Hoja hii inashindwa kutofautisha kati ya kususia kwa lengo la kurekebisha na kususia kwa lengo la kuharibu.
Mashabiki wanapogoma kuhudhuria mechi au kununua jezi, si kwa sababu hawapendi timu yao, bali kwa sababu wanataka viongozi waelewe kuwa maamuzi yao yana madhara.
Yanga mlikataa kucheza derby ya tarehe 15 kama njia ya kulalamikia maamuzi ya TFF ya kuahirisha mechi ya tarehe 8 Machi bila maelezo ya kuridhisha. Mlitaka viongozi wa TFF wawajibike, wengine hata kujiuzulu. Hili halikuonekana kama kuitelekeza timu, bali kama kusimama kwa misingi ya haki na uwajibikaji. Kwa nini basi mashabiki wakifanya hivyo kwa klabu yao, iwe ni kosa?
Kuwawajibisha ni pamoja na kuweka mgomo
Mgomo ni sauti ya kusema "sisi si wa kupuuzwa" na kweli kama Yanga ni ya wanachama basi sauti yenu inapaswa kusikika kwa vitendo na sio maneno tu.
Alishawahi kumnadi Samia kwa kumpigia kampeni na yeye pia kujipigia kupitia jukwaa hilo hilo la Yanga, unategemea kuona tabia hii ikikoma kwa wao wenyewe kujisahihisha?