Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

Arusha itakuwa ni strain ya indica ndiyo ukipiga na jua la Dar unasizi,mwana wa wa Dar atakuwa alikuwa na sativa ndiyo ukivuta unahitaji msokoto mwingine inakufanya unakuwa active.
 
Ni ujinga tu wa watu.
 
Ndio maana siku hizi navuta ganja gram nzima lakini sisikii chochote. Kumbe wahuni wameshaingia hadi huku.
 
Wale wa katika Bar zetu ni kuku wa kisasa wa mayai sio wa kienyeji.
 
 
Acha Bangi
Bangi inahusianaje na UFUGAJI WA KUKU?
 
unakula kuku ili upate nini?ukishalijua hilo kuku wote ni sawa ndugu

akuna mfugaji msomi atayefuga kuku kibiashara na kuwaeka kienyeji itakua huyo shule haijamsaidia,mbinu na mbegu bora ndio zao la kuku chotara wakiwa na ubora na faida zaidi ya hao unaowaita wakienyeji ambao ni zao la mbegu duni
 
Mkuu siku moja jaribu kutembelea mabanda ya wafugaji wakubwa wa kuku ukajionee acha kukariri vitu vya mitandaon, we unadhani keji kama hiyo hayo mavi yatakaa muda gani kwenye mayai?
 
Nikifa MkeWangu Asiolewe naomba busara zako hapa tafadhali ndugu yangu..!
POTOSHI.
Hakuna madhara yoyote tofauti na story za kijiweni!

Kuku Chotara. maana yake ni mchanganyiko wa kuku aina 2 kutoka sehemu mbili tofauti na kutengeneza uzao wenye sifa anazozihitaji muhusika (mfugaji).

Mfano unaweza kuchukua kuku Aina ya kuchi (og) then ukapandikiza na kuku wa kienyeji hawa wa kawaida uzao utakao tokea si kuchi halisi wala si kienyeji asili hii kifaranga hicho ndo kitaitwa chotara.

Swali kuku huyu mwenye mchanganyiko wa kuchi na kienyeji atakuwa na shida/madhara gani kwa mtumiaji?

Jibu hakuna madhara yoyote.

Kuku wa nyama au mayai

Kuku wa nyama. Hawa wanafugwa mahususi kwa ajiri ya nyama tu (broiler) na wanaangaliwa kwa umakini mkubwa mno ili wakue kwa wakati hapo itakupasa wale masaa 24 wapewe Madawa yote muhimu ili wasipate changamoto yyte na wakadumaa.

Itakuwa uwalishe masaa24 tena chakula sitahiki na chenye lishe zote muhimu.

Kwanini wanaitwa wa kisasa au kizungu.

Ni vile wanavyotunzwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana maana hawahitaji changamoto yoyote hata iwe ya kimazingira tu wanaweza kuisha wote.

Mfano mtoto wa geti kali kamwe huwezi mlinganisha na mtoto wa kijijni huko kwanza mtoto wa geti kali kuna chakula hawezi kula kabisa na hata hajawahi kudhani hicho nacho ni chakula

Mtoto wa kijijini kule anaweza kula kitu chochote au kunywa maji yoyote bila kuugua hayo yote ni makuzi na malezi aliyolelewa na kukulia. Wa mjini akinywa maji ovyo muhimu ataharisha.

Madhara ya kuku wote hao iwe kienyeji,chotara au broiler yapo kwenye madawa wanayopewa.

Hii ipo kwenye mifugo yote iwe wanyama au ndege na ipo kwenye mazao yote pia.

Hii kila mmoja wetu ni shahidi.

Madawa mengi yanaonya kuhusu matumizi.

Chukulia dawa za mafua zinasema kuku anapotumia dawa angalau zipite siku3-7 ndo ule mayai/nyama yake hali kadharika kwenye wanyama unaambiwa pindi mnyama wako ukimtibu basi usile nyama wala kunywa maziwa yake kwa muda fulani.

Swali je ni nani anayejari? Nani yupo tyr ana kuku 1000 wanaotaga atupe mayai ya kuku wote hao tena kwa siku zote zile?

Jibu ni ngumu sana na hapo ndipo tunapopata madhara kiafya.....

USALAMA WAKO NA WATU WENGINE.

Kwa sasa ni ngumu sana kutoboa au kuepuka matumizi ya madawa huwezi kuwa na kuku 500 halafu hao kuku uwaendeshe bila madawa ya viwandani ni ngumu sana (sijui kwa wengine) kama unahitaji ufuge kwa ajiri ya kitoweo tu ni sawa inawezekana kuwafuga kwa mtindo huo.

Na kumbuka unapofikia idadi hiyo maana yake unafuga kibiashara sasa huwezi kukubali upate hasara zaidi ya m7 kwa kutokutumia dawa za kiwandani.

Mfano mwingine ni kwenye mazao

Mara nyingi viuatilifu vinasema Baada ya kupurizia madawa shambani itakupasa usubiri zaidi ya siku14 ndo uanze kutumia kwa matumizi ya chakula.

Jiulize mazao kama nyanya,Tango, Chinese nk kwa hakika huwezi subri wiki2 ndo uvune haiwezekani.

Hitimisho kuku hawana madhara kama wanavyosemwa madhara yapo kwenye madawa wanayo tumia.

Carleen
 
JIBU ZURI SAAANA, CHA KUMALIZIA MWANDISHI AWE ANAPELELEZA KWANZA KABLA YA KUPOST VITU POTOSHI.
 
Madhara yepi?....tudadavulie kwa takwimu na vyanzo vya kuaminika.
Yaan andika kiripot chako kikae kisayansi mfn:
Mwaka XXX watu ABC walipatwa na ATQ baada ya kula mayai/nyama za kuku toka kwa mfugaji ABC. Uchunguzi wa kina ulipofanyika iligunduliwa madhara haya waliyapata kutokana na XXX katika nyama za kuku waliokula,(unaweka na chanzo chako).
Vinginevyo itakua unatangaza habari potoshi kwa maslahi ya kwako.
Kwa kumalizia.....vita vya biashara vipo vikubwa saana, wa ng'ombe atasema kuku mbaya, wa kuku atasema samaki ana kemilali XXX, wa samaki atasema Nguruwe ana tatizo XXX. Kiufupi, madhara ama faida mtu atapata kulingana na utunzwaji wa mfugo husika( kama mfugo ulifugwa pasipo kuzingatia kanuni za afya basi madhara kwa mlaji atapata na kinyume chake).
 
madawa ya mitishamba kama mwarobain hii husaidia sana Kwa magonjwa ya kuhara, pia Kuna Alovera, majani ya mpapai hii usaidia sana kudhibiti baadhi ya magonjwa nyemelezi ya kuku kama kideri , mafua , kuhara n. K
Hayo majani ya mwarobaini, Aloe Vera na majani ya mpapai, unawapatia kuku kama yalivyo ama unayachemsha kisha unawapatia maji yake, au unayafanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…