Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

Ukiachana na hao kuku ambao mimi huwa hata siulizii ijapo hata bei tu,siku moja nilijipa kazi ya kuchunguza na kuangalia haya mayai yanayoitwa ya kuku wa kisasa,kwakweli sikuelewa kabisa.

Mayai karibia tray 85 huoni hata yai moja lenye uchafu hata kidogo?
Yai halina hata mchirizi wa damu,halina uchafu wa aina yoyote utadhani limechongwa na fundi selemala?

Hapana,kuna namna watu wanaitumia kupata haya mayai wala hayatokani na kuku hata hao sijui wa kisasa mimi nakataa,bila shaka Mchina anahusika hapa.
 
Siku zinazo kuja itakuwa hata ukitaka kupata ganja halisi, itakubidi upande Dar Express au Kilimanjaro Express ukachukue mwenyewe Arusha.

Kila kitu kimemuwa fake. Ku kuthibitisha wanao itwa Ku kuthibitisha wa kienyeji wana uzwa kwenye mabar wengi ni " Chotara"ambao nao pia watakuwa na madhara kama wa kizungu tu.

Hakuna namna zaidi ya kuanza kufuga hao kuku Sisi wenyewe.

Wafugaji wa kuku wa kienyeji toeni mbinu
Mbinu ya kudhibiti magonjwa ama mbinu za kuongeza uzao na madawa ya mitishamba

Kama ni magonjwa Kuna kideri
Kuna mafua pia Kuna ndui hii uathiri sana kuku wadogo,
Kuna taifod hii upelekea kuku kuarisha kinyesi cha njano ama kijani


Kiufupi swala la ufugaji kuku wa kienyeji changamoto zake ni kuibiwa mara Kwa mara sababu kubwa vile kuzurura ovyo Kwa kuchangamana hii pia upelekea kupata magonjwa ya mara Kwa mara lakin kama unawapatia madawa ya mitishamba kama mwarobain hii husaidia sana Kwa magonjwa ya kuhara, pia Kuna Alovera, majani ya mpapai hii usaidia sana kudhibiti baadhi ya magonjwa nyemelezi ya kuku kama kideri , mafua , kuhara n. K
Pia usafi wa mabanda ni muhimu
Chakula Bora pumba uduvi pindi wanapotoka asubuhi na jion wanaporudi zingatia pia maji yakutosha

Endelea kupitia comment zaid utajifunza kupitia wadau wengine wa ufugaji
 
😀😀..

Mkuu nikajua ganja, umenikumbusha mbali Sana, kipindi bado nipo chuo Kuna jamaa yangu alisafirisha Bangi debe 2 kutoka Arusha mpaka dar... Haikua hata biashara yake out of the blue tu alifanya ivo alijua akifika dar atapata mpunga, kufika akawa hajuani na mtu dar, nae kuogopa
Kuuzwa akanicheki, mimi hapo hata mambo ya Bangi siyajui Wala nini, ila pale maeneo ya mabibo hostels Kuna eneo korofi lilikua linaitwa ubanda pale Kila kitu haramu utapata, basi nikasogea pale nikacheki na mtu tukaenda kimara wakaelewana wakalipana nikapewa na mimi upambe maisha yakaendelea



Kesho jamaa aliyenunua Bangi kanifata geto analalamika "aisee jamaa unataka kuniharibia biashara yangu hapa mjini mi ntaishije"


Hapo nishaingia kiubaridi najua labda kashikwa, namuuliza kwani shida nini man?


Ndo ananiambia hii Bangi mliyonipa Kali Sana aisee wateja wangu wakichukua stiki asubuhi hawarudi tena wanakua wamesizi wakati hua nawauzia mpaka stiki tano Kwa siku yaani Kila baada ya masaa matatu mtu anarudi kuchukua stiki...



Jamaa ndo ananiambia Bangi Kali Sana sio nzuri Kwa biashara Bora uwauzie makapi makapi Kila baada ya muda wanakuja kuchukua nyingine wewe unafanya biashara....

Nikabaki nashangaa
Hiyo itakuwa Ile Bangi yenye Nta Kwa nyuma wenyewe wanaita

" pafu kunya pafu kujamba" Ile ni noma mkuu😆
 
Siku zinazo kuja itakuwa hata ukitaka kupata ganja halisi, itakubidi upande Dar Express au Kilimanjaro Express ukachukue mwenyewe Arusha.

Kila kitu kimemuwa fake. Ku kuthibitisha wanao itwa Ku kuthibitisha wa kienyeji wana uzwa kwenye mabar wengi ni " Chotara"ambao nao pia watakuwa na madhara kama wa kizungu tu.

Hakuna namna zaidi ya kuanza kufuga hao kuku Sisi wenyewe.

Wafugaji wa kuku wa kienyeji toeni mbinu
Njoo magetoni nikupe mbuni za ufugaji wa kuku wa kienyeji
 
Siku zinazo kuja itakuwa hata ukitaka kupata ganja halisi, itakubidi upande Dar Express au Kilimanjaro Express ukachukue mwenyewe Arusha.

Kila kitu kimemuwa fake. Ku kuthibitisha wanao itwa Ku kuthibitisha wa kienyeji wana uzwa kwenye mabar wengi ni " Chotara"ambao nao pia watakuwa na madhara kama wa kizungu tu.

Hakuna namna zaidi ya kuanza kufuga hao kuku Sisi wenyewe.

Wafugaji wa kuku wa kienyeji toeni mbinu
Hata mahindi Lima mwenyewe ya chakula,mboga za majani Lima mwenyewe,hifadhi mbegu za kienyeji, Kwa wale watu wa Imani nadhani wanaelewa tushatahadharishwa ,Lima, fuga no way
 
Ha haa huyo sadali wa ganja anawauzia ma famfa

Ila sishangai kwa Dar ila huku tunakula og tu
Ukimuuzia mtu famfa harudi tena!
 
Back
Top Bottom