Wanayanga, msisuse timu yenu kwa maamuzi ya kihuni ya Mtu mmoja.

kanuni za Fifa ziko wazi hakuna kuhusisha michezo na siasa, yanga walituaminisha wana viongozi wenye weledi mkubwa ni wazi wamefanya makusudi inabidi wawajibishwe.
 
Kususia timu sio kuharibu ni kufikisha meseji na kurekebisha nidhamu.

Ni kweli Yanga ni mali ya wanachama lakini hiyo haimaanishi mashabiki wasiwe na namna ya kuonesha kutoridhishwa kwao kwenye mambo mabovu kama haya.

Kususia timu ni namna ya kuwathibitishia viongozi kuwa mashabiki sio wa kupuuzwa ni njia ya kuleta nidhamu kwa viongozi wa Club.

Ni muhimu kufahamu kuwa tayari kuna watu wameanzisha kampeni ya kuzitaka mamlaka za juu za soka FIFA na CAF zichukue hatua kufuatia sakata hili. Hii inaonyesha kuwa jambo hili si la kupuuzwa, na linaweza kuathiri hadhi ya klabu kimataifa.

Nisionekane nasema haya kwa sababu mimi ni shabiki wa Simba, ambaye kiasili ni mpinzani wako na muda wote nakuwazia mabaya—hapana. Hata kama lingetokea upande wa Simba, bado ningeungana na watu wanaoshauri njia sahihi za kuwawajibisha viongozi. Maadili hayana jezi. Haki haichagui rangi ya timu.
 
Kususia timu ni kuitelekeza timu
Sisi tunataka Yanga iwe hai na shindani siku zote
Changamoto za uongozi haiwezi kufanya tususie Mali yetu, labda tuwaondoe au kuwawajibisha viongozi
 
Kususia timu ni kuitelekeza timu
Sisi tunataka Yanga iwe hai na shindani siku zote
Changamoto za uongozi haiwezi kufanya tususie Mali yetu, labda tuwaondoe au kuwawajibisha viongozi
Hoja hii inashindwa kutofautisha kati ya kususia kwa lengo la kurekebisha na kususia kwa lengo la kuharibu.

Mashabiki wanapogoma kuhudhuria mechi au kununua jezi, si kwa sababu hawapendi timu yao, bali kwa sababu wanataka viongozi waelewe kuwa maamuzi yao yana madhara.

Yanga mlikataa kucheza derby ya tarehe 15 kama njia ya kulalamikia maamuzi ya TFF ya kuahirisha mechi ya tarehe 8 Machi bila maelezo ya kuridhisha. Mlitaka viongozi wa TFF wawajibike, wengine hata kujiuzulu. Hili halikuonekana kama kuitelekeza timu, bali kama kusimama kwa misingi ya haki na uwajibikaji. Kwa nini basi mashabiki wakifanya hivyo kwa klabu yao, iwe ni kosa?

Kuwawajibisha ni pamoja na kuweka mgomo

Mgomo ni sauti ya kusema "sisi si wa kupuuzwa" na kweli kama Yanga ni ya wanachama basi sauti yenu inapaswa kusikika kwa vitendo na sio maneno tu.

Alishawahi kumnadi Samia kwa kumpigia kampeni na yeye pia kujipigia kupitia jukwaa hilo hilo la Yanga, unategemea kuona tabia hii ikikoma kwa wao wenyewe kujisahihisha?
 
Una hoja nzuri
Me sikupingi kila mwenye akili timamu amechukizwa na Kitendo cha Rais wa Yanga kuchangia CCM michango yetu sisi wana Yanga masikini kuwapa wanyonyaji bila kikao maalum.
Lakini hatua ya kususia ni kubwa mbona tuna mikutano mkuu September 7, tutambana atujibu
 
Haya ndo mawazo yangu pia kwenu mashabiki wa Yanga.
 
Wanachama itabidi wambane vizuri SANA Hersi kuhusu hili jambo kwenye kikao Cha tarehe 7 September. Wanachama pia wawe na msimamo mmoja.
 
Exactly [emoji817]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…