Umekosea, haikuwa hivyo.
Kikosi cha kwanza kabisa cha Urusi kilikuwa cha elites, wale top cream kabisa, ambao walitarajiwa kuliangamiza jeshi la Ukraine ndani ya siku 2. Kikosi hiki kilipigwa vibaya sana na kupoteza askari wengi, hadi kulazimika kuukimbia mji mkuu wa Kyiv ambao ndio uliolengwa na shambulio la awali.
Baada ya hapo wakaenda mashariki mwa Ukraine, wakitumia wanajeshi wa kawaida wakiongozwa na makamanda wazoefu, bahati mbaya matokeo hayakuwa mazuri kwa Urusi. Askari wengi waliuawa, mpaka makamanda wakuu waliuawa, hali iliyotajwa kuwa ilichangiwa sana na kukosa morali kwa wanajeshi hao wa Urusi. Baada ya hapo Putin ndiyo akaamua kuwaajiri kikosi cha wapiganaji wa kulipwa Wagner, na wakati huo huo akipitisha sheria ya watu kupelekwa vitani kwa lazima. Vijana wengi wakaikimbia nchi. Waliobakia wakapelekwa jeshini kwa nguvu. Wananchi hawa waliogeuzwa kuwa askari baada ya kupewa mafunzo ya miezi 2, wengi wao waliangamia. Ndipo Putin akaja na mpango wa kuwatumia wafungwa, nao wengi wao waliuawa, akiwemo kijana mtanzania aliyeenda masomoni, kisha akafungwa jela, akapewa offer ya kuachiwa kama ataenda frontline na kupigana kwa miezi 6. Miezi 6 haikufika, akauawa. Wa namna hiyo walikuwa wengi.
Ni ukweli kuwa Urusi ina wakati mgumu, inataka iwe na askari wengi frontline, huku ikiwa na wasiwasi kuwa ikiwapeleka askari wake wote, halafu wengi wakafa, je vita ikiingia nchini mwake atafanyaje!! Ndiyo maana Urusi inalazimika kuwabakiza wengine wasiguse vita kabisa, wakisubiria kama vita itaingia ndani ya nchi yao.
A number of Russian
general officers[a] have been
killed during the
Russian invasion of Ukraine. As of 7 November 2024,
Ukrainian sources claimed that 18
Russian generals and 1
admiral had been killed during the invasion, while Russian sources have confirmed 8 deaths. Although seven of the Ukrainian claims were rebutted, the loss of even two general officers is rare. The scale of these losses is unprecedented since the
Second Chechen War, in which Russia lost ten generals.
[