Nimegundua ndoa nyingi hazidumu kwa sababu wanawake wengi wameingia kwenye ndoa na wanaume waliokuwa tayari kuwaoa na sio wale wenye mapenzi ya dhati kwao.
Inatokea unampenda mwanaume ila hakuoi .anatokea mwingine anatangaza ndoa inabidi ukubali .muda nao haucheleweshi matokeo
Ndoa inakuwa ndoana maana hakuna feelings wala nidhamu.
Ni ngumu mwanamke kusex na mtu asiempenda,ni ngumu kumuheshimu mwanaume usiempenda.
Mbaya zaidi itokee huyo mwanaume alipendewa fedha na fedha imeisha ,basi hyo ndoa ni inakuwa jehanum kabisa
Daaah, ulicho kiandika ni kweli, acha nikupe story mbili,
Wiki hii iliyo isha leo, kuna dogo alitoa mahari hapa jirani ndoa ikatangazwa kanisani, ikawa send off ya binti , dogo hakutokea, wamepiga simu wajuavyo dogo hapokei, ikabidi waende kuuliza kwa wazazi wazazi nao hawafahamu dogo aliko enda, Rafiki mtu kuulizwa akasema dogo yupo Dar na ameondoka jana yake kwa basi asubuhi mapema,
Basi watu waliochanga michango yao wamekwazika na ndoa haikufungwa mpaka leo, taarifa za chini chini
dogo yupo na kademu anakokapenda sana huko Dar, na amesema asitaftwe kwa maana hakuwa amemkubali huyo alotaka kumuoa ila alijilazimisha tu,
story ya pili,
Mtoto wa mchungaji alikuwa fundi nguo akapewa mimba na mvulana fundi nguo mwenzake wakati alikuwa ameshalipiwa na posa kabisa na kijana mwingine,
Ndoa imefungwa watu hawajui kama binti anamimba ya miezi 4 jamaa akakabidhiwa mke baada ya ndoa zimepita siku chache mke anaanza onyesha mabadirika maana mabinti wengine mimba zinajificha kwenye matiti, mama mkwe kumuuliza mtoto wake vip ulimpa mimba ndipo ukamuoa jamaa akasema sikuwahi kulala naye hata siku moja,
Alipo banwa binti akasema ukweli kuwa mimba ni ya fundi mwenzake, fundi kupigiwa simu na wazee akakili kuwa mimba ni yake maana binti alikuwa anampenda sana na hata alipo mkatalia kuwa ameshatolewa posa inabidi atulie yeye alizidi kumsumbua kuwa anampenda sana, akawa anamfuata Getto,
Ndoa imesha vunjwa mpaka sasa