Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Ukishajiona hautoshi kwenye nafasi ya kuwa mume, nakushauri usioe tu. Ni vyema umejitambua mapema.
hahaha kuna wanawake wengine ukioa kama wewe walai vile utaishia kufungwa, so mimi ni kama wewe yaani wote "ke" hahahahah
 
Yaani.
Hili la kuto kusoma sikubaliani nalo kabisa.
Kupitia kusoma nimejifunza mengi Sana..pengine Hadi kuwa hivi nilivyo Ni kwa sababu ya shule

Naombeni mnielewe mimi simaanishi kwamba wanawake wasiende shule. Shule ni muhimu tena sana kwa dunia ya leo. Mimi mwenyewe binti yangu lazima aende shule tena ntampeleka shule zenye ubora kuliko hata zile nilizosoma mimi.

Kilichonifanya mimi kuwa na mawazo hayo ni mambo ninayoyaona yakiendelea kwenye mahusiano/ndoa ambazo ni za wasomi(hasa mwanamke) jinsi gani zilivyokuwa na misuko suko kulinganisha na zile ambazo hazijengwi na wasomi(hasa mwanamke).

Kwanini ni uongo kwamba ndoa nyingi zinazovunjika ni zile ambazo zinaundwa na wasomi(hasa mwanamke)?

Ni uongo kwamba asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na mahusiano yao ni wale walioa wanawake wasomi?

Ni uongo kwamba asilimia kubwa ya ndoa zinazoteswa na pepo la ubinafsi ni wasomi?

Sasa kama majibu ya hayo maswali hapo juu ni hapana, kwanini tusione kuna kasoro kubwa kwa mwanamke aliyesoma linapokuja suala la ndoa?

Sipingi watu wakuoa wasomi ila na tahadharisha tu kinachoweza kuwakuta hili wajiandae kwa lolote.

Wanawake waliosoma are good to be with but they have forgone their marriagibility for education/career.
 
Jamani mbona tunaelewa tu zungumzeni taatibu bwana
 
Baadhi ya wanawake ni nyoka sio tu katika masuala ya matumizi bali pia ktk masuala mazima ya ugawaji wa tendo la ndoa. Usiombe mwanake akawa na mchepuko.....atakunyima mbunye hadi nawe utaanza kuchepuka, utake usitake. Sijui wanawake huwa mnakwama wapi.
Mwanamke umebahatika kupata mwanaume wako wa ndoa,mnaishi vizuri tu,lakini kwa nini sisi wanawake tunakuwa tunawategea wanaume na huku unajua fika hali ya mmeo? Na huku tuna ingiza vipato vyetu wenyewe

Kuna mkaka nimemuonea hadi huruma

Huyu kaka ni mfanyakazi wa serikali na mke wake pia

Siku za hivi karibuni amemaliza chuo,ila gharama za chuo alikuwa anajigharamikia kwa kiasi kikubwa na kulingana na maisha ya chuo na gharama ,aliweza kukopa kwenye Benki moja hivyo kwa wastani kwa makato ya mshahara wake ,mshahara ukawa mdogo sana,na ulivyotoka wa mwezi uliopita alilipa kodi ya nyumba na nyingine kwenye shughuli za kilimo,akawa hana kitu

Na bahati nzuri mke wake anajua hali yake ya uchumi na kila kitu

Sasa leo mke wake kasafiri kwenda nyumbani kwao,na kwa vile mke wake anajua hali ya mme wake,mwanaume akafikiri mwanamke angefanya shopping ya mahitaji ya ndani kabla hajaondoka ili watoto wao watatu na mmewe wasipate shida

Lakini mwanamke hakununua mahitaji ya ndani ameondoka kwenda kwao akisema wazazi wake wamemuita kwa dharura

Mwanaume alivyojaribu kumuuliza "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Majibu ya mwanamke" Hivi wewe si ndo mwanaume, yaani unadiriki kuniambia jambo kama hilo,kwani mimi ndo mwanaume wa familia,wewe fanya mpango mle na wanao lakini sio kuniambia mambo ya ajabu"

Loh! Kaka wa watu mpaka nimemhurumia,

Jamani na sisi wanawake tuwe na utu,familia ni ya wote, na kama mwanaume hali si nzuri,ajibika asilimia 100,lakini si kwa roho mbaya hiyo
 
Yeye ni mwanaume, mwanaume anakwamaje kwamfano?!!!!![emoji1745][emoji1745][emoji1745][emoji1745][emoji1745][emoji1745]
Mwanaume ni binadamu, kukwama kupo tuu! Mbona sie tunakwama?, na kazi tunafanya?!
 
Naombeni mnielewe mimi simaanishi kwamba wanawake wasiende shule. Shule ni muhimu tena sana kwa dunia ya leo. Mimi mwenyewe binti yangu lazima aende shule tena ntampeleka shule zenye ubora kuliko hata zile nilizosoma mimi.

Kilichonifanya mimi kuwa na mawazo hayo ni mambo ninayoyaona yakiendelea kwenye mahusiano/ndoa ambazo ni za wasomi(hasa mwanamke) jinsi gani zilivyokuwa na misuko suko kulinganisha na zile ambazo hazijengwi na wasomi(hasa mwanamke).

Kwanini ni uongo kwamba ndoa nyingi zinazovunjika ni zile ambazo zinaundwa na wasomi(hasa mwanamke)?

Ni uongo kwamba asilimia kubwa ya wanaume wanaoteswa na mahusiano yao ni wale walioa wanawake wasomi?

Ni uongo kwamba asilimia kubwa ya ndoa zinazoteswa na pepo la ubinafsi ni wasomi?

Sasa kama majibu ya hayo maswali hapo juu ni hapana, kwanini tusione kuna kasoro kubwa kwa mwanamke aliyesoma linapokuja suala la ndoa?

Sipingi watu wakuoa wasomi ila na tahadharisha tu kinachoweza kuwakuta hili wajiandae kwa lolote.

Wanawake waliosoma are good to be with but they have forgone their marriagibility for education/career.

Hii umeiconclude kwa ke wote ndomana unakua attacked ila kiukweli hivi vitu vinatokea kwasababu tofautitofauti either ni kwa ke or me na sio wote walioenda shule hawana adabu kwenye ndoa zao ni wachache kwa kukosa maadili na wengine wamejitoa sana kwa me lakini wameishia kupewa maumivu ndomana wamegeuka kuwa malshababu period
 
Hataki tusaidiane, aache kazi alee watoto. It's very simple, huwezi kuamka 0500hrs kila siku, tunakula chakula cha dada, watoto wanapelekwa na dada, wanajifunza tabia za dada, wewe unarudi 2000hrs then ulete story za kipumbavu.

Be "a stay home wife", ili ulete watoto kama " nature" inavyosema. Otherwise if you go out there, I should see the fruits of your labor.

Na hapa wengi ndio wanafeli aidha kwa kutokujua au wanajua lakini wanalea tu ujinga.

Unamkuta kidume anakwambia kabisa eti mimi hela ya mke wangu siigusi hata kidogo, mahitaji yote ya nyumbani ni juu yangu, kwanzia karo za watoto mpaka mshaara wa mfanya kazi wa ndani anawajibika yeye tu. Halafu sasa wakati wote yeye na mkewe kila siku wanatoka hasubui na kurudi giza limeingia kwa ajili ya kutafuta ridhiki.

Yaani hela za mkewe zinakuwa ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi kama vile kununulia mawigi,nguo,kusaidia ndugu,kulipia michango ya harusi na kuwatoa out watoto weekends.

Cha kustahajabisha zaidi mwanaume wa hivi unakuta wakati anatafuta mwenza elimu na kazi ilikuwa ndio vipaumbele vyake vikuu kwa mwanamke.

Kimbembe kinakuja siku jamaa akiingia kwenye crisis kiasi cha kushindwa kucarry hizo responsibilities kama alivyozoea. Na huo ndio anaona ni muda mauafaka wa yeye kusaidiwa na mke wake kutekeleza majukumu ambayo kwa muda mrefu amekuwa akiyabeba yeye tu.

Hapa sasa ndio movie ya kihindi ya Amita batchan inapoanza kukolea rasmi, baada ya kuanza kukutana na kauli za “majukumu yako hayanihusu”.... hakika huo ndio utakuwa muda wa kutambua matazamio yako ambayo umekuwa nayo kwa miaka mingi ulikuwa unajidanganya, ndio muda wa kuanza kuwatamani wale rafiki zako walioa wake wasiokuwa na elimu wala kazi ukiwaona wana ahueni kubwa sana ukilinganisha na wewe.
 
Mwanamke umebahatika kupata mwanaume wako wa ndoa,mnaishi vizuri tu,lakini kwa nini sisi wanawake tunakuwa tunawategea wanaume na huku unajua fika hali ya mmeo? Na huku tuna ingiza vipato vyetu wenyewe

Kuna mkaka nimemuonea hadi huruma

Huyu kaka ni mfanyakazi wa serikali na mke wake pia

Siku za hivi karibuni amemaliza chuo,ila gharama za chuo alikuwa anajigharamikia kwa kiasi kikubwa na kulingana na maisha ya chuo na gharama ,aliweza kukopa kwenye Benki moja hivyo kwa wastani kwa makato ya mshahara wake ,mshahara ukawa mdogo sana,na ulivyotoka wa mwezi uliopita alilipa kodi ya nyumba na nyingine kwenye shughuli za kilimo,akawa hana kitu

Na bahati nzuri mke wake anajua hali yake ya uchumi na kila kitu

Sasa leo mke wake kasafiri kwenda nyumbani kwao,na kwa vile mke wake anajua hali ya mme wake,mwanaume akafikiri mwanamke angefanya shopping ya mahitaji ya ndani kabla hajaondoka ili watoto wao watatu na mmewe wasipate shida

Lakini mwanamke hakununua mahitaji ya ndani ameondoka kwenda kwao akisema wazazi wake wamemuita kwa dharura

Mwanaume alivyojaribu kumuuliza "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Majibu ya mwanamke" Hivi wewe si ndo mwanaume, yaani unadiriki kuniambia jambo kama hilo,kwani mimi ndo mwanaume wa familia,wewe fanya mpango mle na wanao lakini sio kuniambia mambo ya ajabu"

Loh! Kaka wa watu mpaka nimemhurumia,

Jamani na sisi wanawake tuwe na utu,familia ni ya wote, na kama mwanaume hali si nzuri,ajibika asilimia 100,lakini si kwa roho mbaya hiyo
Wewe mwana nke umeolewa?
 
Ila huyo kaka ana moyo nae kumuuliza mwanamke "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Kaka zangu tafuteni hela tafuteni hela mbebe majukumu yenu wenyewe
hapana Unakosea!! kuna kipindi sisi wapapambanaji tunakosa hata mia..huyo mwanamke ningemuacha huwa sitaki ujinga hata kama nina watoto nae
 
Hii umeiconclude kwa ke wote ndomana unakua attacked ila kiukweli hivi vitu vinatokea kwasababu tofautitofauti either ni kwa ke or me na sio wote walioenda shule hawana adabu kwenye ndoa zao ni wachachekwa kukosa maadili na wengine wamejitoa sana kwa me lakini wameishia kupewa maumivu ndomana wamegeuka kuwa malshababu period

Hapo una uhakika kwamba ni wachache?

uhalisia audanganyi dada/kaka.

Tusiende mbali sana tuchukulie tu hii Jf kama sample, wanaume wanaoleta threads za vilio ni wanaume ambao wako kwenye mahusiano na wanawake wa kundi gani kama sio wasomi?

Pia sijasema kwamba wanawake ambao hawajasoma hawasumbui kwenye ndoa, wanasumbu ndio. Lakini udadi yao huwezi ukailinganisha na waliosoma.
 
Back
Top Bottom