Wapenda haki hatutompa Kura Diamond Platnum kama tulivyokubaliana

Wapenda haki hatutompa Kura Diamond Platnum kama tulivyokubaliana

CCM (Ya Dr Bashiru na Prof Polepole) aliokua anawapigia campaign wampitishe bila kupingwa BET AWARDS. Wamehitimu Shahada ya kuiba kura.

Binafsi, Diamond angekua anachuana kwenye hizo tuzo na "FUNGU LA MAVI", basi ningelipigia kura hilo fungu la mavi, ila sio huyo jamaa. Hatetei jamii wala chochote kwa taifa letu, ila anataka yeye atatetewe;

1) Ana dhalilisha wanawake (Kujaza mimba na kuwaacha), as if yeye ndio rijali peke yake.

2) Akisaidia au kutoa msaada basi lazima ajitangaze, wakati mwenzake Alikiba anasomesha shule na kuwalea mayatima kibao na hajitangazi.

3) Hashughuliki kutetea vijana wasio na ajira kitaifa, waliosoma na hawana ajira. Ajira zake kwa vijana anatoa kwa anaowajua tu.

4) Hashughuliki na kutetea uvunjwaji wa haki za binaadamu, anajifanya hayupo kisiasa ila kwenye campaign anakua mstari wa mbele.

5) Hashughuliki na kupaza sauti juu ya uonevu unaofanywa na viongozi wa mikoa na wilaya.

6) Ana haribu jamii, hasa vijana, kuvaa hereni/vikuku n.k
Kama hizi ndio akili za watz wengi tuna safari ndefu sana kufikia uchumi wa juu hv kweli unamuonea wivu mwanaume kumtia mimba mwanamke.
 
Kwakuwa Diamond anapambanishwa na wasanii wa mataifa mengine, kwa maana hio ni msanii pekee kutoka Tanzania na pekee kutoka ktk ukanda huu wa Afrika Mashariki kupeperusha bendera basi kwa kauli moja TUTAMPA KURA KIJANA WETU DIAMOND PLATNUM

Mambo ya siasa na uanaharakati uwepo wa akina Zitto, Mbowe, Lissu unatosha sana ktk uwakilishi

Kwenye soka tunawakilishwa na Samatta, kwenye Music Diamond ndie nembo ya nchi kimataifa

Go go Diamond Platnum,,, You are the true icon of Tanzania Music
Naunga hoja, et watenda haki, ujinga mtupu hata nchi hawajashika et watenda haki
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Mtu anaandika utopolo kama huu maskini tu unakunuka na wivu mkubwa kwa diamond
 
Hii ndio shida ya kuwa na mbunge mmoja , mda mwingi mnajikita kwenye ujinga badala ya kuendeleza chama chenu, kadanganyeni watoto huko nyie ni chadema hakuna wapenda haki wala ukwa
Akili ndogo Sana hawa wanaharakati mavi wanajiita Chademu, namm kura yangu wanapoteza
 
Huu uzi umekaa kiboya boya Sana......unafikiri kura yako moja nyeusi itabadilisha matokeo....... diamond platnumz kama ni kushinda atashinda Tu na kama ni kushindwa atashinda Tu........usiwe group moja na wapumbavu.......kwenye kampeni za ccm ni Nani asiye jua kuwa ccm wanatoa pesa nyingi kulipa wasanii na ndio sehemu Yao ya kurudisha pesa zao za studio....maana wewe na kubwatuka kwako kote hapa oooh anaimba matusi sijui nini ujawai hata kununua kaseti ya zaikO langa langa au muhidini mwinyishehe.......unataka diamond aje Kura na kulala Kwa BABA yako?? Kulikuwa na wasanii wangapi pale kwenye ccm mpaka iwe ni diamond pekee?? Acha wivu butu kenge wewe pambania maisha yako ilimradi the most high amekupa roho yake na pumzi ........au unafikiri tuzo zile ni kama za kirimanjaro uku bongo??.........Kule hakuna fitna wala kujuana kama unajua unajua Tu.....Acha wivu mchko wew
Achana na hao Chademu, wanajifa wao ndio mungu watu
 
Kama hizi ndio akili za watz wengi tuna safari ndefu sana kufikia uchumi wa juu hv kweli unamuonea wivu mwanaume kumtia mimba mwanamke.
🤣🤣🤣🤣

Jamaa anaongea kwa uchungu kweli kisa Diamond kumtia mimba mwanamke mwenye akili zake, sijui alitaka hio mimba abebeshwe yeye mleta mada au dada zake
 
Hakunaga kanuni ya hivyo Duniani na mbinguni.

Ubaya hulipwa Kwa ubaya
Wema Kwa wema. Tit for tat
Ukihubiri utengano ukitengwa usilalamike.
Jpm kila siku mlikuwa mnalia kuwa analeta mpasuko wa kitaifa kwa kuwapendelea ccm. Yani alikuwa anaongoza taifa kwa kufuata itikadi za kichama. Hata kwenye ziara alikuwa akifika sehemu anauliza kama diwani au mbunge ni wa ccm.
Chadema tulilipinga hili sana la kuwagawa watanzania kwa itikadi za vyama vyao.
Lakini naona sasa wanachadema wenzangu mnaelekea kule kule kwamba asiye upande wetu ni adui yetu.
Kama ni kusimamia haki tuisimamie pasipo kujali anayebidi kupata hiyo haki ni nani. Siyo tu kupiga kelele bali tu sisi tunapominywa ila kama kaminywa mwingine tuone sawa.
Diamond na mtanzania yeyote ana haki ya kuwa shabiki/mwanachama wa chama chochote na hiyo haimfanyi kuwa adui mpaka ianzishwe kampeni ya kwamba kwakuwa hafuati itikadi zetu za kisiasa basi asipigiwe kura. Kwa kufanya hivyo hatuna tofauti na ccm wakisema kuwa serikali ya ccm haitampatia kazi mtu yoyote ambaye ni mwanachama wa upinzani.
 
Naomba LEO niandike kidogo,
Mwaka 2008 nilichaguliwa kuwania TUZO za MTV BASE ambazo zilifanyika katika jiji la ABUJA - NIGERIA, Nilikuwa nimechaguliwa kugombea Category Ngumu sana ya BEST HIP HOP ARTIST ambapo nilikuwa nagombea na The GAME, LIL WAYNE na msanii wa NIGERIA anaitwa 9ICE, Nilikuwa Msanii pekee kutoka TANZANIA na nilikuwa nimeambatana na @josephkusaga @kelvin.twissa kutokana na Nafasinzao kwenye MUZIKI wa AFRIKA,
Kwa kweli nilijua kabisa kuwa SITASHINDA kwenye nafasi hiyo kutokana na ubora wa wale watu nguli niliokuwa nashindana nao ila niliona hiyo ni nafasi yangu kubwa na ya kipekee ya kuitangaza nchi yangu na utamaduni wetu na nilivaa vazi ililowavutia wengi VAZI la KIMASAI na nilipewa Heshima kubwa ya kukabidhi TUZO kwa mmoja wa washindi. Kilichotushangaza sisi tuliotoka TANZANIA ni CAMPAIGN ya nchi nzima ya WANAIJERIA ya kuhakikisha msanii wao 9ICE anashinda TUZO hiyo na sio TUZO hiyo pekee bali TUZO zote ambazo Wanaijeria wanagombea, Ilikuwa ni KAMPENI kubwa ya nchi nzima , KAMPENI hiyo iliongozwa na WAZIRI wao wa SANAA na UTAMADUNI sambamba na WAZIRI wao wa UTALII, Nia yao ilikuwa kuwauza wasanii wao wa nchi yao kwa TAIFA lao, Mwisho kwenye Category yetu msanii 9ice alishinda mbele ya JAYZ, LILI WAYNE na Mimi, Binafsi sikuwahi kumsikia kabisa mpaka leo ni miaka 15 imepita sijui hata alishawahi kuimba kitu gani, Kwa mwaka huo zaidi ya asilimia 90 za AWARDS zilibakia Kwa WANAIJERIA,
Hii ina ni funzo kubwa sana kwetu Watanzania kuwa anaposimama MTANZANIA yeyote kugombea TUZO yeyote au jambo lolote Duniani ni lazima tusimame nae pamoja bila kujali Makundi yetu , Itikadi zetu, dini zetu wala makabila yetu maana hapo Inasimama TANZANIA na sio mtu mmoja mmoja,
Kwa MFANO huu wa NIGERIA Nitumie nafasi hii ya muhimu kuwaomba WATANZANIA wote kwa umoja wetu tusimame pamoja na tumsapoti Kijana wetu diamondplatnumz ambae ni msanii pekee wa TANZANIA na anasimama kidete kuiwakilisha TANZANIA kwenye TUZO kubwa za BET aweze kushinda AWARD hii kwa manufaa ya TA

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
WAPENDA HAKI HATUTAMCHAGUA DIAMOND PLATNUM


Na, Robert Heriel


Katika Tuzo za BET Diamond ni moja ya Wasanii wanaowania Tuzo hizo.


Wapenda haki, wanaharakati na Wana mtandao wote kuanzia Facebook, Instagram, JamiiForums, na Twitter Kama tulivyokubaliana hatutampa Kura Diamond Platnum na hatashinda tuzo hizo Kwa sababu ameshindwa kutumia nafasi yake vizuri kuilinda, kuijenga na kuitetea jamii yake.


Diamond hajawahi kutetea jamii ya Watanzania.


Utekaji na mauaji yalivyopamba Moto Diamond alikuwa wakwanza kutoa kibao chenye ujumbe usemao " Acha Nikae kimya" maudhui ya wimbo ule yalilenga kuhafifisha na kutia uoga jamii isipige kelele kuhusiana na vitendo hivyo vya udhalimu.


Diamond ni tofauti kabisa na Wasanii wa Nigeria Kama kina P Square, Burns boy, Davido n.k ambao mara kadhaa walijitokeza kuungana na jamii kuipinga serikali pale inapokosea mpaka kuandamana kabisa.


Diamond hawezi chaguliwa na watu wote walioenda shule, waliostaarabika, wapenda haki na wanaharakati.


Kwa hapa Nchini waliojaribu na wanaojitahidi kutetea haki na kutetea jamii ni kina Ney wamitego, Roma mkatoliki, Profesa Jay miongoni mwa wengine.


Diamond ni Aina ya wanamuziki wanaoiona jamii Kama jamii ya vibushuti sio ajabu ndio maana nyimbo zake nyingi hasa za siku hizi niza vibushuti, zinalenga watu wenye Low IQ.


Diamond Kama angenoga Kama angeimba nyimbo Kama za kipindi kile mathalani "nimpende Nani" ukimuona" Nitampata wapi" lakini sio hizi za Jeje na mfano wa zile za nyoka pangoni.


Kama tulivyokubaliana Kura asipate.


Ili iwe funzo Kwa Wasanii wa kizazi kinachokuja.


Msanii ambaye ni kioo cha jamii badala aungane na jamii yeye anaungana na serikali. Ajabu hii.
Hii ipo katika nchi yetu pekee.


Hata Marekani wenye muziki wao Wasanii wao huwa upande wa wananchi.


Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Roho mbaya haijengi.
 
Waliompandisha ndio hao hao watakaomshusha.....kazi ipo
 
Back
Top Bottom