Wanawake wenzangu naombeni ushauri: Umewahi kukutana na kulifanya jambo hili?

Wanawake wenzangu naombeni ushauri: Umewahi kukutana na kulifanya jambo hili?

Akili za Wanawake bhana,
Yaan kijana humpendi ila vyake unakula na bado unawaza aendelee kukupa vingine
 
1. Mjane anatembelewa na kijana mdogo anaedai kutaka mtindi wa ng'ombe-mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu

2.mjane anabadilishana namba na kijana mdogo -mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu

3.mjane na kijana wanatambulishana majina ikiwemo yale ya utotoni-mjane anaendelea kukunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu

4. Mjane anavutiwa na jina kijana mdogo-mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeief

5.mjane anapiga stori na kijana mdogo adi usiku wa manane-mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu.

6.mjane anapokea misaada kutoka kwa kijana mdogo-mjane anaendelea kukunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeief

7.mjane anaendekeza ukaribu na kijana mdogo-mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu

8.mjane anatumia gari ya kijana mdogo-mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeief

9.kijana anamkaribisha mjane geto kwake akapaone-mjane anachekacheka anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu.

10.mjane anaendelea kumzungusha kijana huku alijua nia yake-hata hivyo mjane anakunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu.

11.baada ya kuona huu sasa uboya kijana anaweka wazi nia yake kwa mjane-mjane anajitoa ufaham anaendelea kukunja pesa ya kijana mdogo na haombi ushauri Jeiefu.

12.kijana anamwambia mjane wakacheki afya kabla ya kuzagamuana(kijana anataka kuzaa na mjane)-mjane anachekacheka na kumjibu kijana mdogo "sawa" na haombi ushauri Jeiefu


13.mjane anabaini kumbe yale maziwa mtindi ilikuwa gia tu ya kijana kuingilia-hata ivyo mjane anapuuza hayo yote na kuendelea kukunja pesa ya kijana bila kuomba ushauri wowote kwa mwanasheria wake wala hapa Jeiefu

14.Baada ya kijana kuona rasilimali zake zinateketea na hapati majibu yaliyonyooka anaamua kusitisha huduma-mambo ya msingi ya mjane yanakwama maana alishaanzisha ujenzi madale kwa ela ya kijana.

15.baada ya kusisitiziwa atoe utam, mjane anashtuka na kufungua macho na kugundua kuwa;

(i) kumbe yule kijana mfadhili wa muda mrefu ni mdogo na ivyo sio "my type"

(ii) mjane ni mweupe (sijui kaambiwa na nani) na ivyo yule kijana mfadhili wa muda mrefu sio "my type"

(iii) mjane ana shepu na ivyo kijana mfadhili wa muda mrefu sio "my type"

(iv) kajigundua ana 39 na ivyo yule kijana mfadhili wa muda mrefu sio "my type"

(v) ana sauti ya kumtoa nyoka pangoni na ivyo yule kijana mfadhili wa muda mrefu sio "my type"

Hivi tumeishia wapi wajamen?
 
Habari wanaJamiiForums.

Mimi ni mama wa watoto 2 wakike. Sipo kwenye ndoa kwa sasa Mume wangu alifaliki miaka 6 iliyopita.
Na kifo chake kiliniacha maumivu makali sana sihitaji kukumbuka kabisa. Kwani niliona watoto wawili wa kiume(mapacha) wanaumri kama wa mtoto wangu wa kwanza na wamefanana hivyo hivyo na Baba yao.

Ni kitu kilinishitua sana na kuniacha na maumivu makali sana. Sasa ni single mother nilijaribu kumove on ila mtu yule alikuwa ni mume wa mtu nilikuja kujua baada ya miezi 7 kwenye mahusiano.

Sasa wanawake wenzangu naombeni ushauri kwa hili mimi ninaishi tuu na watoto wangu na ninajishughulisha na salon ya kike ni kibwa sana, pia nauza na vinywaji kama soda na juice.

Sasa miezi kama 9 iliyopita nilifahamiana na kijana mmoja anaumri wa miaka 27 kwenda 28. Mara nyingine sipendi mazoea na wanaume nawaona kama ni waongo tu. Lakini huyu nilimzoea kwa sababu la jina lake ni la kabila letu means wote ni kabila moja.

Alijua maisha yangu ninayoishi kwani alikuwa anakuja kununua mtindi sana maana nauza na mtindi.

Tulibadilishana namba za simu na kuwasiliana , na kuna kipindi tukawa hata tunapiga story hata night.

Nilimzoea kiasi cha kujua maisha yangu na kuanza kuniasidia hasa watoto wangu.

Kiukweli alinisaidia sana tena sana, nikawa ninamshukuru kwa lile, pia alinisaidia kuninunulia hata baadhi ya Vifaa vya salon vya kisasa kwenye salon yangu. Kwa kweli ukalibu nae uliongezeka.

Yeye anafanya kazi na ana gari na mishe zake zingine.

Sasa ishu ni kwamba kama 3 weeks ago aliaanza kuniambie kuwa ananihitaji mimi nikufahamu home kwake niende nipajue na kupiga nae story. Alivyoniambia hivyo nikajua nia yake ni nini. Kusema ukweli nilimzungusha kama 1 week hivi.

Ila mwishowe akaanza kunitongoza siunajua vijana. Sasa sikumjibu lolote kwani sikutana kumjibu vibaya kwa urafiki tulionao. Tena akaenda mbali zaidi na kuniambie usijali tutapima ili tuwe safe dear. Nikamwambia sawa tu dear.

Wanawake wenzangu naombe ushairi mimi mama nina 39 japo ndio nina mvuto na ni mweupe kiasi na shape yangu na sauti yangu hii. Nimeshidwa kumkatalia wala kumjibu vibaya.

Ila naona ni kijana mdogo tena wakumvulia chup* kweli. Naona kama nikifanya hivi anaweza hata tangaza kwa vijana wenzie, maana ndo tabia ya vijana wadogo. Pia katika maisha yangu sijawahi kusexy na kijana mdogo tena aliyenizidi umri zaidi ya 10 years, wote niliokutanao wamenizidi mimi umri.

Pia nahitaji kuanzisha bishara nyingine aliniambie atanisaidia.

Sasa kama kuna mwanamke mwenzangu amewahi kutembea na kijana mdogo aliyemzidi umri kiasi hicho hata kama sio hivyo anipe experience kidogo nijue namna ya kudeal ni hii.

Karibu mwenzangu.
MWANZO 4:7

“Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”

UWE NA SIKU NJEMA
 
Sasa kipenzi na misaada yake basi asipokee naona hana pa kukwepea na hapo anakwambia mambo ya biashara mpya ameambiwa atasaidiwa tena

Na kingine ukisoma vizuri mwanamke mwenzetu ni kwamba na ye ameshampenda jamaa sema anaona aibu ya umri tu
Uyo hajampenda jamaa
umaskini TU unampeleka puta
Angekua na kipato keshamtolea nje MDA Sana uyo kijana
 
Vile wanaume nasi tuko busy tunaandaa notes za kufa mtu za kumnasua bibi kizee alienasa kwa kijana mtana shati😁😁😁
AIPysi.jpeg
 
Kwa huyo maza ni mvulana tena kivulana kidogo kwenye hili naona wengi mmeathirika na huu utandawazi mnawaona celebrties wakiishi hivyo lkn kwenye jamii zetu hii haifai kabisaa, yupo aunt yangu kaolewa na mwanaume anaemzidi 12 yrs,,, ila mateso anayopata asalaleeeee alikuwa pisi ya kwenda, imeenea idara zote sura somalia tako beseni guu la bia rangi ya mtume ila kapururuka hatamaniki sababu ya huyo barobaro wake
Unamshaurije, na vitu alivyotumia atavirudisha vipi?
 
Back
Top Bottom