Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni


unajua mambo mengi ya wapare huamuliwa kwa mashauriano. na mashauriano hayo mara nyingi huwa marefu sana mpaka watu wafikie muafaka. na mara nyingi muafaka ukishafikiwa wote walioshiriki ktk shauri hilo hufungwa na maamuzi hayo.

mimi nimeshuhudia hata suala la ndoa za kipare; majadiliano ya posa, wazee wakisimamia taratibu hatua kwa hatua. kwa mfano mahari ya kipare inahusisha matoleo ya mbuzi na ng'ombe. na kuna taratibu za kipi kitangulie. sasa wazee huwa wakali kwelikweli ikiwa mtoa mahari atakiuka hatua ktk suala hilo. ukiacha suala la mali zilizoko ktk mahari kuna suala la mahali ambapo mahari inatakiwa itolewe au ipokelewe. kwa mfano, mpokea mahari anatakiwa aende kwenye boma la mtoa mahari achague yeye ng'ombe anaowataka.

kwa mtu ambaye anashuhudia kwa mara ya kwanza anaweza kudhani anashuhudia mahakama ikifanya kazi. maana zoezi zima huhusisha vijana wenye kumbukumbu nzuri ambao huelezea suala zima toka lilipoanza mpaka lilipofikia. halafu wako wazee ambao ni wajuvi wa mila na taratibu na hao hutoa muongozo, au huingilia kati kunapotokea ukiukwaji wa mila za ndoa.

binafsi naamini makuzi hayo ndio husababisha wapare kuwa na "dna ya kupenda kesi."🤣
 
barabara hii mnayoiona kutoka Same kwenda milimani Chome ilichimbwa na wananchi wa wilaya ya Same kwa utaratibu wa kujitolea. utaratibu huo wa kazi za maendeleo za kujitolea unaitwa "msaragambo."

serikali ya mwalimu nyerere ilikuja kuwapa sapoti wananchi kwa kutoa baruti za kupasua muamba mkubwa ili barabara iweze kupitika. Mwalimu Nyerere alipotembelea Same na kuona wananchi wakijituma ndipo alitamka kwamba , " wapare ni wachina wa tanzania. "

 
Stori za vijiweni hizoo... Kwanza alipigwa na butwaa kukuta kuna vafumwa walioendelea kushinda yeye...
 
Kwetu Upareni kaka kitovu changu kiko huko mahali panaitwa Store Mombasa
Mwaka huu naenda upareni kwetu, Usangi.

Nimemisi sehemu za upareni kwetu kama , chekereni, store Mombasa, Mchali, Kikweni.
 
Asipo kuelewa basi ana tatizo la afya ya akili
 
We muongo. Hakuna mpare anasema kwa ni Moshi. Wilaya za Wapare ni Same na Mwanga
Huwa hawataki kutaja hasa maeneo waliyotoka, yaani Chome, Mwanga, Ugweno na Usangi.

Ukiwauliza wanasema kwao Moshi [emoji23]
 
Mshana Jr
 
Umefika Ugweno kweli wewe? Maeneo ya Mriti, Vuchama Ngofi, Fumbua ng'ombe n.k

Je Kaseni na Sungo?

Mkuu acha kabisa, wenyeji wa huko wenyewe huwa hawarudi makwao na kuishi mpaka leo, wakienda ni kuzika tu na kurudi siku hiyohiyo
 
Ndugai kaenda ugogoni baada ya kutimuliwa bungeni.
 
Kwa sababu Moshi ni ya wachaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…