Wapi nitapata kazi ya malipo ya 5000 kwa siku?

Wapi nitapata kazi ya malipo ya 5000 kwa siku?

Huu Uzi Umenikumbusha Ilikuwa Mwaka Wa Kwanza Nimemaliza Field Nikajiuliza Nirudi Mkoani Au Nibaki Mjini Nitafute Kazi Nifanye.

Nikashauriana Na Mshikaji Wangu Baadae Akasema Amesikia Kuna Sehemu Per Day 10000/= Tukajazana Tukasema Mjini Kupata Kazi Rahisi Sana Yaani Mkoani Unapewa Shamba Kubwa au Kufwatua Tofali Unapata Pesa Ndogo, Ila Dar Kazi 10000. Tukasema Ndio Maana Wanasema Kuwa Ni Wanaume Wa Dar.

Eeh! Bana Eeh! Tumeenda Kwenye Kazi Kumbe Chakula Wanakata Hapo Hapo 3000 Inabaki 7000 . Tulifanya Kazi Hadi Jioni Tunategemea Kupewa Hiyo Buku Saba, Kumbe Hupewi Siku Hiyo Hiyo Unapewa Siku Inayofata Ili Usikimbie Kazi Siku Inayofata Maana Ile Kazi Ilikuwa Ya Kutumia Nguvu Sana Kwahiyo Hadi Jioni Mnakuwa Mmechoka Sana.

Ile Siku Usiku Niliona Thamani Ya Boom Kwa Kipindi Kile Ilikuwa Sijui 5000/7000 Kwa Siku Nikasema Serikali Inatupa Kiasi Kikubwa Sana Kisa Kuingia Darasani Tu.

Jamaa Yangu Alivunjika Shingo Kutokana Na Ile Kazi Ikabidi Ku_postpone.

Toka Siku Ile Huu Mji Niliheshimu.

Pole Sana Mkuu Na Imani Mungu Atajalia Utapata Kazi Maana Mambo Yote Duniani Yanatokea Kwa Muda.

Keep moving & striving.
 
Back
Top Bottom