Wapenzi wa nyama ya kuku inabidi tuanze kufuga wenyewe

JIBU ZURI SAAANA, CHA KUMALIZIA MWANDISHI AWE ANAPELELEZA KWANZA KABLA YA KUPOST VITU POTOSHI.
Uko sahihi. Watu wanadanganyana na vile watanzania wepesi kuamini maneno ya kijiweni na ni wepesi pia kuyasambaza.

Kuku kama broiler anakula kama mchwa masaa24 akishiba analala hapohapo kwenye combo cha chakula na kunya atakunya hapohapo wewe unategemea asikue haraka.
 
Hayo majani ya mwarobaini, Aloe Vera na majani ya mpapai, unawapatia kuku kama yalivyo ama unayachemsha kisha unawapatia maji yake, au unayafanyaje?
Miti shamba si ya kuipa kipaumbele sana kama unafuga kibiashara utalia kilio kikuu.

Hayo kama alivyotaja hapo

Maandalizi yake.

Alovera.

Chukua majani yake katakata vidogovidogo sana au saga na blenda au pondaponda kisha loweka mfano mimi majani 3 ya makubwa ya aloveea huwa naweka kwenye maji lita10 wengine zaidi ya lita10 yazidi yasizidi hayana madhara.

Majani ya mpapai fanya vilevile kipimo.maalumu huwa ni kukisia tu hayana madhara.
 
Hawezi kukupa ushahidi ya madhara. Wa Tanzania tumezoeshwa kulishwa nadharia za ajabu sana,kama mtu nmeona anasema mayai ya layers ni yanatengenezwa na mchina kisa masafi hayana uchafu wowote mtu kama huyo utamueleza nini. Kama ushahidi wa u fake wa mayai anasema ni masafi sana,inaonesha hata ukitamka cages ni neno geni.

Kuku wa kisasa na chotara wana madhara yapi ayaseme angalau matatu,hana ushahidi.
 
Watanzania ni wajinga mno mno mno awe amesoma au hajasoma ni wachache sana tulio vuka stage ya kulishwa matango poli.

Ukifuga kuku kienyeji kwa mtindo wa kuku wa nyama ndani ya miezi3-4 unachinja unakula.

Sasa mfuge kienyeji sasa umwache ajitafutie chakula atatoboa miezi7 hajafika kuchinjwa niko hapa!
 
Asante sana
 
Wewe hata tukushauri tukiwa uchi wa mnyama huwezi kutuelewa hili nalo tumwachie Mungu tu.
 
Mkuu tunashukuru sana. Nataka kushauri kibiashara usijikite sana kwenye tiba za kienyeji.

Pia kwa ufugaji bora kabisa fuga Nusu huria. Hii itawasaidia kuku wasiende huko na kule.
 
Hata mahindi Lima mwenyewe ya chakula,mboga za majani Lima mwenyewe,hifadhi mbegu za kienyeji, Kwa wale watu wa Imani nadhani wanaelewa tushatahadharishwa ,Lima, fuga no way
Hutoboi.
Mahindi
Karanga
Nyanya
Mchicha
Tikitiki
Nyanya chungu
Tango
Malimao
Chungwa
Mpunga
Nk
Yote hayo utalima mwenyewe mkuu?
Nakufuga iwe samaki au wanyama utafuga mwenyewe?

Haiwezekani
 
Mkuu siku moja jaribu kutembelea mabanda ya wafugaji wakubwa wa kuku ukajionee acha kukariri vitu vya mitandaon, we unadhani keji kama hiyo hayo mavi yatakaa muda gani kwenye mayai?View attachment 3403627
Huyo hata usimame Posta ukiwa uchi kisha umueleze hatua kwa hatua hata kuelewa.

Licha ya hizo cage kuku akitaga kwenye mapumba ya munga yai linakuwa jeupe au safi kama malaika.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚Mi hapa %90 viko nyumbani nachuma
Mkuu inatakiwa jamii au nusu ya wanajamii warudie asili yao kwa mtu mmoja tu huwezi.

Ulime mihogo,dengu,njugu mawe,nanas,miwa ufuge nyuki sijui hata machine ya kusagia unga wako uwe nayo mwenyewe ili unga wako og usichanganyikane na unga wa mahindi ya kisasa je utatoboa?
 
Ni sahihi Kila mtu Kwa sehemu yake arudie asili
 
Mungu akubariki mno mno kwa hii knowledge unayoitoa bure hapa..!!
you are the best..!πŸ™
 
Maelezo mazuri,wale vichwa ngumu pitieni hii post.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…