Wanywa pombe kali huwa mnajiuliza swali hili mkiwa mnakunywa?

Majibu ya wanywa pombe watakayokujibu hapa sijui kama utarudi tena,wewe hujiulizi mtu mpaka anafilisika kwa pombe kwanini anashindwa kuachana na kampani za pombe,kila akijaribu kujitoa wanampa maneno ya kumtia moyo, na ukitoka utakandiwa kuonesha wewe ni mmoja wa watu wa hovyo kuliko yoyote yule ambaye alishawahi kutokea,waache,dalili za kuumwa zikishaanza huwa wanajitoa wenyewe kimyakimya...
 
NILICHOJIFUNZA KWENYE MADA HII YA BWANA felakuti NI KWAMBA WATU WENGI SANA;
1. Wamekariri vitu vingi sana kwamba vipo kwa namna hii au ile, lakini hawana hoja za kutetea walichokaririshwa
2. Maisha yetu kwa sehemu kubwa yanaendeshwa na mapokeo. Tumepokea imani nyingi sana toka kwa waliotutangulia, lakini hatukuwahi kuhoji why mapokeo hayo yapo hivyo yalivyo
 
Dorpe
 
Usitake kutuaminisha kuwa waliofilisika wote walikuwa wanakunywa pombe..!! Kuna masikini wanywa juisi ujuwe..!!
 
Sasa unataka ufe ukiwa mbichi kama embe bolibo ili iweje?Kwani unaenda kushindana umaridadi/urembo/utanashati kaburini?Kula pombe wewe acha upompompo!Kwanza Yesu akija kututwaa atatupatia miili mipya.Nini shida wewe?
 
Situmii pombe kali,ila unaweza usinywe pombe kali ukafa kwa corona,ajari kama kunagukiwa ghorofa,kaswende, malaria,kisukari n.k,so tusijaji sana hayabmaisha anayajua Mungu tu.
 
Mungu tu atusaidie maana kila kitu siku hizi ni Sumu na Kifo kiko palepale.
 
Halafu pombe kali nyingi Tanzania ni feki na ni sumu halafu TBS wanapata chochote kitu na wenye Mamlaka hupata kijibahasha cha kaki.
 
Kwenye kujaribu vitu ujanani, nimejaribu vingi ila pombe kali ni kitu ambacho sijawahi kukielewa kwa kwel. Yani unakunywa kitu kinakuchoma kooni, bado ukilewa hujielewi. Asee bora mpepe kuliko haya mapombe.
 
Bro nakuhakikishia one unknown day you will be sick on your death bed pamoja na kwamba hunywi pombe wala juisi za viwandani.........
 
Walevi wanajifariji



Acha afya zao zizorote tupite na wake zao

Watanyooka tu
 
Umaskin mkubwa sana mkuu..
Ila wenye kampun hizo za pombe wanaendelea kua matajiri, juzi kuna mmoja kanunua gari ya milioni 700 na wako huko.kwenye mitandao.wanayaonesha mafanikio yao makubwa
Hili jambo hua linanikasirisha sana
Kuna slogan kwenye biashara inasema......ukitaka kupiga pesa mingi, tatua shida za maskini. Wenye akili ameona maskini hawez kununua wine ya laki na kitu, wakaja na visungura vya buku ili maskini nae apate starehe, kumbe ndo kuangamiza vijana, wenyewe wanapiga pesa za maana. Sema pombe kali ni ufala. Kitaa kuna wana wawili wamekata moto ndani ya wiki moja, kwa kunywa haya maspirit ya mchongo
 
Umughaka kwa mala ya Kwanza Leo umenena kwa hekima sana
 
Rekebisha hapo kuwa tajiri anakunya maji πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
Yote kwa yote 2090 wote tutakuwa hatupo πŸ˜₯
Tajiri kumbe upo, siku hizi hata kwenye ile namba yako hupatikana kabisa au umebadili namba 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…