Wanywa pombe kali huwa mnajiuliza swali hili mkiwa mnakunywa?

Kwa mfano leo wewe na mimi tumekufa, lakini wewe umekufa huku maini yako bado mazuri sana, na mimi nimekufa huku yangu yana matobo kisa pombe, MAINI YAKO MAZIMA HUKU UKIWA UMEKUFA YANA FAIDA GANI TENA?
Unakosea sana.Kufa kwa uzembe ni tofauti na kufa kwa bahati mbaya.
 
Unywe usinywe utakufa tu na kwenda kuwa msosi wa funza na mchwa afsa..
Sikia nikuambie mzee, nature inasema kuna kuzaliwa kuishi na kufa..sasa usi justify kunywa sumu sababu unajua kuna kufa, hizo kama.ajali n.k zinazotokea ni uncertainities za kimaisha, you are at wrong place at wrong time, na kuna kufa kwa uzembe wako, kufa kwa kua muda umefika(Gods plan) na kuna kufa kwa uzembe wa mtu/watu wengine ..
 
Sio swala la.kuishi milele.mkuu. sumu hizo.zinaua
Sasa unywe sumu sababu unajua kua kuna kufa. Hio ni akili ama matope. Mungu amekubariki.kukupa miaka 80 ya kuishi, wewe unaipunguza kwa kusema sababu kuna kufa ngoja ninywe sumu(pombe kali).
Hivi utajuaje kwamba miaka yako umeipunguza? Unamaanisha kwamba kuna mtu anajua miaka yake ya kuishi?
 
Agiza fanta orange mkuu, uilipe mwenyewe.
 
Utajifariji kwa kejel hizi ila acha pombe sumu acha kuwapa utajir wenye makampun ya pombe huku wewe ukiangamia na kuiweka familia kwenye mateso makubwa
Ubaya wa pombe huja pale mhusika anashindwa kunywa kwa kiasi
 
Mkishazeeka ndio mnajifanya kuacha pombe
 
Ukichunguza kwa makini utagundua Watu wa sekta ya afya ndio wanywaji wazuri wa hizo pombe kali..
Kuna kitu tunafichwa hapa
 
Hata Soda ukinywa uncontrollably utapata matatizo hayo hayo. Uwe na kiasi tu kwenye ulaji na unywaji wako iwe alcoholic drinks au soft drinks.
 
Daah, akili imekimbilia kwa TYCOON wa K-VANT...jamaa pesa ipo nyingi sana...tangu enzi za Kiroba Original

Na Bado K-VANT inanunulika kinoma mtaani
 
Huyo tajiri Hafi?
 
Embu naomba uelezee mechanism ya pombe kali mpaka kuunguza ini mjulishaji.
 
Mkishazeeka ndio mnajifanya kuacha pombe
Kwanza huwezi kuthibitisha mtu kazeeka.

Pili, hata kama kweli, isn't that the point? Unafanya mabalaa yote udogoni ukishakua unaacha?

Tatu, kama unataka kunywa kunywa tu, kwani kuna mtu kakukataza?

Unahamaki nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…