Wanawake wa kizazi hiki mbona hawana hofu ya Mungu jamani?

Wanawake wa kizazi hiki mbona hawana hofu ya Mungu jamani?

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Nisikuchoshe ndugu yangu, ngoja nizame mazima kwenye mada kuna mwananmke nilikua nampenda sana (ndiyo kabla ya jana alikuwa kila kitu kwangu) anaitwa G, tulikuwa kwenye mahusiano mazito tangu 2019 mpaka jana tulipoweka nukta.

Kilichonichosha mpaka nikaandika uzi huu ni kuwa, jana aliniomba tutoke kwa mlo wa usiku maana amekumbuka sana kuku wa sekela wa wapemba. Basi nikamwambia poa akitoka kazini atulie skan kwake ntampitia saa mbili, maana mimi ni mzee wa mitikasi 'born town' ile misheni Town, halafu kwenye mahusiano huwa sina kupaniki.
Kwahiyo nikajisemea akiwa tayari sawa asipokuwa tayari poa, sasa nimerudi home mida ya 12 nikamtext "Baby get prepared mi naangusha kidogo ukiwa tayari holla up", akajibu "Poa lovie" ikaisha hivyo. Mimi kwenye kujiandaa huwa sichukui zaidi ya dk. tano, napiga maji waa shwaa, najilipua wese la Nivea afu namaliza na deodarant langu la roller la bellagio mchezo umeisha.

Basi nikalala kimtindo nikaja shituka ngoma moja unusu, nikajiandaa nikawa nimekaa tu sebleni namsikilizia. Ilivyofika ngoma mbili kimya, nikaona nimvutie waya, piga kama mara tano hivi mchumba haokoti, nikaona siyo kesi nikamtwanga text, "Lovie whatsapp, are u on it?au umehairisha?" Kimya!
Nikasikilizia baada ya nusu saa, nikavuta tena waya haokoti, nikamtext "Don't bother plan changed, naenda kijiji kusip na wana." Kimya! Nikaona siyo kesi labda mchumba kachoka job kalala.

Nikawasha chuma nafika kijiji, nikashusha Guinness smooth 3 kiroho safi, hapo kumbuka ni saa nne ndiyo nashangaa text inatinga "Baby are u vexed?" mwanaume najiandaa kujibu ikatinga ya pili, "Sorry lovie kichwa kinaniuma sitaweza, sorry my boo."

Mara paap nikavutiwa waya, excuses nyingi mi nikamwambia sijamind wala nini na augue pole ntamletea masapta baadaye. Akasema don't bother hajisikii kula ntamuona kesho, basi ikawa imeisha hiyo. Nikaona siyo tabu nikavuta pisi moja inaitwa Queen halafu nikamkumbuka mwanangu Kevoo aje tumonde naye.
Akanipanga anaumwa, nikajisemea leo wakaribu yangu spana mkononi basi nikavunga. Mida mida text ikaingia "Baby utakua hapo kijiji au utahama?" Mi nikarespond kiutani "Mgonjwa usiniambie umemiss mjulubeng mara hii hahhhaa, sina vibe nikitoka hapa mazima home." Nikajibiwa "Emoji la cheko, nope baby just take care usilewe sana", kiukweli sikuhisi kitu nikajua tu labda mawivu yake nikavunga.

Basi tumepiga vitu na Queen tukahimia Diamond, napo tukasip ilivyofika ngoma nane tukahamia The Dream. Sasa pale The Dream parking ipo sehemu ya lodge, yaani unapaki lodge ndiyo unajivuta lounge kupiga masanga.

Kilichonistua ni ile napark nikakuta gari la mchumba, moyo ukapiga paa! Aisee niliduwaa asikwambie mtu, manusura niparue Vnane la wadosi fulani. Mtu mzima nikapaki bado sielewi, Queen akaniuliza vipi? Nokamwambia mood tu imekata we chukua boda usepe mi napumzika kidogo narudi home.Manzi akataka kunipeti nikamkata dry, akaona hii kali bora asepe. Akaniambia mi nasepa, nikamwambia poa nikamchapa 30 ya boda afu nikavunga.

Nimekaa parking kama dk 20 mlinzi akanifuata bro vipi, ikabidi nimwambie kuna manzi namsikilizia nilivyoona ananiletea kiwingu nikamkata 10 basi poti akafurahi hadi akaniambia, "Bro hata ukisepa ntahahakikisha hata nzi hagusi huu mchuma", nikasema poa.

Moyoni nikasema sisepi hadi nione itakuwaje leo, roho ikawa kama inanitema dizaini kama kuna dude limenikaba kooni, nikasema sikubali nikamvutia mchumba waya, ikaita wee, deshi nikavuta ya pili ikaaita wee ndiyo ikapokelewa. Nikamuuliza "Ulikuwa hujalala mama?" "Kichwa kinaniuma hata usingizi sipati, nipo kitandani tu nachezea simu", nikasema poa, nikaminya red, nanda ikakata.

Halafu moyoni nikajisema au nisepe? Itakua gari kamuazima shosti ila upande wa pili ukakataa nikasema sisepi hadi nihahakishe....

......Inaendelea Down......
 
Mapenzi mashenzi!!

Mkuu lakini na nyie mlikuwa mnasuburi nini kuoana mkaishi wote? Huenda labda bidada aliona huna mpango akaamua kuanza kujipa raha mwenyewe.
big no!

baada ya kuona jamaa hana mpango wa kuoa, bas angeolewa kwingne yangekuwa maamuzi ya busara.

alichokifanya ni uhuni tu al-maarufu kama "umalaya" wala huyo sio mke bora.

nakumbusha: mwizi hapendi aibiwe!
 
Back
Top Bottom