Wapalestina ni wavamizi kwa mujibu wa Quran

Kwakuwa umenukuu biblia nami nitakupeleka huko

Japo mpaka sasa mmeshindwa kuleta hata andiko la kipande cha gazeti kuwa Allah anawatambua WAPALESTINA na hiyo Ardhi aliwapa WAPALESTINA

Surat Al-Isra (17:104)
وَقُلْنَا مِنۢ بَعْدِهِۦ لِبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱسْكُنُوا۟ ٱلْأَرْضَ فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ ٱلْـَٔاخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًۭا
"Na tukawaambia baada yake (Musa) Wana wa Israel: Kaeni katika ardhi. Na utakapofika ahadi ya mwisho, tutawakusanya nyote pamoja."


Kutoka 6:7-8
"Nami nitawatwaa ninyi kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu wenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niwatoaye mtoke katika mizigo ya Wamisri. Nami nitawaleta mpaka nchi ile ambayo naliwaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kwamba nitawapa iwe urithi wao; mimi ndimi Bwana."

Mungu anaendelea kuthibitisha kuwa ardhi ya Kanaani ni urithi wa Wana wa Israeli milele.

Zaburi 105:8-11
"Ametilia agano lake kumbukumbu milele, neno aliloliagiza kwa vizazi elfu, agano alilolifanya na Ibrahimu, na kiapo chake kwa Isaka, akakisimamisha kwa Yakobo kuwa amri, na kwa Israeli kuwa agano la milele, akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, kuwa sehemu ya urithi wenu."

Hii ni mojawapo ya uthibitisho wa wazi kuwa ahadi ya ardhi kwa Wana wa Israeli ni ya milele.
 
Endelea na inavyoelezea kilichofuata baada ya kupewa
 
Hao wapalestina ni watu wa imani gani,? Halafu jiulize ,Je hiyo imani inatambuliwa na ALLAH ama laa?
 

Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya fisadi katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa

Hapo umeelewa nini ?
 
Soma kwa kuelewa umetaja Quran , nimekwambia AYA ina thibitisha kuwa Waisrael ni wavamizi kwa hoja yeyote ile kwasababu walikuta watu hapo

QURAN 2:22
Wakasema:” Ewe Musa! Huko kuna watu majabari . Nasi HATUTAINGIA huko mpaka WATOKE humo; wakitoka humo hapo TUTAINGIA “
 
Ndio ila haindoi kuwa ni wavamizi ambao walitumia nguvu dhidi ya wenyeji
 
Je baada ya kufadhilishwa zaidi ya watu wengine walifanya mambo gani pindi walipoletewa mitume?
Yohana 4:22
"Ninyi mwaabudu msichokijua; sisi twaabudu tukijua; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.

Warumi 3

1 Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?

2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?

4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
 

Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.
Aya zinazozungumzia hiyo nchi na ardhi unazozisema ndo hizi zimeizungumzia pia kuhusu Qurani kama unavyoona hapo juu, Je hao Waisraeli unaowatetea, ni Waislamu ?
 
Nilichogundua waislamu wengi ni maamuma ,hamjui jinsi Allah wenu anavyowatambua Wana wa Israel,

Allah wenu kwenye Quran hawajui WAPALESTINA

Hii mada hamuiwezi nileteeni Mufti mkuu
Shida hii hujui Quran kabisaa , itakuumbua vibaya mno
 
Katika Qur’an na Taurati, ardhi hiyo (Ardhi Takatifu) iliahidiwa kwa Bani Isra’il. Katika Qur’an 5:21, Musa anawaambia watu wake:

"Enyi watu wangu! Ingieni katika ardhi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekujaalieni, wala msirudi nyuma, mkageuka kuwa wenye kukhasirika."

Hii inaonyesha kuwa kwa mujibu wa Qur’an, ardhi hiyo ilikuwa imeahidiwa kwao na Mwenyezi Mungu.
 
Uislamu umeanza mwaka 600s A.D

HISTORIA haidanganyi
 
Halafu unaweza kunukuu ayaat za Quran halafu ukawa huelewi chochote. Hiyo aya uliyoinukuu inaelezea jinsi ambavyo ALLAH amewakusanya mayahudi sehemu moja ili apate kuwafutilia mbali. Soma na aya ya sura 17:4-8 upate kuelewa vizuri.

Wayahudi waliacha imani sahihi ya kumuabudu ALLAH na wakaua sana mitume na mingine mingi wakaikataa...Sasa ALLAH amesema kuwa itakapofika ahadi ya mwisho (zama hizi za mwisho) atawakusanya wote sehemu moja na kitakachofata ni vita kubwa kati ya Waislam na Wayahudi na ndio itakuwa mwisho wa uyahudi na mayahudi hapa duniani.


Mtume Muhammad (pbuh) alisema kuwa hakitasimama Qiyama mpaka pale waislam watakapopambana na mayahudi. Itafikia mahali myahudi atakimbia kujificha nyuma ya jiwe ila jiwe litasema kumuita muislam kuwa nyuma yake amejificha myahudi.
 
Soma 22 nini wayahudi walijibu HAWAWEZI kuingia mpaka wale wenyeji wao watoke mbona jambo lipo wazi sana
 
Uislamu umeanza mwaka 600s A.D

HISTORIA haidanganyi
Kwa mujibu wa Quran uislam ulianza toka kipindi cha nabii Adam a.s. Mwanadamu wa kwanza kuumbwa alikuwa Muislam.

Mitume yote ya Mungu walikuwa ni waislam
 
Hizi ni porojo za Muhammad

Na wewe kabisa unaziamini?
 
Nimekuomba Aya kuhusu kupewa WAPALESTINA,cha ajabu unapiga porojo tu
Kwani katika Qurani au Biblia,kuna sehemu inaonyesha kuwa ardhi ya Tanganyika ndio Ardhi ya Tanzania,ukileta
kesho nakuja kanisani
 
ushaanza kuchanganyikiwa sasa unaleta maneno ya muuaji wa wanafunzi wa Yesu (Paulo)
 
Nimekuomba Aya kuhusu kupewa WAPALESTINA,cha ajabu unapiga porojo tu
Palestina ni jina la eneo sio jamii , ni kama watanzania tu ila ndani unakutana na watu tofauti kama wagogo , wangoni wenye historia tofauti kumbe huelewi kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…