Wapi nikatafute maisha kati ya Botswana, Mauritius,Namibia au Sychelles?

Kama umechoka na maisha ya bongo ninakushauri katika nchi ulizozitaja bora uende nchini Botswana katika nchi za bara Asia nenda Japan au South Korea Au brunei..
Katika nchi za Bara la ulaya nenda ireland au Sweden, au Ujerumani, au Switzerland, au Belgium Au Kanada au Australia
Nipe Tarehe uliyozaliwa na mwezi wako nipate kukupa ushauri wa nchi gani ya dunia inayo kufaa kwenda kuishi na kuweza kufanikiwa kimaisha
 
Hapana nilishatoka nilikuwa naenda Canada pale nilikaa kwa mda kidogo alafu wanawake wa kule wanavaa nguo fupi na ni walevi
Mkuu inaonekana unauelewa na hiyo nchi, sio mbaya ukawapa vijana muongozo huu

1. Uliwahi kukaa kwa muda gani na ilikuwa mwaka gani huo?

2. Taratibu za kuishi kule zipoje kwa maana ya vibali kwa wageni, mfano uki "over stay" huwezi kusumbuliwa na migrations?

3. Utamaduni wao kwa ufupi upoje? Mfano vyakula vyao vikuu nk....

4. Niliwahi kusikia ukiwa mgeni lazima ujulikane sababu wao wapo wachache hivyo ni rahisi kufahamika. Je ni kweli?

5. Je unaweza kufanya kazi hizi unskilled bila ya kuwa na kibali?


Ni hayo mkuu lakini kama kuna mengine unaweza kujazia wengi wakapata kuifahamu zaidi hiyo nchi. Asante
 
Sorry mkuu...kama una uhakika maeneo uliyotaja ndipo yalipo maisha kwanini tusiombe serikali yetu tukufu kupitia wizara ya mambo ya nje isiyafuate hayo maisha ituletee hapa nyumbani?
 
Una ujuzi gani kama ni daktari wa binadamu Botswana kutakufaa, mimi nilienda zamani 1991 nilifika hadi mji unaoitwa Kanye, ipo hospitali inaitwa Kanye hospital ya Adventist, (wasabato), shemeji yangu alikuwa anafanya kazi hapo, nilipita hapo nikielekea south Africa
 
Nenda botswana mtafute huyo mtu +26773647948 atakusaidia sana ni m tz au mtafute ecureui sethora motsholele (huyu mbotswana) kwenye facebook bonge la mtu wewe tu jinsi utakavyointerack naye
Mkuu hii haiwezi kumletea shida mwenye namba yake kwa kuiweka hapa? Au haina shida? Maana asije kushangaa anatafutwa na msururu wa watu akajiuliza imekuwaje wamepata namba yake!
 
Kuwa Mzalendo, endelea kuyatafuta nchini mwako usaidie kuijenga nchi kama wenzenu walivyojenga kwao.
 
Pamoja na yote umtangulize Mungu na uwe mvumilivu na mwenye subira kwa kila hatua uipitayo na nidhamu ya fedha/kipato utakacho jaaliwa hapo utatoboa.
 
Mauritius watu wapo poa sana nimeshafanya auditing miezi 9 nili enjoy sana
 
Nenda botswana mtafute huyo mtu +26773647948 atakusaidia sana ni m tz au mtafute ecureui sethora motsholele (huyu mbotswana) kwenye facebook bonge la mtu wewe tu jinsi utakavyointerack naye

Mkuu hii haiwezi kumletea shida mwenye namba yake kwa kuiweka hapa? Au haina shida? Maana asije kushangaa anatafutwa na msururu wa watu akajiuliza imekuwaje wamepata namba yake!
Sio vizuri kusumbua watu yaani unaanzajeanzaje kumsumbua mtu hiyo ni namba ya kweli mt yupo botswana ukiwa huko anaweza kuwa na msaada anapatikana gaborone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…