Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

Siku zinazo kuja itakuwa hata ukitaka kupata ganja halisi, itakubidi upande Dar Express au Kilimanjaro Express ukachukue mwenyewe Arusha.

Kila kitu kimemuwa fake. Hata hawa wanao itwa Kuku wa kienyeji wana uzwa kwenye mabar wengi ni " Chotara"ambao nao pia watakuwa na madhara kama wa kizungu tu.

Hakuna namna zaidi ya kuanza kufuga hao kuku Sisi wenyewe.

Wafugaji wa kuku wa kienyeji toeni mbinu
Mkuu badirika kidogo. Huyu kuku bloiler anakuwa wa kisasa kwa kulishwa tu vyakula mashudu na dawa. Ukimuwacha akae nje ale mwenyewe nyama yake inakuwa sawa na ndege kuku wote. Anakuwa amekula madini, vitamini , protini ya wadudu.
Conversely, iwapo utamchukua kuku wa kienyeji pure ukamuweka kwenye banda ukamlisha sawa na bloiler atakuwa kwa haraka na nyama yake haita fanana na ya kienyeji japo itakuwa nafuu.
Kuhusu kuju pure wa kienyeji wameisha baki wachache sana vijijini, wengi wame cross na majogoo ya saso, kloiler nk.
Hivyo ni sahihi ni ngupu kupata kuku pure wa kienyeji.
Hata binadamu nao kumpata pure wa kabila flani mjini ni ngumu, wengi wameishachanganyana makabila mbalimbali na mataifa mbalimbali, miaka ijayo tutakuwa na machotara wengi wa kichina.
Tukubaliane na wakati, karibu kijijini walau tunapata pata vitu pure kidogo.
 
Kwa ninavyojua, kuku wa kienyeji na wale wanataga mayai madogoo alafu meupe pe!. Na kuwapata wale kuku mjini ni kipengele hadi vijijini huko.
 
POTOSHI.
Hakuna madhara yoyote tofauti na story za kijiweni!

Kuku Chotara. maana yake ni mchanganyiko wa kuku aina 2 kutoka sehemu mbili tofauti na kutengeneza uzao wenye sifa anazozihitaji muhusika (mfugaji).

Mfano unaweza kuchukua kuku Aina ya kuchi (og) then ukapandikiza na kuku wa kienyeji hawa wa kawaida uzao utakao tokea si kuchi halisi wala si kienyeji asili hii kifaranga hicho ndo kitaitwa chotara.

Swali kuku huyu mwenye mchanganyiko wa kuchi na kienyeji atakuwa na shida/madhara gani kwa mtumiaji?

Jibu hakuna madhara yoyote.

Kuku wa nyama au mayai

Kuku wa nyama. Hawa wanafugwa mahususi kwa ajiri ya nyama tu (broiler) na wanaangaliwa kwa umakini mkubwa mno ili wakue kwa wakati hapo itakupasa wale masaa 24 wapewe Madawa yote muhimu ili wasipate changamoto yyte na wakadumaa.

Itakuwa uwalishe masaa24 tena chakula sitahiki na chenye lishe zote muhimu.

Kwanini wanaitwa wa kisasa au kizungu.

Ni vile wanavyotunzwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana maana hawahitaji changamoto yoyote hata iwe ya kimazingira tu wanaweza kuisha wote.

Mfano mtoto wa geti kali kamwe huwezi mlinganisha na mtoto wa kijijni huko kwanza mtoto wa geti kali kuna chakula hawezi kula kabisa na hata hajawahi kudhani hicho nacho ni chakula

Mtoto wa kijijini kule anaweza kula kitu chochote au kunywa maji yoyote bila kuugua hayo yote ni makuzi na malezi aliyolelewa na kukulia. Wa mjini akinywa maji ovyo muhimu ataharisha.

Madhara ya kuku wote hao iwe kienyeji,chotara au broiler yapo kwenye madawa wanayopewa.

Hii ipo kwenye mifugo yote iwe wanyama au ndege na ipo kwenye mazao yote pia.

Hii kila mmoja wetu ni shahidi.

Madawa mengi yanaonya kuhusu matumizi.

Chukulia dawa za mafua zinasema kuku anapotumia dawa angalau zipite siku3-7 ndo ule mayai/nyama yake hali kadharika kwenye wanyama unaambiwa pindi mnyama wako ukimtibu basi usile nyama wala kunywa maziwa yake kwa muda fulani.

Swali je ni nani anayejari? Nani yupo tyr ana kuku 1000 wanaotaga atupe mayai ya kuku wote hao tena kwa siku zote zile?

Jibu ni ngumu sana na hapo ndipo tunapopata madhara kiafya.....

USALAMA WAKO NA WATU WENGINE.

Kwa sasa ni ngumu sana kutoboa au kuepuka matumizi ya madawa huwezi kuwa na kuku 500 halafu hao kuku uwaendeshe bila madawa ya viwandani ni ngumu sana (sijui kwa wengine) kama unahitaji ufuge kwa ajiri ya kitoweo tu ni sawa inawezekana kuwafuga kwa mtindo huo.

Na kumbuka unapofikia idadi hiyo maana yake unafuga kibiashara sasa huwezi kukubali upate hasara zaidi ya m7 kwa kutokutumia dawa za kiwandani.

Mfano mwingine ni kwenye mazao

Mara nyingi viuatilifu vinasema Baada ya kupurizia madawa shambani itakupasa usubiri zaidi ya siku14 ndo uanze kutumia kwa matumizi ya chakula.

Jiulize mazao kama nyanya,Tango, Chinese nk kwa hakika huwezi subri wiki2 ndo uvune haiwezekani.

Hitimisho kuku hawana madhara kama wanavyosemwa madhara yapo kwenye madawa wanayo tumia.

Carleen
Hii reply ilipaswa kuwa uzi kamili.
Umemaliza kila kitu kiongozi
 
Ndo ananiambia hii Bangi mliyonipa Kali Sana aisee wateja wangu wakichukua stiki asubuhi hawarudi tena wanakua wamesizi wakati hua nawauzia mpaka stiki tano Kwa siku yaani Kila baada ya masaa matatu mtu anarudi kuchukua stiki...
  • Hii hatari.
  • Ila kwenye kuku wa kisasa ni hatari zaidi.
 
Mkuu badirika kidogo. Huyu kuku bloiler anakuwa wa kisasa kwa kulishwa tu vyakula mashudu na dawa. Ukimuwacha akae nje ale mwenyewe nyama yake inakuwa sawa na ndege kuku wote. Anakuwa amekula madini, vitamini , protini ya wadudu.
Conversely, iwapo utamchukua kuku wa kienyeji pure ukamuweka kwenye banda ukamlisha sawa na bloiler atakuwa kwa haraka na nyama yake haita fanana na ya kienyeji japo itakuwa nafuu.
Kuhusu kuju pure wa kienyeji wameisha baki wachache sana vijijini, wengi wame cross na majogoo ya saso, kloiler nk.
Hivyo ni sahihi ni ngupu kupata kuku pure wa kienyeji.
Hata binadamu nao kumpata pure wa kabila flani mjini ni ngumu, wengi wameishachanganyana makabila mbalimbali na mataifa mbalimbali, miaka ijayo tutakuwa na machotara wengi wa kichina.
Tukubaliane na wakati, karibu kijijini walau tunapata pata vitu pure kidogo.
Sio kweli
 
Siku zinazo kuja itakuwa hata ukitaka kupata ganja halisi, itakubidi upande Dar Express au Kilimanjaro Express ukachukue mwenyewe Arusha.

Kila kitu kimemuwa fake. Hata hawa wanao itwa Kuku wa kienyeji wana uzwa kwenye mabar wengi ni " Chotara"ambao nao pia watakuwa na madhara kama wa kizungu tu.

Hakuna namna zaidi ya kuanza kufuga hao kuku Sisi wenyewe.

Wafugaji wa kuku wa kienyeji toeni mbinu
Mi nakula bata. Wajanja hawajaistukia hii sekta. Nawafuata mwenyewe Bagamoyo kwa wafugaji namwambia "mlowe yule dimbwini..."
 
Back
Top Bottom