Tunachotakiwa kufahamu, ni kwamba jaji hupatikana kutoka jamii yetu. Rais anapatikana kutoka jamii yetu.
Jamii ikiwa na watu wengi wanafiki, waongo, wala rushwa, waoga, basi uwezekano mkubwa:
1) Rais atakuwa na sifa hizo hizo
2) Mawaziri watakiwa wa namna hiyo hiyo
3) Majaji watakuwa wa namna wa namna hiyo hiyo
4) Polisi watakuwa wa namna hiyo hiyo
Inakuwa ni kwa bahati sana, kumpata mtu tofauti na walio wengi katika jamii. Watu hao waliowahi kuwa tofauti na walio wengi, ndiyo kama Mwalimu Nyerere, Warioba, Jaji Lugakingira, Jaji Samata, Jaji Augutino Ramadhani, Jaji Nyalali. Sasa kwa vile walio tofauti ni wachache, ni lazima kuwe na mfumo unaolazimisha kwenye nafasi kama za Urais, jaji, wapatikane watu kama hao. Bahati mbaya mfumo huo hatuna.
Bahati mbaya zaidi, uchaguzi wa mwaka 2015, ulimwingiza Rais asiye na vigezo kabisa, aliyeamini kuongoza kwa kutumia nguvu, udikteta na hila. Ili atawale kwa namna anayoitaka bila bugudha, aliua Bunge, aliua mahakama. Mahakamani akawajaza maofisa wa TISS. Hawa wote waliohusika na kesi ya Mbowe, siyo majaji, ni maofisa wa TISS ambao marehemu aliwajaza mahakamani ili kuua mhimili wa mahakama.
Siku tukibahatika kumpata kiongozi jasiri, mwenye hekima, upeo mkubwa na weledi, hawa maaifa wa TISS, wote wanatakiwa kuondolewa mahakamani. Lakini cha muhimu zaidi ni katiba mpya ambayo italazimisha upatikanaji wa majaji kwa vigezo vya sifa na uwezo.
Bahati mbaya jamii yetu pia imejengwa na watu waoga, na wanafiki kupindukia. Huu ujinga mwingi unaofanywa na watawala, mahakama na bunge, ni matokeo ya unafiki na uoga wa sisi wananchi.
Angalia hata hapa jukwaani, watazame watu kama Jingalao, Cremia, Chinembe, Stroke, qnd the like, ukitazama michango yao unaweza kudhani ni brainless, lakini yawezekana wana akili timamu lakini akili yote imemezwa na unafiki. Wao hata kitu ambacho ni dhahiri kabisa kuwa ni cha hovyo, alimradi kimefanywa na mtu wa CCM, au kiongozi ndani ya Serikali, hata kiwe takataka kwa kiwango gani, watasifia. Hata huko mitaani, watu wa namna hiyo ni wengi. Kuwategemea watu wa namna hiyo kuleta mabadiliko nchini mwetu, ni ndoto. Wao kila kitu hakuna cha muhimu, kikubwa ni matumbo yao. Wengi wanawaza fedha na vyeo.
Kwa ujumla, kwa sasa, majaji wengi hawa waliochongwa na mwendazake ni wala rushwa wakubwa, weledi ni zero, kujipendekeza 100%. Baadhi ya ninaowafahamu, pamoja na hawa walioendesha kesi ya Mbowe na wenzake, ni hovyo kabisa, hata kama wangeondolewa huko TISS, wakabakizwa mahakamani, uwezo wao ni mdogo kuliko hata mahakimu wa Wilaya, wale wenye uwezo.