Wapi mnapata pesa za kujenga wandugu? Mbona kwangu naona chenga tu?

😀😀😀Hatari sana,endelea kupambana mkuu
 
Kila mtu anazama zake za kupata hela nyingi kumbe ni muhimu zama hizo zikitufika tutumie pesa vizuri na kuweka akiba
 

Inaendelea...
Niliishia hapa.
Nilipambana mabibo nikawa siunzi tena mifuko nikajiingiza kwenye UKULI.
Tuendelee..
Baada ya kuacha kuuza mifuko,nilijiingiza kwenye UKULI wa kubeba mizigo minzito,hiyo ilikuwa 2017 niliparangana sana ishu ikaja jinsi ya kuwahi sokoni maana magari yanaingia kwanzia saa 9 za usiku na sehemu napoishi ni ubungo kibangu juu ya kwa bondia, na sehemu hiyo kuna mbwa wengi sana.

Saa 9 usiku nilikuwa natoka kibangu nakimbia kwa miguu napishana na mbwa na mambo ya ajabu chungu mnzima,mbwa walikuwa wananikimbiza kila siku mpaka wakaanza kunizoea kila wakiona nakuja kwa mbali wanatanda barabarani zaidi ya mbwa 20 napita kati kati yao huku roho inaenda mbio,kuna siku kidogo nitafunwe na mbwa nilishambuliwa bahati nzuri nilibeba fimbo ndio iliyonisaidia maana walining'ata mguuni na mgongoni,nilipata majeraha sikuweza kufanya kazi kwa week moja maana niliumia mgongoni na miguuni ilijaa meno ya mbwa daah niliumia sana.

Ndani nilisave laki 8,nikaamua kuhama kibangu kwa kuwa nilikuwa sina chombo chochote cha ndani zaidi ya begi langu,nikanunua kitanda,godoro,sofa,jiko la gesi na vyombo vyote vya kupikia ila hivyo vitu nlinunua USED kwa mtu alikuwa anaviuza.
Nikaamia ubungo mwisho,basi nikawa karibu na soko la mabibo hiyo ilikuwa 2018 nilifanya kazi kwa bidii nikajaza kila kitu ndani,yani ukiingia kwenye chumba changu utamani kutoka gheto la maana.

Katika kufanya kazi sokoni,kuna Dada alitokea kunikubali(sio kimapenzi),na kuniamini akawa ananitumia pesa nimnunulie vitu vya hotelini,kweli nilifanya naye kazi kwa uaminifu sana hata kazi za UKULI nkaanza kupunguza.
Ndani ya miezi sita nilisave ndani million 2 nikaamua kufungua library ya movies,baada ya kufungua library nikaacha kazi ya ukuli rasmi mwishoni mwa mwaka 2018.

Ila sokoni nikawa naenda kwa ajili ya kumnunulia yule Dada vitu vya hotelini,baada ya kumnunulia narudi zangu nafungua library yangu kweli maisha yakaanza kubadilika.

Kimbembe kilianza pale nilipokutana na huyu mwanamke...
 

Kumbe wale jamaa wakataa ndoa huwa wapi sahihi.
Eeh! Huyo mwanamke alikuja na nuksi zipi….
 
endelea mkuu, ili tuupe ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…