Watu wa makabila mbali mbali walioko mijini ama mbali na nyumbani (sehemu ya asili yao) mara nyingi wakitaka kusema wanarudi kwao watataja jina husika la mji ama sehem anayotoka... Mfano kwa mchaga atasema naenda moshi... Muhaya atasema naenda bukoba, mngoni atasema ashuka zake songea nk.
Ila inanishangaza kwa wapare... Mara nyingi sana utaskia naenda upareni... Au atamuuliza mtu "hivi lini unapandisha upareni" na wakati wana sehem zao km usangi, ugweno, chome, same nk...
Ni mazoea ama kuna sababu maalum?
View attachment 2443480
Moshi ni makao makuu ya Mkoa Wa Kilimanjaro.
Moshi wanaishi watu Wa MAKABILA Mengi na SIO wachagga peke Yao.
Wachagga wanaishi vijijini kama Rombo, Marangu , Kibosho , Hai, Siha n.k.
Moshi ni Jina la Jumla Kwa wakazi wakazi Wa Mkoa Wa Kilimanjaro mana ndio makao makuu ya Mkoa.
Hakuna sehemu inayoitwa upareni au uchagani. Ndio Maana Hata wachagga hawasemi tunarudi Uchagani Bali wanasema tunaenda Moshi. Kwa HIYO wapare nao hawawezi kusema tunaenda Upareni mana hakuna Eneo linaloitwa upareni Bali kuna Ugweno,Usangi, Same ,Gonja na kadhalika.
Kwa wahaya Nako ni HIVYO HIVYO ,Bukoba ni makao makuu ya Mkoa Wa Kagera . Lakini kuna Ngara ,Muleba,Karagwe,Biharamulo,Kyerwa,Misenye, Kanyigo , Mtukula n.k.
Hatusikii wakisema naenda Mtukula au naenda Muleba Bali naenda Bukoba Hata kama anaishia Biharamulo.
Hata Arusha ,huwezi kusikia MTU akisema ,"Narudi Meru, au narudi Bahati au Loliondo " .Utasikia ," Narudi Arusha" . Anataja makao makuu ya Mkoa Wa Arusha kama center ya Mkoa .
Na pia hii inatokana na shamrashamra za Krismass ambazo zinatiliwa mkazo sana na na Wakristo hasa Wakatoliki.
Maeneo kama Mwanga na Same Katika Mkoa Wa Kilimanjaro hayana Wakristo (Wakatoliki) WENGI . Same wengi ni Wasabato na Waluteri ambao Hawana sana shamrashamra za Krismass. Mwanga wengi ni Waislam. Kwa HIYO zile hamasa za Krismass Kwa wakazi Wa Mkoa huo zinatofautiana SIO kikabila Bali ni kiimani zaidi.