Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Katika mafundisho ya jamii, jamii za zetu zote zinamtaarisha mtoto wa kike kuwa mlezi wa familia. Kuondoka nyumbani kwa mtoto wa kike ni kukabidhiwa kwa mume. Mume huyu anakua ndiyo mtu wa kukulinda na wewe unategemewa umlee. Ujue chakula chake, usingizi wake na afya yake.
Katika familia zenye kipato cha kati ambako mama na baba wote wana majukumu mazito maofisini au hawa wenzetu walio hamia Ughaibuni taratibu hizi zinabadilika. Kukitokea kutofautiana katika ndoa mara nyingi mgogoro husuluhishwa kwa talaka na mali kugawanywa.
Kwanza binti kabla hajachumbiwa huyo mchumba anaangaliwa (1) ametoka katika familia gani. (2) ana elimu gani na ajira gani.
Nimekutana na familia nyingi za Wachina na Wahindi. Mama ndiye mwenye elimu na ajira ya kueleweka, mume ana ajira ya kusukuma siku lakini mama akirudi nyumbani ni mke wa kumuandalia mume wake na watoto chakula. Mshahara unagawanywa katika majukumu bila kujali nani ameingiza kiasi gani. Hawa watakuambia wametoka kijiji kimoja.
Familia hizi hutokaa usikie matatizo yao ya ndoa. Hata wakiwa na tofauti zinamalizwa ndani ya familia.
Tunalalamika kuwa vijana wetu wanakiuka maadili kwa kuzaa nje ya ndoa. Tumeacha kufundisha jamii umuhimu wa familia pia tuanze kulea watoto wa kike kwkuwaandaa kwa majukumu sawa na wakiume. Tuache ile dhana ya kuwa mwanaume ndiye mpambanaji katika familia.