Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Ukiingia kwenye ndoa hakuna mimi kuna SISI,Wakristo si huwa mnasema mwili mmoja?unakuwaje mwili mmoja nusu inafuraha na nusu inahuzuni?Wewe huna mume and with that attitude you wont have a husband,utazalia nyumbani!

Tumia akili kujibu hoja sio hisia mkuu nimejibu hoja ya ke wasisome sio alichojibu huyo mama kwa familia yake
 
Single BABA na single MAMA hawatoisha nasema...Mke kama huyo wanini aseeee? Akienda kwa wazazi wake akirudi atakuta nshahama na watoto npo sehemu ingine Ndo ajue mimi mwanaume au mwanamke na sitomwambia.

Akipiga simu namjibu simple and clear..Anza life kivyako Vitu vya kuanzia maisha hivyo hapo (maana sitobeba hata kijiko) Ndo atajua...wakati mwingine Upele humwota asie na kucha.
 
Mkuu nilisoma nikaelewa niliamua nikuzingue tu.

Kumsaidia mwanaume si vibaya ingawa hapa inategemea na ndoa yenu ilivyo.

Kikubwa nilichoshangaa ni kauli ya mwanaume kuwa "mbona umetuacha bila kitu ndani" ni bora angekaa kimya.

Kauli yake ni kama kakata tamaa anasubiri kulelewa, kuletewa yaani utafikiri huyo mke ni mzazi wake sio kauli ya kiume.
Hawa watu tunafahamiana tu kwa ukaribu, shida ipo kwa mwanamke,anadai wakati jamaa yupo chuo,hela yake ilitumika sana kwenye mambo ya familia na mwanaume alichangia kidogo sana,basi mwanaume ndo ana miezi 2 tangu atoke chuo,na tangu jamaa ametoka chuo,mwanamke kama ameacha ile hali ya kuisimamia familia ingawa anajua fika kuwa mumewe ana hali mbaya ya kiuchumi,yaani anaona hela yake kuendelea kutumika na mwanaume yupo
 
Single BABA na single MAMA hawatoisha nasema...Mke kama huyo wanini aseeee? Akienda kwa wazazi wake akirudi atakuta nshahama na watoto npo sehemu ingine Ndo ajue mimi mwanaume au mwanamke na sitomwambia.

Akipiga simu namjibu simple and clear..Anza life kivyako Vitu vya kuanzia maisha hivyo hapo (maana sitobeba hata kijiko) Ndo atajua...wakati mwingine Upele humwota asie na kucha.
Duh! Si kwa hasira hizo
 
Hawa watu tunafahamiana tu kwa ukaribu, shida ipo kwa mwanamke,anadai wakati jamaa yupo chuo,hela yake ilitumika sana kwenye mambo ya familia na mwanaume alichangia kidogo sana,basi mwanaume ndo ana miezi 2 tangu atoke chuo,na tangu jamaa ametoka chuo,mwanamke kama ameacha ile hali ya kuisimamia familia ingawa anajua fika kuwa mumewe ana hali mbaya ya kiuchumi,yaani anaona hela yake kuendelea kutumika na mwanaume yupo
Sasa kumbe mwanamke alichangia sana familia kuliko mke ila hapa baadhi ya wanaume washaanza kutoka mapovu.

Na ubaya wa wanaume ukiwazoesha kulea familia ndiyo inakua kimoja wanarelax.

Ni bora kila mtu akabaki na majukumu yake.
 
Hataki tusaidiane, aache kazi alee watoto. It's very simple, huwezi kuamka 0500hrs kila siku, tunakula chakula cha dada, watoto wanapelekwa na dada, wanajifunza tabia za dada, wewe unarudi 2000hrs then ulete story za kipumbavu.

Be "a stay home wife", ili ulete watoto kama " nature" inavyosema. Otherwise if you go out there, I should see the fruits of your labor.

Na ndohichi wanachotakiwa kukifanya me wote sasa kama hawawezi simamia misimamo yao wenyewe dharau ndoinayofata maana mpk mke anaondoka nyumbani bila kuaga anatoa tu taarifa inaonyesha wazi hakuna maeleeano ndani ya nyumba na me hayupo kwenye nafasi yake kama kichwa cha familia
 
Halafu tukisema humu mwanamke aliyesoma ni LIABILITY kwenye ndoa tunaonekana wapuuzi, mara ohoo.. hatujiamini..blah blah blah!

Labda tuwekane sawa kwenye kitu kimoja na wote mnaojiandaa kuoa wanawake wasomi/wenye kazi muipate hii.

-Kadri mwanamke anavyozidi kusoma umuhimu wake kwa mwanaume unapungua. Na hata akiangia kwenye ndoa ni kwa ajili ya kupandisha social status tu.

-Mwanamke aliyeelimika hasa aliyefika ngazi za juu ana ndoto binafsi nyingi sana za kutimiza na huwa hazifi hivi hivi tu. Anaweza akazitelekeza kwa muda lakini siku akipata fursa ya kuzitimiza ndoto zake lazima aitumie fursa hiyo hata kama tayari yumo ndoani na hajari kama itaathiri ndoa.

-Mwanamke hata awe na uchumi mkubwa kiasi gani lakini ile natural instinct ya utegemezi haiwezi kumtoka, sana sana akijitahidi atakupunguzia mzigo tu kama mmezaa nae yeye atajigharamia mwenyewe huku watoto akikuachia wewe.

-Kadri mwanamke anavyozidi kuishi na wewe kwenye ndoa ndivyo anavyozidi kukuchoka hasa kama anajiweza kiuchumi na haoni hatari kuvunja ndoa maana hana cha kupoteza.

Kiufupi tu ni kwamba wanawake wasomi ni watu wenye matatizo mengi sana ndoani.

To a woman more education more problems in marriage-wise.
Brother unawajua wanawake kuliko waooo...... Umewastudy sana asee
 
Kila nikiingia jamii forum ndoto zangu za kuoa mwakani lazima ziyeyuke kwa asilimia kubwa sana .. Eeeh mungu tusaidie na hawa wanawake
Siyo lazima sana kuoa mkuu. Mbona unaweza ishi peke yako na maisha yakawa murua..
 
Huyo mkaka ni Nani yako na Umejuaje kuhusu jambo la ndani ya familia yake? Tuanzie hapo kwanza.

Kama sijakosea naww Ni miongoni mwa wanaokula hela za huyo mkaka... Ndo maana mkewe hataki kufanya chochote maana Anajua kuna mtu anapewaga hela...

NB:
Ile kauli ya yule mdada ya kwamba FANYENI MPANGO NA WANAO MPATE KULA... Alimaanisha watoto na mume waje kwako.. We muulize vzur
 
Niko neutral

Sasa kama uko neutral itabidi uchague mwanamke ambaye utaweza kuishi nae kineutral neutral tu.. maana kuna muda utahitaji kumagufuli na pia kuna muda unahitaji kwenda kidiplomasia na huyo mwanandani wako!

Tena nakushauri umdake huyu dada wakujiita Ladyred mtawezana sana.
 
Jaribu kujibu Kwa mujibu wa uzi ulivyo...

Sasa mleta uzi si ndio kasema ameambiwa na jamaa haya yote? Ukitaka uweke kabisa namna unavyotaka watu wachangie uzi wako.

Uzi unasema tena kwa kunukuu, jamaa amemuuliza mkewe.."..mbona umetuacha bila kitu?.." Nakujibu kwa kadri uzi ulivyo, hiyo ni kauli dhaifu sana kutolewa na mme.
 
Back
Top Bottom