Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #21
Mimi nimeamua tusifanye mpaka ndoa
Hiyo ni sahihi Kabisa kama naye atakusubiri.
Zaidi kama wewe ni Bikra
Hapo ndipo shughuli ilipo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nimeamua tusifanye mpaka ndoa
Nadhani ni sahihi hiyo Mahari ungelipiwa wewe...Aziz alikosea sana😉Je,ni sahihi single maza with 2 kids kulipiwa mahari ya 30M plus fuso 2 za mombe?😊
Siku moja hebu andika mada kwa wanaume jinsi ya kupata milioni 20 kwa.mwaka .anzia na m 20 Tu . Maana wewe unawaza Tu wanawake halafu ndoa yako itakuwa mbaya hata shetani atakuwa anakucheka
Bikra sina ila tumeafikianaHiyo ni sahihi Kabisa kama naye atakusubiri.
Zaidi kama wewe ni Bikra
Hapo ndipo shughuli ilipo
Mkuu hiyo mbinu ni Kwa ma lofa tu, mi kitambo nilisha set radar nawa pima.Mbinu ya KUKABIA JUU inaenda kuwa game changer kwenu wabishi
kikao kinachofuata hatukualiki umetoa siri za kambiNa Mbinu ya KUKABIA JUU haijawahi kushindwa.
Diamond Platinum huoni anajaribu kufurukuta Lakini Zuchu amekamia Mechi.
Upiganaji wa Zuchu unafaa kwa Watu Aina ya Diamond na kataa Ndoa.
Yaani unakabiwa juu alafu king'ang'anizi kiasi kwamba wanawake wengine wanakosa Nafasi hata nukta kujaribu bahati yao
Fact
Nime cheka kwa sauti😆😂Siku moja hebu andika mada kwa wanaume jinsi ya kupata milioni 20 kwa.mwaka .anzia na m 20 Tu . Maana wewe unawaza Tu wanawake halafu ndoa yako itakuwa mbaya hata shetani atakuwa anakucheka
Mkuu hiyo mbinu ni Kwa ma lofa tu, mi kitambo nilisha set radar nawa pima.
Kisha waki jaa nawa lima
Mimi nimeamua tusifanye mpaka ndoa
Sasa mond ndio reference ya wanaume wote?, yaani wewe ujanja wako una fanana na wa nasibu!🤓🤓
Kuna maspesheli wa hizo mbinu utakuja kuniambia.
Muulize Diamond
kikao kinachofuata hatukualiki umetoa siri za kambi
Sasa hapo una mfundisha awe ndoo ya mtaa!Hiyo mbinu nzuri. Na ukiimudu hiyo unaweza kuwa na wanaume hata 10 umewapa nafasi ya potential husband bila madhara kwako.
Atakaewai kukuoa ndie anakula tunda.
Usijifunge kuwa na mmoja tu siku akiondoka unakuwa amekupotezea muda kwa hasara
Hiyo mbinu nzuri. Na ukiimudu hiyo unaweza kuwa na wanaume hata 10 umewapa nafasi ya potential husband bila madhara kwako.
Atakaewai kukuoa ndie anakula tunda.
Usijifunge kuwa na mmoja tu siku akiondoka unakuwa amekupotezea muda kwa hasara
kuwa na busara mi mwenyewe maneno ya dharau nayajua sana tu.Nadhani ni sahihi hiyo Mahari ungelipiwa wewe...Aziz alikosea sana😉
By the way karibu #Kataa Ndoa Siti yako ipo wazi mkuuNimewasaidia Mkuu wasijesema Kaka Yao Nina Roho mbaya
Alafu mbinu ya KUKABIA JUU mara nyingi ndio watu hujikuta wanahonga Mpaka majumba.
Mwanamke anayetumia mbinu ya KUPAKI BASI mara nyingi hata wakiolewa maisha yao huwa ya shida Sana. Hawatunzwi
By the way karibu #Kataa Ndoa Siti yako ipo wazi mkuu
Elimu nzur Kwa sis vijana wakileoWANAWAKE WENGI WANAOFANIKIWA KUPATA NDOA NI WALE WANAOKABIA JUU
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuna Mbinu mbili za kupambana. Kuna wale wanaotumia Mbinu ya KUPAKI BASI na MBINU YA KUKABIA JUU
1. MBINU YA KUPAKI BASI
Hawa ni wale kwenye mahusiano ambao wanasubiri Mpaka mwanaume afuate taratibu zote. Aende nyumbani kwa Wazazi ajitambulishe, atoe sijui Mahari na taratibu zingine za kiutamaduni.
Mbinu hii ilikuwa mbinu yenye Tija kwa nyakati za zamani Kipindi ambacho Mila za kijadi na wazazi walikuwa na nguvu dhidi ya watoto wao.
Ninaposema nguvu ninamaanisha Wazazi walikuwa full responsible na majukumu ya kimalezi. Ikiwa ni pamoja na kuacha urithi kwa watoto.
Kwa zamani pia jukumu la Mahari lilikuwa jukumu la familia ya Mwanaume hasa Baba.
Hivyo kijana wa kiume jukumu lake ni kutoa taarifa kwa Wazazi kuwa amepata Mchumba sehemu Fulani au wazazi wanasema wamemtafutia kijana wao Mchumba.
Na shughuli za Posa na Mahari zinaratibiwa na Wazazi wa kijana.
Wajibu huu wa Wazazi ndio uliwapa nguvu Wazazi kuingilia mahusiano ya vijana wao na wakiamua waliweza kuyavunja Kabisa.
Pia wajibu huu ndio uliifanya desturi ya kuchaguliwa Mke kuwa Jambo la kawaida na kijana asingeweza kufurukuta kukaidi.
Kifupi Mwanamke aliolewa na Ukoo Mzima WA mwanaume kwa Sababu ukoo au familia husika ilihusika kutoa Mahari.
Lakini Mbinu hii imejikufa Kifo cha ASILI baada ya wazazi kushindwa vibaya kutimiza jukumu Hilo.
Zama hizi kijana ndiye mwenye jukumu la kuhangaika mwenyewe Kutafuta mwenza wake na kujitafutia Mahari.
Mila ya kujitafutia Mahari kwa kijana mwenyewe imekuja na faida na hasara Zake.
Hasara Mojawapo ni vijana kuchelewa Kuoa.
Wazazi kutokuwa na nguvu na Mamlaka kwenye mahusiano ya vijana wao.
Mabinti waliolewa kutoona nguvu ya wazazi wa mwanaume kwa Sababu hawana nguvu yoyote ya kuamua lolote ndani ya Mahusiano Yao.
Ndoa kuachana kwa urahisi.
Mabinti hawakuwa na njia yoyote zaidi ha kutumia Mbinu ya KUPAKI BASI mpaka pale mwanaume atakapokuja nyumbani kumchumbia na kumuoa.
2. MBINU ya KUKABIA JUU
Mbinu hii ni matokeo ya vijana kuachiwa jukumu la kuchagua mwenza na kutafuta Mahari Kwa mwenza wake.
Jambo hili limefanya vijana wengi kuchelewa Kuoa na wengine kufikia Hatua ya kutooa Kabisa.
Wanawake wengi wamejikuta wakibadili Mbinu na kuiacha Ile Mbinu ya KUPAKI BASI.
Kumsubiria mwanaume Mpaka aje nyumbani kwao imekuwa Kusubiri Embe kwenye mti wa Mpapai.
Wanawake wengi wameamua kuishi kinyumba na Wanaume na kuzaa watoto Kabisa. Kisha baada ya Miaka mingi ndio huna kubariki ndoa.
Mbinu ya kumfuata mwanaume ili akuoe ndio huitwa MBINU ya KUKABIA JUU.
Katika Mbinu hii inakanuni zake kama zilivyokanuni za Mbinu ya KUPAKI BASI.
Ni kosa kubwa mwanamke ku-date na mwanaume na kushiriki tendo la ndoa huku kila Mmoja anaishi kivyake. Hilo ni kosa la kiufundi ambalo wanawake wengi wanalifanya.
Huwezi kushriki tendo la ndoa na kijana alafu hajakuoa alafu hamuishi pamoja. Ni kutengeneza mazingira ya kutumika na kuachwa kirahisi Kabisa.
Ni Bora uamue Moja, utumie Mbinu ya Kusubiri Kabisa nyumbani na usifanye ngono na huyo kijana Mpaka Akuoe.
Au uamue kwenda kuishi naye Kabisa moja kwa Moja kiunyumba muanzishe maisha yenu. Kisha baadaye mtafunga Ndoa.
Kisheria, Kukaa na mwanamke au mwanaume kiunyumba, nyumba Moja Kwa zaidi ya miezi sita tayari huyo kisheria hiyo ni Ndoa.
Lakini ku-date na mwanaume hata Miaka Saba au kumi, lakini kila mtu anaishi kivyake hautambuliki kama Mke na Mume hapo hakuna Ndoa.
Utagundua kuwa, Njia Bora ni Bora ukabie JUU, ukaishi na huyo kijana wote sehemu Moja ili ijulikane Moja kama atakufukuza tokea mwanzoni au atakubali ukaze humohumo ndani ya nyumba. Hapa kuna Mbinu nyingine za kimedani.
Binti yangu usiwe Mjinga.
Ndoa ni ya watu wawili tuu. Yaani mwanamke na mwanaume tuu. Wengine ni mashahidi tuu.
Ndoa sio lazima pawepo na wazazi, sio lazima pawepo na Askofu au Sheikhe, ndoa sio lazima iwepo serikali ndio ifungwe. Ndoa ni yenu wawili. Sisi wengine Tu mashahidi tuu.
Usikariri Mbinu. Badilika kulingana na Dunia inavyoenda. Angalia ni Mbinu ipi utaitumia itakupa unafuu na faida.
Usijesema Babaako sikukuambia.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam