Wanawake weusi chukueni miaka 5 tena,mna mwonekano mzuri na wakizalendo, hamjajichubua

Wacha makasiriko
 
Jamaa umeandika umemaliza wazo la Sadaka hata mimi nimejikuta nakuunga mkono
 
Maneno yao si mageni jijini..!! 😹

Nimekumiss pia wifi yangu mzuri na mpole.. πŸ₯°
hiyo mpole nimecheka sana kuna tukio nimekumbuka..

nilikuwa najijua mimi ni mpole mpaka siku nipo na rafiki zangu mahali kuna kaka akataka kutuletea ukorofi niliruka kwenye kiti mpaka chini nikaenda kumrushia teke ambalo alikwepa na halikufika hata usawa wa tumbo..

ila akilini mwangu nilikuwa nawaza nimpige teke la kichwa kama kwenye movie..!πŸ₯Ή

Vincenzo Jr na dosho12 mtaniponza siku moja..
 
SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, kuna taarifa!

MTOA TAARIFA (N'yadikwa): Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, naomba kutoa taarifa.

SPIKA: Endelea kutoa taarifa yako.

MTOA TAARIFA(N'yadikwa): Mheshimiwa Spika, nataka kulipasha bunge hili wezeshi la jf kuwa nimefuatilia kwa makini hoja iliyotolewa na mwanabodi, ambapo amewasifu wanawake weusi kwa upekee wao, haiba yao ya asili na namna wanavyobeba thamani ya utu, urembo na ustahimilivu.

Mheshimiwa Spika, nataka kuliambia jukwaa hili kuwa kwa kauli hiyo ya mdau, mimi kama mzalendo N'yadikwa na mwana wa Afrika, siwezi kubaki kimya. Nikiwa na akili timamu namuunga mkono kwa dhati kabisa!

Mheshimiwa Spika, wanawake weusi si tu ni nguzo ya jamii zetu, bali pia ni nembo ya uzuri wa Kiafrika, ujasiri, na ustaarabu. Wamebeba majukumu ya familia, wamepigania uhuru wa asili yetu, si wanafiki wa kuiga yasiyo yao na wanaendelea kuonesha kuwa rangi nyeusi ni nzuri mnoo na inavutia.

Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo, naomba kuhitimisha taarifa yangu kwa kusema: "Mwanamke mweusi ni fahari ya dunia, si kwa rangi tu bali kwa utu, hekima, na thamani ya kipekee aliyonayo."

SPIKA: Mtoa hoja unapokea taarifa?!

MLETA HOJA: Napenda kumuunga mkono ndugu yangu N'yadikwa kwa kukazia hoja na kujazia nyama. Asante sana
 
πŸ˜…πŸ˜… Punguza kuangalia movie za ngumi na vita ndugu yangu. Sasa hyo siku si walikucheka mno 🀣🀣
 
Wifi ulijikuta jet li 😹😹
 
Unajua kutangaza matangazo ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…