Wapi nitapata mganga wa Kienyeji mzuri?

Wapi nitapata mganga wa Kienyeji mzuri?

Nimeeka haya maelekezo kwa kumsaidia mtoa mada na wala sifanyi biashara wala kumpigia mganga yeyote promo, naomba muhusika kama atafanikiwa kwenda huko aje alete mrejesho na awape na wengine kwa faida yao, nitabeba dhambi moja, dhambi zingine jibebesheni wenyewe kwa wenyewe.
Mkuu nitumie mawasiliano ya watu wa lugulu maana naona umefunga pm
 
Kwanini usimchukue huyo wa kwako wa nyamadoke ambaye kwa uhakika sio mganga wa ukweli ni mganga wa michongo namfaham mana ana mpaka ukurasa wa facebook, uongo kweli
Kijana wa miaka 30-40 aiijue fb na yuko town, hahaha.you must be kidding...

halafu msiwachukulie watu washamba shamba hivi.

kuwa fb ni sehem ya social interaction
 
Kama uko serious tafuta usafiri wa toka hapo ulipo uende mpaka simiyu(bariadi mjini),kama utakua unatokea upande wa mwanza utashuka stendi ya somanda ama bariadi mjini, utapanda boda mpaka lugulu kwa buku tano na kama unatokea shinyanga utawaambia wakushushe lugulu. Baada ya hapo kuna kama vijiji viwili sijavishika jina(kama uko serious)utanifata PM nitakupatia namba za wenyeji watakaokupokea na kukupeleka eneo husika..
Mtaalam sio mzee ni kijana mwenye weledi na hataki pesa yako zaidi ya elfu mbili(2000)kabla ya kukuganga.malipo yake ni ahadi tu baada ya kufanikiwa utarudi kutoa shukrani.

Mkuu mambo unayotaka kuyajaribu uwe na moyo.
Pm kuko locked mkuu
 
Ndugu kwema
Nimemkumbuka pia mganga wa pale Ukerewe, alimrudishia jamaa bida zake zilizoibiwa, aliwapa watu wapige kazi boda mpya 3 alafu wao wakajiona masonko wakatoroka nazo kila mtu akahama mkoa, kilichofuatia kila mmoja wao anakuja mbio kutoka huko alikokuwa anapiga mwano anamtafuta mwenye boda na kuangukia pale pale anakata moto[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nipo hapa kwa Mwamposya. Watu wametoka Mikoani. Wengine wametoka nje ya nchi.
Mwamposya anawatibu sasa. Anawagusa mmoja mmoja. Mstari mrefu wa watu. Wamesimama shoulder to shoulder mstari wa 100 metres.
Hiyo ni awamu ya kwanza. Sasa awamu ya pili inaambiwa ijitayarishe.
 
Unaweza toa namba hapa kumbe wewe ndio Wanted!! Hapana Aisee....
 
Watoto wawili wenye umri wa miaka miwili na miaka 7, Wakazi wa Kata ya Shabaka Wilayani Nyangwale Mkoani Geita wameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana, kisha miili yao kutupwa shambani.

Mperwa Sahani, mama mzazi wa mmoja wa watoto hao amesema: “Nilimkuta mtoto wangu amelala chali akiwa amekatwa shingo, nikambeba hivyohivyo hadi nyumbani kisha ndiyo nikatoa taarifa.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema: “Tunamshikilia mganga wa kienyeji, mfanyabiashara na kikongwe mmoja na upelelezi unaendelea.”

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom