Wapenda haki hatutompa Kura Diamond Platnum kama tulivyokubaliana

Wapenda haki hatutompa Kura Diamond Platnum kama tulivyokubaliana

🤣🤣🤣🤣

Jamaa anaongea kwa uchungu kweli kisa Diamond kumtia mimba mwanamke mwenye akili zake, sijui alitaka hio mimba abebeshwe yeye mleta mada au dada zake
😄😄 tena unaweza kukuta alieandika hvyo ni mtu mwenye familia au cheo kizur tu kwenye chama cha siasa aiseeee.Wao wanahubiri demokrasia ila hawataki wengine wawe na hyo demokrasia kazi kweli kweli.
 
Ukihubiri utengano ukitengwa usilalamike.
Jpm kila siku mlikuwa mnalia kuwa analeta mpasuko wa kitaifa kwa kuwapendelea ccm. Yani alikuwa anaongoza taifa kwa kufuata itikadi za kichama. Hata kwenye ziara alikuwa akifika sehemu anauliza kama diwani au mbunge ni wa ccm.
Chadema tulilipinga hili sana la kuwagawa watanzania kwa itikadi za vyama vyao.
Lakini naona sasa wanachadema wenzangu mnaelekea kule kule kwamba asiye upande wetu ni adui yetu.
Kama ni kusimamia haki tuisimamie pasipo kujali anayebidi kupata hiyo haki ni nani. Siyo tu kupiga kelele bali tu sisi tunapominywa ila kama kaminywa mwingine tuone sawa.
Diamond na mtanzania yeyote ana haki ya kuwa shabiki/mwanachama wa chama chochote na hiyo haimfanyi kuwa adui mpaka ianzishwe kampeni ya kwamba kwakuwa hafuati itikadi zetu za kisiasa basi asipigiwe kura. Kwa kufanya hivyo hatuna tofauti na ccm wakisema kuwa serikali ya ccm haitampatia kazi mtu yoyote ambaye ni mwanachama wa upunzani.
Umeandika points sana kama waelewa wataelewa.
 
WAPENDA HAKI HATUTAMCHAGUA DIAMOND PLATNUM

Na, Robert Heriel

Katika Tuzo za BET Diamond ni moja ya Wasanii wanaowania Tuzo hizo.

Wapenda haki, wanaharakati na Wana mtandao wote kuanzia Facebook, Instagram, JamiiForums, na Twitter Kama tulivyokubaliana hatutampa Kura Diamond Platnum na hatashinda tuzo hizo Kwa sababu ameshindwa kutumia nafasi yake vizuri kuilinda, kuijenga na kuitetea jamii yake.

Diamond hajawahi kutetea jamii ya Watanzania.

Utekaji na mauaji yalivyopamba Moto Diamond alikuwa wakwanza kutoa kibao chenye ujumbe usemao " Acha Nikae kimya" maudhui ya wimbo ule yalilenga kuhafifisha na kutia uoga jamii isipige kelele kuhusiana na vitendo hivyo vya udhalimu.

Diamond ni tofauti kabisa na Wasanii wa Nigeria Kama kina P Square, Burns boy, Davido n.k ambao mara kadhaa walijitokeza kuungana na jamii kuipinga serikali pale inapokosea mpaka kuandamana kabisa.

Diamond hawezi chaguliwa na watu wote walioenda shule, waliostaarabika, wapenda haki na wanaharakati.

Kwa hapa Nchini waliojaribu na wanaojitahidi kutetea haki na kutetea jamii ni kina Ney wamitego, Roma mkatoliki, Profesa Jay miongoni mwa wengine.

Diamond ni Aina ya wanamuziki wanaoiona jamii Kama jamii ya vibushuti sio ajabu ndio maana nyimbo zake nyingi hasa za siku hizi niza vibushuti, zinalenga watu wenye Low IQ.

Diamond Kama angenoga Kama angeimba nyimbo Kama za kipindi kile mathalani "nimpende Nani" ukimuona" Nitampata wapi" lakini sio hizi za Jeje na mfano wa zile za nyoka pangoni.

Kama tulivyokubaliana Kura asipate.

Ili iwe funzo Kwa Wasanii wa kizazi kinachokuja.

Msanii ambaye ni kioo cha jamii badala aungane na jamii yeye anaungana na serikali. Ajabu hii.
Hii ipo katika nchi yetu pekee.

Hata Marekani wenye muziki wao Wasanii wao huwa upande wa wananchi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kila mtu ashinde mechi zake
 
Kwani lini mmewai mpa kura na akashinda.
Mkuu sisi kama mashabiki wa chelsea bado tuna deni na wewe. Ulituahidi masaburi lakini mwisho ukatokomea kusikojulikana. Kwahiyo sisis kama mashabiki wa chelsea tunaomba ututimizie ile ahadi yetu pendwa kama ulivyoahidi.

Nawasilisha.....
 
WAPENDA HAKI HATUTAMCHAGUA DIAMOND PLATNUM

Na, Robert Heriel

Katika Tuzo za BET Diamond ni moja ya Wasanii wanaowania Tuzo hizo.

Wapenda haki, wanaharakati na Wana mtandao wote kuanzia Facebook, Instagram, JamiiForums, na Twitter Kama tulivyokubaliana hatutampa Kura Diamond Platnum na hatashinda tuzo hizo Kwa sababu ameshindwa kutumia nafasi yake vizuri kuilinda, kuijenga na kuitetea jamii yake.

Diamond hajawahi kutetea jamii ya Watanzania.

Utekaji na mauaji yalivyopamba Moto Diamond alikuwa wakwanza kutoa kibao chenye ujumbe usemao " Acha Nikae kimya" maudhui ya wimbo ule yalilenga kuhafifisha na kutia uoga jamii isipige kelele kuhusiana na vitendo hivyo vya udhalimu.

Diamond ni tofauti kabisa na Wasanii wa Nigeria Kama kina P Square, Burns boy, Davido n.k ambao mara kadhaa walijitokeza kuungana na jamii kuipinga serikali pale inapokosea mpaka kuandamana kabisa.

Diamond hawezi chaguliwa na watu wote walioenda shule, waliostaarabika, wapenda haki na wanaharakati.

Kwa hapa Nchini waliojaribu na wanaojitahidi kutetea haki na kutetea jamii ni kina Ney wamitego, Roma mkatoliki, Profesa Jay miongoni mwa wengine.

Diamond ni Aina ya wanamuziki wanaoiona jamii Kama jamii ya vibushuti sio ajabu ndio maana nyimbo zake nyingi hasa za siku hizi niza vibushuti, zinalenga watu wenye Low IQ.

Diamond Kama angenoga Kama angeimba nyimbo Kama za kipindi kile mathalani "nimpende Nani" ukimuona" Nitampata wapi" lakini sio hizi za Jeje na mfano wa zile za nyoka pangoni.

Kama tulivyokubaliana Kura asipate.

Ili iwe funzo Kwa Wasanii wa kizazi kinachokuja.

Msanii ambaye ni kioo cha jamii badala aungane na jamii yeye anaungana na serikali. Ajabu hii.
Hii ipo katika nchi yetu pekee.

Hata Marekani wenye muziki wao Wasanii wao huwa upande wa wananchi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Miziki yake tutacheza lakini kura nooo 😁😁😁
 
CCM (Ya Dr Bashiru na Prof Polepole) aliokua anawapigia campaign wampitishe bila kupingwa BET AWARDS. Wamehitimu Shahada ya kuiba kura.

Binafsi, Diamond angekua anachuana kwenye hizo tuzo na "FUNGU LA MAVI", basi ningelipigia kura hilo fungu la mavi, ila sio huyo jamaa. Hatetei jamii wala chochote kwa taifa letu, ila anataka yeye atatetewe;

1) Ana dhalilisha wanawake (Kujaza mimba na kuwaacha), as if yeye ndio rijali peke yake.

2) Akisaidia au kutoa msaada basi lazima ajitangaze, wakati mwenzake Alikiba anasomesha shule na kuwalea mayatima kibao na hajitangazi.

3) Hashughuliki kutetea vijana wasio na ajira kitaifa, waliosoma na hawana ajira. Ajira zake kwa vijana anatoa kwa anaowajua tu.

4) Hashughuliki na kutetea uvunjwaji wa haki za binaadamu, anajifanya hayupo kisiasa ila kwenye campaign anakua mstari wa mbele.

5) Hashughuliki na kupaza sauti juu ya uonevu unaofanywa na viongozi wa mikoa na wilaya.

6) Ana haribu jamii, hasa vijana, kuvaa hereni/vikuku n.k

7) Ana dharau kwa wazee, jinsi alivyomdharau na kumdhalilisha yule Mzee Abdul si jambo zuri. Hata kama sio baba yake mzazi, ila alivyomlea wakati mdogo ni tosha kwa yeye kumheshimu kama baba yake.
Umasikini wako haujasababushwa na Diamond
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mtu unaandika kwa uchungu hivi kisa kumuonea wivu mwanaume kutia mabint mimba?
 
wakati wa chaguzi sihuwa anawapigia kampeni CCM?? hao hao ndo wambebe, mimi nachinjilia mbaliiiii ebu leteni link nichinje mbulumundu
 
Ina maan kule PM hujaona au? [emoji23][emoji23][emoji23] wee jisahaulishe tyuuh haya bhana, ma fix zako hizo. Lol
Hamna kitu PM yangu. Niwekee hapa hapa basi chap halafu unaifuta. Labda PM yangu ina shida.
 
Huyo jamaa anachojua ni kufundisha watoto wa kiume kuvaa visuruali vya kubana, kutoboa masikio, kusuka rasta, kuimba matusi, kudhalilisha watoto wa kike, kusifia ngono na anasa! Hala lolote ni ujinga tu. Kizazi cha nyoka kitampa kura ila si Mimi aisee.
Avatar yako tu inaonyesha wewe ni kizazi cha nyoka. Basi kama ni tofauti basi we mwenzetu kizazi cha Sokwe[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Etii wapenda haki, my foot
Unayofanya we ndo mtenda haki au?
Kila mtu afanye yake, mi nampigia ashinde asishinde fresh tuu kwan Nini!

Acha chuki binafsi
Usiwe na hasira kura yako haiitajiki mkuu.
 
Sikuwahi kujua Kama na we jamaaa ni zero kiac hiki sasa Kwan siasa na mzik wap na wapi yani kijana ni hard worker lakina kisa eti ni ccm [emoji16][emoji16] kijana tutampigia kura na atapita hey burna ana msaada gani kwako mbon hata kiba, mmakonde , na wasanii almost wot walikua wanawapigia kapn ccm acha watu watafute feza na kuwakilish taifa we Kama hupig baki na uchaw wako .. komb lazim lirud nyumban m n chadema dam ila kwa hili la mkumbo w kigogo hampati mtu ...den hat akikosa utapt faida gani [emoji16][emoji16] we ni zeroooooo kam mbulula wengine

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 
Nachoshangaa wapenda haki hawana tatizo na wanamtetea Mama Samia ambaye ndiye alikuwa Makamu wa rais kwenye utawala dhalimu ila msani tu Diamond ndio analaumiwa kuwa alikuwa upande wa dhalimu na hajawahi kutumia nafasi yake kutetea jamii. Binafsi nashindwa kuelewa maana kama Makamu wa rais tu alishindwa hata kumkosoa kuonesha hakubaliani na Boss wake na tumesikia kauli zake kipindi cha kampeni ila yote hayo kasameheka, sasa sijui Diamond anapataje lawama?
 
Back
Top Bottom