Wanyonge wenzangu, bei ya Saruji huko kwenu ipo vipi?

Wanyonge wenzangu, bei ya Saruji huko kwenu ipo vipi?

23,0000 unaona ni kawaida? Halafu haya makampuni ya sementi kucheza na soko kwa kuamua kuumiza watu wa miji fulani haijakaa sawa. Bahati mbaya watu wako busy kusubiri viapo. Hawa inapaswa wawe wanapewa adhabu retrospective.
Ni makampuni ama serikali yako imeweka makodi lukuki?
 
23,0000 unaona ni kawaida? Halafu haya makampuni ya sementi kucheza na soko kwa kuamua kuumiza watu wa miji fulani haijakaa sawa. Bahati mbaya watu wako busy kusubiri viapo. Hawa inapaswa wawe wanapewa adhabu retrospective.
kwamba uliwasaidia mtaji?
 
Mfumuko wa bei ni kitu kibaya sana, ukichukulia na hali mbaya za watanzania wengi zilivyo kiuchumi, hakika tutateketea.

Hapo bado hatujawekewa vikwazo vya kiuchumi na mabeberu kwasababu ya ule uchaguzi feki uliofanyika, mbona tunakwenda kuwa Zimbabwe.
Uchumi mbaya ni kwako tu, tz tuko uchumi wa kati mfuko wa siment hata uuzwe elf 50 watz wengi tu tutamudu kununua!
 
Nilikua najenga ka servant quotta kangu imebidi niache, simenti imetoka 18,500 hadi 24,000.

CCM hata tukiwapa miaka 500 hakuna kitu cha maama watatufanyia.
Kwani unafikiri wana mapenzi mema na wananchi? Hawa wapo kwa ajili ya matumbo yao tu.
 
Hatari sana...

Gharama za ujenzi kuongezeka, Gharama za makazi kuongezea, gharama za maisha kua juu...



Cc: mahondaw
 
Lissu aliwaahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi, ila hamkumchagua mkataka mitano tena. Na mfumuko wa bei uwaangamize !
 
Inapaswa ipande zaidi ya hapo kwa sasa.Hata ikifika laki itakuwa bado bei ya chini..
 
Inapaswa ipande zaidi ya hapo kwa sasa.Hata ikifika laki itakuwa bado bei ya chini..
Kosea Kuoa Lakini Siyo Kuchagua Ukikosea Kuchagua Ni Mpaka Baada Ya Miaka Mitano
Haa😁😂😅😄😄😃😃😁😂
 
Kosea Kuoa Lakini Siyo Kuchagua Ukikosea Kuchagua Ni Mpaka Baada Ya Miaka Mitano
Haa😁😂😅😄😄😃😃😁😂
Mkuu kuna mambo ambayo sijawahi shangaa nikisikia watu walalamika kuhusu mfumuko wa bei huwa sielewi hata kidogo.

Hayo yote tmejitakia na ni HAKI YETU.Ni stahiki zetu hizo kama ilivyo mahitaji muhimu ya binadamu kuna hili moja kwa watanzania kulalamaaaa weeeee...wakati maamuzi yanafanyika tunajifanya wahariri na mashujaa wa kubeza.

Nasema hiivi hata mfuko ufike milion na kama wenye nyumba wanasikia watie tu mfuko wa kodi za nyumba upae zaidi.

Kuna sehemu wote tukielewa,ndio akili zitakaa sawa.
 
Hao watakuwa mawakala wakubwa ambao wanachukua mifuko 5,000 na KUENDELEA.sasa inapotokea Mambo Kama haya ndo hayo Mambo ya kuangaliana usoni wa kumpa cement yanatokea.
Cement HAIJAPANDA BEI Bali haipatikani.
Sasa hapa ndipo watu wanaamua kuuza wanavyotaka wao maana wanajua una shida nayo hata wakikuambia PC's 1 ni 50,000 utanunua Kama hautaki nenda
Kwenye magodown huko inasemekana cement inatolewa kwa vi note
 
Na bado subiri shilingi ishuke thamani mpaka iwe 5000 kwa $1
 
Viwanda vingi vya Cement mwisho wa mwaka huwa vinakuwa kwenye matengenezo ya karibu miezi miwili. Inawezeka hiyo ndo sababu ya Cement kuadimika na gharama kuwa juu.
 
Hili suala la uhaba saizi viwanda vingi haviwezi kuzalisha maximum production sababu ni zaidi ya mwezi hawajaagiza malighafi za kutengenezea cement. Hivyo vingi vinatumia malighafi walizokuwa nazo awali na kuzalisha Kwa kiwango cha kawaida ingawa uhitaji huku sokoni ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom