Mtoa mada alisema yule mdada baada ya kupewa pesa nini kiliendelea kwake???Afya ya Akili ni tofauti na Afya ya Mwili,
Afya ya Mwili ni lazima vipimo vya maabara vihusike na Afya ya Akili ina sessions zake japo kuna indicators zinaweza kutokea na ukahisi huyu ana tatizo la afya ya akili utaingia nae kwenye therapy ili kujipa uhakika.
dawa nikumpa hela feki.Na vp mzee alimpatia pesa kweli au
"Uzi nimeusoma na kuuelewa vema na ndio maana nikahitimisha kua huyo Mama ana tatizo la Afya ya Akili hakuna timamu angeweza kufanya hayo aliyoyafanya na nikaongezea tena kua huna uelewa wa Afya ya Akili ndio maana umechukulia kiuwepesi,"
Swali lako lilijibiwa hapo
Naomba nikupe maana ya Afya ya Akili[emoji54][emoji54][emoji54] yaani comment hio hio unayojibu unauliza swali liko wapi tena dr wetuu??
Anyway ngoja basi nikuwekee ???
Wewe umajuaje ya kua ana tatizo la kiafya..?
Umenilisha maneno,Ahaaa, twende vzr, nakunukuu mwenyeweee
"wewe una tatizo la afya ya akili"
"Kwa kukujibu ni kua sijagundua kama una tatizo la afya ya akili sababu sijaingia kwenye session na wewe"
Haya tumeweka kumbukumbu vizuri, Rudia kama huja ni attack....
Vizurii, na asante kwa elimuu,Naomba nikupe maana ya Afya ya Akili
Ni hali ya kuwa sawa kiakili na kisaikolojia na kutokuwepo kabisa kwa usumbufu wa akili ya mtu, mfano msongo wa mawazo, hali ya kuwa na mawazo chanya, kuwa sawa kijamii na kuweza kuchangia katika utendaji wako wa kila siku na uwezo wa kuridhisha wa kimawazo na kitabia.
Naimani hapo umepata mwanga ili kujua kua Mtu ana tatizo la Afya ya Akili basi atakua kinyume kwenye maana hiyo hapo juu,
Kujibu swali lako ni kua huyo Mwanamke alionesha kukosa kufanya matendo ya utimamu au matendo chanya ndio maana akawa anatukana watu na kuwadhalilisha, hapo ndipo aligundulika ana tatizo la Afya ya Akili au Akili yake imekosa utulivu na utimamu.
Nadhani mada ililenga maongezi sijui kama kuna tukio alilifanya zaidi ya majibizano kati ya mwanamke, mtoa mada, konda, dereva, na abiria wengine, na kwa mujibu wa mtoa mada.Umegundua mama ana tatizo la akili kwa aliyofanya au kuongea...
Mbona sijaelewaa.
Ahaa sawaa, tukiweka neno ITAKUA, inaondoa dhana ya kwamba ume ni attack?Umenilisha maneno,
Sikukwambia "wewe una tatizo la afya ya akili"
Nilikwambia "ITAKUA NA WEWE UNA TATIZO LA AFYA YA AKILI"
Rudi kwenye lugha hiyo 'Itakua' imesimama kwenye kuhisi na sio hitimisho ni kama vile ningesema "Inawezekana na wewe...." au ningesema "labda na wewe..."
Vizurii, na asante kwa elimuu,
Kwahio kumbe katika MAZINGIRA tunayozungumzia kutukan na maongezi yake ndio yalimfanya aonekane ana tatizo la kiafya,
Haya Baada ya kupewa pesa kanyamaza kimyaa, hii imekaaje Dr.?
Hiki ndio nilikua nataka, kumbe maongezi ndio yamemfanya aonekane ana tatizo la kiakili, baadae alivyoshuka chini wa nje hata hakuweza kumjua, jee ni kwa nini alitulia.Nadhani mada ililenga maongezi sijui kama kuna tukio alilifanya zaidi ya majibizano kati ya mwanamke, mtoa mada, konda, dereva, na abiria wengine, na kwa mujibu wa mtoa mada.
Jibu lako litakua kuongea
Kumbuka dr yule hakua anaongea sbb ya kutaka refund, ila maongezi yake yalikatishwa na ile pesaa.Nikirejea kwa mtoa mada alisema Dereva alitaka kumshusha mara ya kwanza, akatetewa, na baadae abiria wote wakakubali ashushwe na kuna mzee alijitolea kumpa pesa za kukidhi safari yake na za ziada hivyo Bus lilivyosimama akapokea pesa na kushuka na akaonekana anaongea na konda wa Bus lingine,
Sidhani kama alikua ana sababu ya kuendelea kuongea wakati ameshapata refund,
Ama wewe ulikua na maoni gani kwenye hilo?
Yes, sijaku attack na ni vema tukarejea kwenye convo ilipoanzia pale nilipokukwoti na kukuelewesha kua na positive mind badala ya negative mind, huko ndipo yalianzia lakini nilikutaka radhi kama ulihisi umekua attacked sijajua kwanini umelileta tena,Ahaa sawaa, tukiweka neno ITAKUA, inaondoa dhana ya kwamba ume ni attack?
Ulitaka afanye nini akiwa nje wakati wabaya wake aliwaacha kwenye gari?Hiki ndio nilikua nataka, kumbe maongezi ndio yamemfanya aonekane ana tatizo la kiakili, baadae alivyoshuka chini wa nje hata hakuweza kumjua, jee ni kwa nini alitulia.
Inawezekana tatizo lake la akili lilitulizwa na Pesa,Kumbuka dr yule hakua anaongea sbb ya kutaka refund, ila maongezi yake yalikatishwa na ile pesaa.
Labda uniambie tatizo lake la akili linasababishwa na pesa akipata anapona.
Hapo Nakubalii.
Mgonjwa mwengine huyu hapa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Huyo ni mmeru...... Km Kuna nyoka na mmeru, inatakiwa unamuua mmeru unamwacha nyoka aende
Matatizo ya akili is realTupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.
Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.
Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"
Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.
Akajibu "Wee naweee, haya andika..."
Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.
Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"
Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,
Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"
Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa
Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"
Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia
Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).
Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)
Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.
Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"
Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?
Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.
Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.
Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"
Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.
Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".
Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza
"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."
ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.
Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.
Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".
Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.
Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.
Sisi tukasepaa.
Ahaa kule ndio kuna chanzoYes, sijaku attack na ni vema tukarejea kwenye convo ilipoanzia pale nilipokukwoti na kukuelewesha kua na positive mind badala ya negative mind, huko ndipo yalianzia lakini nilikutaka radhi kama ulihisi umekua attacked sijajua kwanini umelileta tena,
[emoji38]
Pesa alipokea ndani ya gari na kuanzia pale akaa kimya, kumbuka alikua alikua ana react kwa kila kile.., iweje tuu achukue watoto akae kimya baada ya pesa?Ulitaka afanye nini akiwa nje wakati wabaya wake aliwaacha kwenye gari?
Na hapo hatujui kwenye hilo bus lingine nini kilitokea ama kuna muendelezo wake?