Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
- Thread starter
- #161
Pamoja na kwamba mwanamke alikua na wewe kuanzia ukiwa starting line je alikua na mchango gano katika iyo safari? Hoja yako umeiweka katika namna ya kuonyesha kwamba katika mahusiano mwanamke anafanya favor kuwa na mwanaume.Ila pia ukifikanikiwa kumpata aliye tayari kuwa na wewe kuanzia kwenye mwanzo wa marathon yako, mheshimu sana. Kwa sababu ya ugumu mkubwa ulioko kati ya starting line na finishing line mara nyingi mwanamke akiambatana na wewe kwenye safari hii lazima afike kwenye finishing line akiwa kachoka, kasahau fashions n.k. Tukumbuke tulipotoka, tuwapende na kuwaheshimu sana wanawake wema waliosimama nasi tulipokuwa hatuna kitu.
Umasikini wa mwanamke sio tatizo la mwanaume, mahusiano ya kimapenzi sio favor ambayo mwanamke anamfanyia mwanaume isipokua ni hitaji la wote.
Watu wengi mwanamke akiwa masikini hamuoni kama umasikini wake ni tatizo isipokua mnafikiri tatizo ni yupo kwenye mahusiano na mwanaume asiekua na hela.
Mwanaume masikini, mwanamke masikini lakini watu wanafikiri kwamba mwanamke anamfanya favor kuwa na uyo mwanaume.
Ndio maana uko juu nikasema, sawa alikua nawe kuanzia starting line mpaka finish line lakini je alikua na output ipi katika iyo safari. Alikua na mchango wa kifedha, ushauri, network, connection, faraja n.k?