio leo ana hela upo naye kesho hana una mkimbia.
Kuishi single kunachangamoto zake na ni Bora kuoa kuliko kuishi single ukiwa bado kijana una nguvu huwez elewa hivi vitu
 
Ahahaaa hujui hata umri wangu we soma tu afu acha mambo ya umri niachie mwenyewe.
Nauhakika bado ni kijana uko 20's ukifika 30's alafu uendelee kuwa single internal struggle itakutesa sana kiasili mwanadamu hajaumbwa kuishi single

Unaongea kirahis rahis sababu bado ni kijana na unanguvu
 
Back
Top Bottom