Wapangaji waijulishe TRA kuwa nyumba si zao ili TRA isifanye kosa kuwatoza kodi ya jengo

Kwa kweli..
Watanzania wengi wana mentality kuwa serikali ikifanya hivi basi wapinge tuu..
Nyie ni mawili kama sio watoto mnaopewa allowances na wazazi wenu basi ni vijana ambao m'mepata access ya maisha mazuri so hapa mnakuja kuonyesha udhaifu wenu kupitia arrogance nature mliyonayo.


Katika hali ya kawaida watu wanapolalamika , mtu mwenye upeo na akili inayofanya kazi sawa sawa huwa anajiuliza kuwa hawa watu wamenyang'anywa kitu gani hadi walalamike hivi ?! Ukisikiliza utaelewa.

Watanzania si kwamba hawapendi kuichangia serikali. Ila hawapendi kudhulumiwa. Serikali hii ni ya mkono unaopokea tu na usitoe inavyostahili.

Wamechukua pesa za Deci, wanechukua pesa za Mr. Kuku. Wanachukua kodi kila uchao, wanakopa nje huko mabilioni, wanachukua hela za wastaafu, wanachukua hela za mafao ya watu waliopo makazini, michango ya walimu kila siku wanabeba.

Huoni hii ni too much?!
 
Utakuta kwenye hiyo nyumba Kuna wapangaji watano,yeye anatoa Mia 200 tu, alafu anayelalamika ii yeye
 
Wew unaoongea tu.. kuna mtu ana anamiliki nyumba nyumba kila chumba kina mita yake.. kwa mfano kuna vyumba kumi.. huoni kama kuna 10000/= apo lazima TRA wapite nayo.. mfumo wao na wa hovyo tu kuna miingiliano mingi sana kwenye hili
 
Hivi kweli watu walioshindwa kutafuta vyanzo vya mapato katika nchi iliyojaa utajiri wa kila aina kama hii unadhani wanao uwezo wa kuchambua kupitia mita za tanesco na kujua kuwa hii ni ya mpangaji na hii ni ya mwenye nyumba?
TRA ni moja ya taasisi zinazolipa mishahara na posho nzuri lakini kwa yanayoendelea ni kwamba wamechoka kukusanya kodi na wameamua kukaa na kusubiria makampuni ya simu, tanesco na palipo na mihamala ndio wawakusanyie. Na tatizo kubwa ni kuingiza siasa kwenye hii taasisi nyeti yaani inafanya kazi kama 'mapato' ile ya zamani za Mwalimu badala ya 'revenue authority' huru kama ilivyokusudiwa wakati inaundwa na Merdizedeck Sanare.
Hivi unadhani haya makato ya kukomoana (double taxation) zinazidi mapato ambayo yangetokana na matumizi halisi na sahihi ya EFD machine?
 
Hawezi kukuelewa. Watu wa hivi huwa wanaathiriwa na aina fulani ya privilege. Hawa ndio aina ya vijana wanawekwa wizarani na ndugu zao halafu unashangaa mbona taasisi za serikali zinakuja na sheria za kipumbavu zisizoeleweka, well.... Guess who is always behind .....?! Ni hii sampuli hapa.
 
Urahisi ni kwa mpangaji na mwenye nyumba wakubaliane namna ya kuifidia hiyo kodi ya nyumba toka katika malipo ya pango anayolipa mpangaji. Unakata tsh 10,000 yako toka katika kiwango cha pango cha baba mwenye nyumba maisha yanaendelea
Hii na me niliwaza.. katika kodi ikatwe hiyo 12000/= ambayo ni ya miez 12. Ishu iko kwenye hizi nyumba zenye mita zaidi ya moja.. kuna nyumba inamiliki mita hata 5. Hili inabidi mwenye nyumba kwa hali ya haraka aliport mahala husika isajiliwe nyumba 1 zilizobaki zitolewe katika mfumo haina kutia uvivu maana itakula kwake pale wapangaji watapompa kodi wakiwa wamekata na kodi ya jengo.. let say una mita 5 ×12000=60000 matokeo yako wazi kabisa
 
Kabisa mzee kabisa yaani......
 
Kabisa mzee kabisa yaani......
OK, japo mambo hayajawahi kuwa vizuri kihivyo lakini miaka miwili iliyopita tulikuwa tukipewa mrejesho wa trillion 1.3 za makusanyo na aliyetaka details ya kipi kimetoka wapi zilikuwepo (japo kimagumashi). Sasa focus ni kama imehamia kwingine
 
ASIPOKUELEWA HUYO NI MBUMBUMBU!
 
Ila kwa kuondoa kero ni bora kubaki nazo mita zote. Maisha ya kushea luku ni magumu sana. Yana kero
 
Sh.50 ni way low kulinganisha na 1000-10,000. Its likely you dont feel the pinch wangeweka hio 50 kwenye kila sehemu it would make a lot of sense kuliko kuweka %
Hoja yako haina uhusiano na kodi ya majengo(property tax)ya kutozwa 1000/= kila mwezi kwenye LUKU(jumla 12000/=kwa mwaka).😂😂Naona hapo umechanganya madesa!!!
 
Ndugu zangunu watanzania, lipeni/changieni hizi pesa pesa/ 1000 tu ili watoto wetu wote wanaokwenda chuo kikuu wapate mkopo. Ili isiwe kama sasa kuanza kubaguana eti wewe uliyesoma kayumba tu au ni yatima ndio upate mkopo. Mkopo uwe kwa wanafunzi wote walioomba bila kujali ulisoma private au la.

Vya bure tunavitaka, kuchangia mkono mfupi ila harusi na vikoba tuko mstari wa mbele. Acheni ujima, changieni tusonge mbele.

48 BILIONI zimeshakusanywa toka kwenye miamala na 22 bilioni toka kwenye mafuta kwa mwezi mmoja. Na hizo pesa zimeshaelekezwa kwenye vituo vya afya na ujenzi wa barabara za vijijini ili mazao yakakusanywe vizuri.

Mama mitano tena.
 
Hujajitambua bado.
 
Kuna post humu nimesema hii kitu. Kweli mtu ana nyumba analalamika kodi ya jengo 1,000/- kwa mwezi? Wabongo tunalalamika sana ndio maana serikali wanapuuza tu.
 
Kama ni hivi tutaiuliza serikali zile kauli za nchi hii ni tajiri na kusikia namba za tozo za madini zilivyokuwa zikiongezeka imeishia wapi? Mbona sasa ni kauli za tozo aka kodi za kichwa kila mahali?
Ndugu yangu utajiri wa kwanza wa nchi ni watu. Hawa ndio mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa. Na hawa ndio wataotoa tozo/kodi/michango kuendeleza nchi.

Usipoelewa Serikali inatoa wapi pesa, utakuwa katika karne ya ujima au stone period. Amkeni watanzania Tuijenge Tanzania. Kama uko tayari kuiona Tanzania inapaa kiuchumi lazima ufurahi unapoombwa kuchangia maendeleo ya nchi yako.
 
Wapangaji kwenye nyumba nyingi uswahilini hela ya umeme wanalipa 10,000 na wataendelea kulipa hiyo hiyo na hiyo 1,000 ataongeza mwenye nyumba, sioni kelele zinatokea wapi.
 
Elfu moja ukiigawa kwa siku 31 unapata ngapi ili upate kwa siku wanachukua kiasi gani?
Acheni lawama za kijinga.
SWALA HAPA SIO 1000 NI NDOGO KIASI GANI... SWALA KUBWA HAPA NI HIYO HELA ANATAKIWA KULUPA MMILIKI WA JENGO ILA PESA HIYO ITAUMIZA WALE WALIOPANGA KATIKA JENGO HULO IKIWA PESA HIYO INAKATWA KATIKA MATUMIZI YAO YA UMEME SAWA EEH HIYO 1. ISHU YA PILI NI KWAMBA KUNA MAJENGO YANA VYUMBA TOFAUTI MENGINE YANA HADI VYUMBA 10 NA KILA KIMOJA KINA MITA YAKE SAWA EHH KWA IYO KILA MITA WAKIPITA NA HIYO 1000 KWA AKILI YAKO WE UNADHANI KITATOKEA NINI. KWA IYO USICHUKULIE KIRAHISI SANA HII ISSUE
 
Kuna post humu nimesema hii kitu. Kweli mtu ana nyumba analalamika kodi ya jengo 1,000/- kwa mwezi? Wabongo tunalalamika sana ndio maana serikali wanapuuza tu.
Serikali iwapuuze hawa walalamishi. Tanzania itajengwa na watanzania.

Kama tunachukia kweli kutembeza bakuli nchi za nje na kuombaomba misaada, ni lazima tukubali kuchangia.

Amkeni watanzania, kulalamika lalamika hakuna faida.
 
TRA washatoa ufafanuzi. Kama haieleweki nenda ofisi za TRA waambie jinsi nyumba yako ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…