Ina feli vipi wakati haikuanza?
Sasa nazungukaje na jambo lipo bayana na wazi. Wewe unajua utamu wa ndoa wewe. [emoji23][emoji23][emoji23] Sio utamu wakuwa na bwana maana unaweza hata lala na mume wa mtu, konda wa daladala, bodaboda, muhuni yaani unaweza kulala na mtu yoyote.
Ila NDOA bwana ina heshima na raha yake.
Hebu wazia. Upo kwenye ndoa yako ya halali. Mumeo anarudi kazini watoto wanaruka ruka baba yao karudi kazini wakati wewe upo jikoni ukimuandalia msosi.
Anaingia sebuleni mnasalimiana mnaongozana kuelekea chumbani kwenu, sio geto, CHUMBA CHA BABA NA MAMA WANANDOA.
Vitoto vinajisemesha semesha kwa baba yao vikinokoleana, "Baba junior kalamba sukari mchape" [emoji23][emoji23][emoji23] ,baba yao anajibu haya mwanangu ntamchapa baadae", kengine kanasema baba halafu Brighton hajalala mchana na yeye mchape, baba anajibu " haya baba ntamchapa baadae mwanangu mzuri," haoooo mnaingia chumbani unamuuliza mume wako wa NDOA habari ya kazini anakujibu kwa mahaba "Salama, m'meshindaje?" Unaendelea nakuzungumza nae mkijadili moja mbili tatu kuhusu familia yenu halali ya NDOA.
Acha kabisa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using
Jamii Forums mobile app