Wanayanga, msisuse timu yenu kwa maamuzi ya kihuni ya Mtu mmoja.

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,898
Reaction score
40,547
Jana usiku pale Mlimani City imedhihirika Eng Hersi anataka kuitumia Yanga kwa manufaa yake kwa gharama yoyote hata kama ni kuiingiza timu matatizo ya kikanuni.
Hakuna kikao cha timu kilichokaa kwa niaba ya timu ya Yanga na kufikia maamuzi ya kutoa milioni 100 wakati wanachama wanahimizana kuchangia timu. Siyo rahisi mhitaji kama Yanga kuanza kuchangia mwenye shibe kama CCM.
Ni dhahiri aliyofanya Eng. Hersi Jana ni maamuzi yake binafsi na yanalenga kumnufaisha yeye na siyo timu ya Yanga.
 
Kuitenganisha Yanga na CCM ni kujitoa tu ufahamu. Hata asingekuwa Hersi, mwingine kwa nafasi yake angefanya hicho hicho kulingana na mahitaji ya kisiasa yanavyotaka. Ni kama wale wanaomsema Samia. Tatizo siyo Samia.

Tatizo la nchi hii wengi hawajalijua au wanajifanya hawalijui. Kulaumu watu binafsi ni dalili za uoga au ujinga.
 
Mashabiki wa hizi timu kumbuka ni wananchi ambao wengine ni wahanga wa mfumo kandamizi unaofanywa na CCM.

Watu hao pengine walikuwa wakiitumia Club kama sehemu ya wao kujifariji baada ya kuumizwa na CCM.

Unaposema watu wasisusie timu pengine unaweza kuwa na lengo zuri lakini kwa upande mwingine ni kama unafikisha ujumbe kwa hili kundi lililobeba maumivu kuwa mapito yao na majeraha yao hayana mashiko yeyote.

Kwa watu waliopoteza ndugu zao kwasababu ya CCM. Sidhani kama wataweza kuona thamani ya utu inaweza kuzidiwa na mapenzi ya Club kiasi waone huu ushauri wako uko rational.
 
Wanaosusa ni WAJINGA.

Badala ya kususa kwenye mambo ya msingi yanayoathiriwi mustakabali wa vizazi vyao, wanawekeza energy kwenye mambo ya burudani. Shenzy type
 
Jana usiku pale Mlimani City imedhihirika Eng Hersi anataka kuitumia Yanga kwa manufaa yake kwa gharama yoyote hata kama ni kuiingiza timu matatizo ya kikanuni.
Hakuna kikao cha timu kilichokaa kwa niaba ya timu ya Yanga na kufikia maamuzi ya kutoa milioni 100 wakati wanachama wanahimizana kuchangia timu. Siyo rahisi mhitaji kama Yanga kuanza kuchangia mwenye shibe kama CCM.
Ni dhahiri aliyofanya Eng. Hersi Jana ni maamuzi yake binafsi na yanalenga kumnufaisha yeye na siyo timu ya Yanga.
Je una uhakika hizo Hela zimetoka kwenye mfuko wa yanga?,
 
Mashabiki wa hizi timu kumbuka ni wananchi ambao wengine ni wahanga wa mfumo kandamizi unaofanywa na CCM.

Watu hao pengine walikuwa wakiitumia Club kama sehemu ya wao kujifariji baada ya kuumizwa na CCM.

Unaposema watu wasisusie timu pengine unaweza kuwa na lengo zuri lakini kwa upande mwingine ni kama unafikisha ujumbe kwa hili kundi lililobeba maumivu kuwa mapito yao na majeraha yao hayana mashiko yeyote.

Kwa watu waliopoteza ndugu zao kwasababu ya CCM. Sidhani kama wataweza kuona thamani ya utu inaweza kuzidiwa na mapenzi ya Club kiasi waone huu ushauri wako uko rational.
Scars,
Wewe ni platinum member wa Jf kama Mimi. Nafahamu uzito wa michango yako jukwaani. Lengo la ushauri wangu ni kuwaonyesha uhalisia àmbao hata wewe unajua Wazi Hakuna Mwanayanga aliyemtuma Hersi apeleke mchango wa kisiasa jana pale Mlimani City. Ni ngebe na kujipendekeza kwake tu kutaka kupata umaarufu binafsi ndo kulikopelekea afanye aliyofanya.
 
Kuitenganisha Yanga na CCM ni kujitoa tu ufahamu. Hata asingekuwa Hersi, mwingine kwa nafasi yake angefanya hicho hicho kulingana na mahitaji ya kisiasa yanavyotaka. Ni kama wale wanaomsema Samia. Tatizo siyo Samia.

Tatizo la nchi hii wengi hawajalijua au wanajifanya hawalijui. Kulaumu watu binafsi ni dalili za uoga au ujinga.
Unataka tumlaumu Nani wakati aliyekabidhiwa timu kajichukulia maamuzi binafsi ya ovyo? Mimi si Mwanayanga lakini naamini Hersi kajipendekeza yeye Kwa faida yake binafsi.
 
Je una uhakika hizo Hela zimetoka kwenye mfuko wa yanga?,
Hili swali lako linataka kutuaminisha kwamba viongozi wa yanga ni waongo waongo sana, hata kwenye mambo mengi wanayowaambia wanayanga inabidi wasiyaamini moja kwa moja sio? Kifupi ni wahuni tuu
 
Unataka tumlaumu Nani wakati aliyekabidhiwa timu kajichukulia maamuzi binafsi ya ovyo? Mimi si Mwanayanga lakini naamini Hersi kajipendekeza yeye Kwa faida yake binafsi.
Huku ndio tunaita kujitoa ufahamu. Yanga haijawahi kuficha uswahiba wake na CCM. Ni upofu wa kimwili, kiroho, kifikra na kishabiki kama hauoni hilo.
 
Hili swali lako linataka kutuaminisha kwamba viongozi wa yanga ni waongo waongo sana, hata kwenye mambo mengi wanayowaambia wanayanga inabidi wasiyaamini moja kwa moja sio? Kifupi ni wahuni tuu
Communication skills with situation analysis and lobbying
 
Kabla ya kufanya hivo hiyo hoja ingepelekwa kwenye kamati,wajumbe au bodi yoyote ya Yanga hakuna ambaye angeafiki alichofanya Hersi
 
Scars,
Wewe ni platinum member wa Jf kama Mimi. Nafahamu uzito wa michango yako jukwaani. Lengo la ushauri wangu ni kuwaonyesha uhalisia àmbao hata wewe unajua Wazi Hakuna Mwanayanga aliyemtuma Hersi apeleke mchango wa kisiasa jana pale Mlimani City. Ni ngebe na kujipendekeza kwake tu kutaka kupata umaarufu binafsi ndo kulikopelekea afanye aliyofanya.
Kwa busara nataka nichangie hoja yako kwa mtazamo mpana wa kujenga, hususan kuhusu ushzuri wako wa kuwataka mashabiki wa Yanga wasisusie timu licha ya maamuzi ya kihuni yaliyofanywa na kiongozi mmoja.

1. Kususia inaweza kuwa kama njia ya kutoa adhabu ya kijamii/mashabiki
Mfano wa karibu: Kama mtoto akifanya kosa na mzazi akaendelea kumpa zawadi bila kumkemea, mtoto huyo hatatambua kosa lake wala kujifunza.

Vivyo hivyo, kama mashabiki hawataonyesha hasira yao kwa kususia timu, viongozi wa klabu hawatapata ujumbe kuwa wamekosea. Watadhani kila walichofanya ni sawa, na wataendelea kurudia makosa hayo kwa sababu:
  • Hakuna athari ya moja kwa moja kwao.
  • Wanajua mashabiki ni “wafia timu” watasapoti tu bila kujali maumivu yao.
  • Wanatumia udhaifu wa mashabiki kama kinga ya kufanya maamuzi ya kibinafsi bila uwajibikaji.
  • 2. Sababu ya Kiongozi Kuchukua Maamuzi Bila Ridhaa ya wanachama/Mashabiki
Ingawa hakuna aliyemtuma Eng. Hersi kuwasilisha mchango kwa CCM, kuna uwezekano mkubwa alifanya hivyo kwa imani kwamba mashabiki hawatamchukulia hatua yoyote.

Pengine alijua kwamba
  • Mashabiki hawana utaratibu wa kuwawajibisha viongozi.
  • Hakutakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa timu.
  • Mashabiki wataendelea kuja uwanjani, kununua jezi, na kuchangia bila kuuliza maswali.

Swali la Tafakuri​

Je, tunaweza kusema mashabiki wasisusie timu, ilhali viongozi wa klabu wanatumia jasho lao kuunga mkono taasisi inayowaletea maumivu? Je, mashabiki hawa wana sababu ya kuendelea kuisapoti timu bila kujua kesho pesa yao itapelekwa wapi?

Kwa heshima, kususia siyo chuki ni njia ya kutoa ujumbe. Ni namna ya kuonyesha kuwa mashabiki si wa kupuuzwa, na kwamba mapenzi yao kwa klabu hayapaswi kutumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa.
 
Kususa ni njia mojawapo ya kupeleka ujumbe
 
Muitikio mitandaoni na mitaani imeshafikisha ujumbe kwa aliyefanya uhuni ule. Japokuwa Ally Kamwe amekosa Weledi kuliongelea kijinga zaidi, lakini haihalalishi mashabiki nao kuanza kuisusa timu. Na kama kweli viongozi Wana akili wasithubutu kutengeneza makundi ya kuhalalisha tukio Hilo ambalo wanajua Wazi timu ya Yanga haijachanga fedha hiyo.
 
Kwa busara nataka nichangie hoja yako kwa mtazamo mpana wa kujenga, hususan kuhusu ushzuri wako wa kuwataka mashabiki wa Yanga wasisusie timu licha ya maamuzi ya kihuni yaliyofanywa na kiongozi mmoja.

1. Kususia inaweza kuwa kama njia ya kutoa adhabu ya kijamii/mashabiki
Mfano wa karibu: Kama mtoto akifanya kosa na mzazi akaendelea kumpa zawadi bila kumkemea, mtoto huyo hatatambua kosa lake wala kujifunza.

Vivyo hivyo, kama mashabiki hawataonyesha hasira yao kwa kususia timu, viongozi wa klabu hawatapata ujumbe kuwa wamekosea. Watadhani kila walichofanya ni sawa, na wataendelea kurudia makosa hayo kwa sababu:
  • Hakuna athari ya moja kwa moja kwao.
  • Wanajua mashabiki ni “wafia timu” watasapoti tu bila kujali maumivu yao.
  • Wanatumia udhaifu wa mashabiki kama kinga ya kufanya maamuzi ya kibinafsi bila uwajibikaji.
  • 2. Sababu ya Kiongozi Kuchukua Maamuzi Bila Ridhaa ya wanachama/Mashabiki
Ingawa hakuna aliyemtuma Eng. Hersi kuwasilisha mchango kwa CCM, kuna uwezekano mkubwa alifanya hivyo kwa imani kwamba mashabiki hawatamchukulia hatua yoyote.

Pengine alijua kwamba
  • Mashabiki hawana utaratibu wa kuwawajibisha viongozi.
  • Hakutakuwa na madhara ya moja kwa moja kwa timu.
  • Mashabiki wataendelea kuja uwanjani, kununua jezi, na kuchangia bila kuuliza maswali.

Swali la Tafakuri​

Je, tunaweza kusema mashabiki wasisusie timu, ilhali viongozi wa klabu wanatumia jasho lao kuunga mkono taasisi inayowaletea maumivu? Je, mashabiki hawa wana sababu ya kuendelea kuisapoti timu bila kujua kesho pesa yao itapelekwa wapi?

Kwa heshima, kususia siyo chuki ni njia ya kutoa ujumbe. Ni namna ya kuonyesha kuwa mashabiki si wa kupuuzwa, na kwamba mapenzi yao kwa klabu hayapaswi kutumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa.
Kususia chako ni kujipa adhabu au kukiharibu
Nadhani Yanga ni Mali ya Wanachama na mashabiki kwaiyo Wanachama hatupaswi kususia timu yetu
Labda tuwakatae hao viongozi ikiwa ni pamoja na kuwatoa madarakani kama wanavuka miiko na kanuni za FIFA ili kujinufaisha wao Kisiasa bila kujali kama FIFA wakipata hizi taarifa timu yetu yaweza kupata adhabu Kali
Eng Hersi Said atoke wazi aombe radhi
 
Back
Top Bottom