Wapenda haki hatutompa Kura Diamond Platnum kama tulivyokubaliana

Msilipize baya kwa baya,mpeni za kumwaga na atakuwa amejifunza katika hilo unapokuwa msanii nyimbo zako ni za watu wa vyama vyote na mbaya zaidi fans wake ni vijana ambao wengi wapo upinzani.
 
Tutapimaje kama nyie ni watenda haki?
 
Msilipize baya kwa baya,mpeni za kumwaga na atakuwa amejifunza katika hilo unapokuwa msanii nyimbo zako ni za watu wa vyama vyote na mbaya zaidi fans wake ni vijana ambao wengi wapo upinzani.

Hakunaga kanuni ya hivyo Duniani na mbinguni.

Ubaya hulipwa Kwa ubaya
Wema Kwa wema. Tit for tat
 
Nyie nanyi mna chuki zenu za ajabu ajabu khaa!!!

sababu ya kawaida kabisa inayofanya baadhi ya watu wasimpigie kura ni uswahili ,akipata hio tuzo itakua kama fimbo ya kuwachapia wengine.

Lakini hizi chuki zenu za kisiasa aisee inabidi zioungue hazina mantiki yoyote.
 
Kwakuwa Diamond anapambanishwa na wasanii wa mataifa mengine, kwa maana hio ni msanii pekee kutoka Tanzania na pekee kutoka ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki kupeperusha bendera basi kwa kauli moja TUTAMPA KURA KIJANA WETU DIAMOND PLATNUM

Mambo ya siasa na uanaharakati uwepo wa akina Zitto, Mbowe, Lissu unatosha sana ktk uwakilishi

Kwenye soka tunawakilishwa na Samatta, kwenye Music Diamond ndie nembo ya nchi kimataifa

Go go Diamond Platnum,,, You are the true icon of Tanzania Music
 

Kalia chuki hapo.

Ujumbe huu haukuhusu.

Chuki Kwa kipi hasa?

Au umasikini unakusumbua?
 
Maskini hajawahi kumpenda mwenye uwezo
 

Ujumbe umefika, ni kutekeleza tuu Mkuu.
Muda utajibu
 
Kila mtu ana haki ya kupanga ,kuchagua na kufanya kile anachoona kwake Ni sahihi Kwan uyo Diamond Ni nani Hadi Kila mtu amfanyie kinachomfaa.kura n haki ya mtu na Ni Siri .mashabiki zake watampa kura na wengine wampgie kura wanaeona Ni sahihi.
 
Natumaini watakua katika categories tofauti hivyo nawapigia wote.

Ni Haki yako

Ila uzi huu unahusu wanaharakati, wapenda haki, wanamtandao wenye kusomwa na watu wengi. Hatutompa Kura mond ndivyo tulivyokubaliana na ndivyo itakavyokuwa.

So wewe kampe Kura Diamond ni haki yako ili kumfanya apate walau Kura ya kumezea mate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…